Wanaosema kazi au ajira hakuna, tuambieni mnataka kazi zipi?


hahah unaamini commnunist propaganda? tanzagiza wanahesabu dada mtembeza matembele, muuza mboga, mchoma mahindi barabarani, boda boda, mama ntilie, wapiga debe, machinga wote hao wanahesabu ni ajira.

ajira maana yake mwajiriwa analipwa mshahara pamoja na kukatwa paye i.e kodi kwenye mshahara na nssf, wanaokatwa hivyo ndiyo waliojiriwa, the rest ni ajira iisiyo rasmi, sasa ajira isiyo rasmi siyo uchumi.

sasa piga hesabu watu waliojiriwa tanzagiza na kulipwa mshara ambao unakatwa kodi na nssf ni asilimia ngapi ndiyo utapata namba halisi ya unemployed tanzagiza ...
 
Tupo ulimwengu wa kiberi na si ujamaa
 
Elimu kubwa namna hii unampa kijana anayebeti hakuelewi.
 
Kila mtu anatamani akiamka asubuhi viatu vimepakwa rangi, shati na suruali vimenyooshwa vizuri, gari inanguruma nje kumsubiri kwenda "ofisini"!

Mengine tunaishi kwa sababu ni matokeo, sio uchaguzi. Wachache wanafanya kile walichoota wakiwa wadogo.
 
lete takwimu
 
Elimu kubwa namna hii unampa kijana anayebeti hakuelewi.

yeah wanadanganywa sana na hao walioshikilia power, kwa hali ya kawaida serikali wanapaswa kuwajibika kwa kushindwa kuzalisha au kuweka mazingira ya kutengenzea ajira, lkn kwa kuwa serikali hawataki kuwa responsible wanajitoa na kuruhusu bodaboda halafu wanasema boda boda ni ajira ...
 
Kwa ulimwengu wa sasa wa ushindani wa mauzo, lazima kutumia mbinu zote za kuuza, hii ya kusubiri mteja dukani au ofisini ilishapitwa na wakati, lasivyo hutouza na utakosesha mapato kwa taasisi (biashara).​

yeah a lkn umuajiri kwa kumlipa mshara ambao unakatwa kodi (paye) na kumlipia nssf halafu ndiyo unaweza labda kuanza kuongelea khs ajira labda ...
 
Kila mtu anatamani akiamka asubuhi viatu vimepakwa rangi, shati na suruali vimenyooshwa vizuri, gari inanguruma nje kumsubiri kwenda "ofisini"!

Mengine tunaishi kwa sababu ni matokeo, sio uchaguzi. Wachache wanafanya kile walichoota wakiwa wadogo.
Tatizo nafasi ni chache, wahitaji ni wengi
 
So what, unasikilizaga ama kusoma hotuba za kiongozi akichaguliwa siku ya ufunguzi wa Bunge?
wewe ni nani anakwambia haya maneno ?
Utapuuzwa, penda kujisomea hata ukiolewa upate cha kumfunza mumeo aone nawe umo si vigodoro pekee.

Misleading Nigga!
Kwa ulimwengu wa sasa, hakuna viwanda vinavyomilikiwa na serikali 100% labda nchi za kikomunisti
 
Tunataka kazi ambazo tumesomea na kukaa darasani ,ingekuwa tunahitaji kutembeza vyombo tusingekopa Loan Board kuhenya miaka minne 4 ,miwili 6 na mitatu hadi 6 Chuo.
 
Hawa ambao wako mitandaoni wanapiga makelele kama ajira yao , leo wapo Marekani, Dubai, Uk n.k taasisi zao zinatambulika kisheria?
Wamejiajiri wanalipwa kulingana na followers wao mfano. Rachel Dangwa, Mange Kimambi, na kuna fala mwingine anajiita Kinepa hakuna cha maanaa wanachoongea zaidi ya kuropoka tu bila mpangilio. Kwahiyo wafuasi wao ndo misukule ya kuwaingizia pesa
 
Tunataka kazi ambazo tumesomea na kukaa darasani ,ingekuwa tunahitaji kutembeza vyombo tusingekopa Loan Board kuhenya miaka minne 4 ,miwili 6 na mitatu hadi 6 Chuo.
Wengi wameenda kusoma fani (rahisi) zisizohitajika sokoni; ukimuuliza kwa fani uliosoma, unaweza kutengeneza au kuvumbua nini, anakuwa hana jibu.
 
Wengi wameenda kusoma fani (rahisi) zisizohitajika sokoni; ukimuuliza kwa fani uliosoma, unaweza kutengeneza au kuvumbua nini, anakuwa hana jibu.
Issue ni mfumo ya elimu yetu ndiyo imewafanya wawe hivyo ,ilitakiwa ukimaliza form iv inaenda Technical/Vocationcal school/college kwa ajili ya kupata ujuzi ukimaliza technical unaingia chuo kwenye fani yako moja kwa moja kwa ajili ya ubobezi.

mtu aliyemaliza Technical/vocational anaweza kujiajiri.

SHule ziwe na elimu ya kuweza kujiajiri mf mtu akimaliza aweze kutengeneza keki/sabuni/kuunda mashine ,ushonaji ,elimu ya biashara/ujasiliamali ,elimu ya ubunifu ,elimu ya ujenzi ,uchongaji ,ushonaji ,elimu ya kilimo nk. Tukifanya hivyo kwa kubadili mitaala hakuna atakayelalamika ajira hakuna ila tukiendelea na elimu hii ya Panzi ana miguu mingapi au Juma anacheza mpira ,mama anapika wali ,swali je juma anacheza nini? Jibu Mpira TIKIIIIIII hatutoboi.
 
Mfano, wewe ungepewa wizara, ungeweza kubadilisha?
 
Maslayi madogo kazi ya tembo, mshahala wa sungura.
 
Ukishaelewa hivyo, amka asubuhi mshukuru Mungu wako halafu nenda kapige kazi, achana na ndoto za utotoni.
Bado watu hawajishughulishi wakisubiria hizo nafasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…