Wanaosema kazi au ajira hakuna, tuambieni mnataka kazi zipi?

Kwa ulimwengu wa sasa, hakuna viwanda vinavyomilikiwa na serikali 100% labda nchi za kikomunisti
Yes, vipo 185 vimekufa, ingieni ubia basi au unatetea tu hata upuuzi unaofanywa ?
Kiwanda cha nyama kimegeuzwa kanisa hapo Kawe, upo hapo ?
 
Watu binafsi wakijitokeza kwa kuandika barua na kuomba kutumia maeneo hayo kwa uzalishaji huku wakilipa kodi inawezekana. Swali, ni wangapi wanaweza kuzalisha wakipewa maeneo hayo?​
 
Nimeona matangazo mengi ya kuhitaji vijana kwa ajili ya kazi mbalimbali, mfano: kazi za masokoni, za majumbani, minadani, za kibiashara, kutembeza vyombo, nguo n.k, lakini waombaji hawaonekani.

Tatizo ni nini?

Ebu tuambieni ukweli, mnataka kazi gani?​
Wewe unatembeza nini? tuanzie hapo kwanza.
 
Nina vijiwe 20 vya mahindi ya kuchoma, kila kijiwe kinanipa faida ya 10,000 kwa siku; kwa mwezi naingiza milioni 6
Kama ni kweli umenifungua akili, inaweza kuwa biashara ya kawaida sana lakini ukapata pesa, ila unawezaje kupata vijana waaminifu wa kufanya nao kazi?
 
Ninachokumbuka cheti cha form 4 nilikichana maana niliona hakina maana na sikukosea kwa maisha nilionayo kweli hakikuwa na maana yeyote hapa ni kilimo mwanzo mwisho
 
Biashara ndogo ndogo zinalipa sana kama utakuwa na vijiwe vingi, na itakulipa sana kuliko yule mwenye biashara kubwa inayoonekana. Changamoto ni kuwapata wafanyakazi, kwa sababu wengi hawataki kuaibika.

Suluhisho, ni kwenda huko vijijini na kuwachukua wafanyakazi.​
 
Siku nguvu zikikuisha utaishije?
 
Mfano, wewe ungepewa wizara, ungeweza kubadilisha?
Kwa Waziri hawezi kubadilisha ,anayeweza kubadili mifumo ya mitaala ni Rais ...Rais akikubali ataunda jopo la wataalam wa kumshauri jinsi ya kufanya then ataishusha kwenye wizara ,wizara itaandaa bills kwenda bungeni kisha kubadili mfumo mzima.

Pia Rais ataingiza/atahidhinisha fedha kwenye kufanya implementation ya mifumo mizima.
 
Kwani hatuna tafiti zozote zile zinazoelezea changamoto za mfumo wa elimu tulionao na unaoshauri kuwepo na aina fulani ya mfumo?
 
Hatujapata Rais wa kufanya implementation ,mambo ya kusoma panzi ana miguu mingapi haina tija.

Sera/tafiti/maoni/mapendekezo yaliyopo kwenye makaratasi kabatini ni mazuri sana ila hakuna wa kuyatekeleza.
 
Biashara ndogo ndogo zinalipa sana kama utakuwa na vijiwe vingi, na itakulipa sana kuliko yule mwenye biashara kubwa inayoonekana. Changamoto ni kuwapata wafanyakazi, kwa sababu wengi hawataki kuaibika.

Suluhisho, ni kwenda huko vijijini na kuwachukua wafanyakazi.​
Kuna mtu namfahamu ni graduates yeye anafanya biashara ya utumbo, very smart.Nahisi itakuwa inamlipa vizuri.
 
Inaweza ikawa inamlipa kiasi au sana lakini kama utakuwa na viofisi/goli vingi, utakusanya zaidi, changamoto ni usimamizi.
 
Back
Top Bottom