Uchawi ni dhana potofu.
Ni vizuri watu wakajielimisha na kuacha upotoshaji.
Zamani watu walifanya matambiko wakiamini yatasaidia mvua kunyesha. Mvua zilinyesha si kwasababu tambiko lisababisha mvua kunyesha, kwani Mvua hunyesha kwa kufuata taratibu za kiasili (natural water cycle), hili lina uthibitisho wa kisayansi na mtu yeyote anaweza kuthibitisha.
Chumaulete ni dhana ya kichawi (kipotoshaji) ambayo ilikuja baada ya kugundulika kwa sarafu na noti, wakati dunia ílopokuwa kwenye nfumo wa barter trade dhana ya chumaulete haikuwepo. Hii inadhirishwa na utaratibu wa kimaisha wa jamii kama: wahadzabe, na piraha kwenye hizi jamii ambazo hawatumii pesa kabisa hakuna kitu kama chumaulete.
Wakati Academy za timu kama barcelona, man city, monaco, real madrid, nk, zinazalisha wachezaji wa mpira wa miguu kama pedri, foden, mbappe, hakimi. Huku Africa bado tunaamini kwamba uchawi unaweza kutumika kama nyenzo ya kutusaidia kwenye mashindano ya mpira wa miguu.
Yaani wakati nchi zilizoendelea zínawekeza kwenye Academy huku Africa watu wanaamini kwamba labda wazungu wanatumia uchawi mkubwa kuliko wao (Waafrika) ndio maana Timu za taifa za Afrika zinashindwa kufanikiwa kwenye .mashindano ya kombe la dunia.
Sayansi na Teknolojia ndio nyenzo pekee ambayo inaweza kutusaidia kujibu maswali magumu tunayoulizwa na mama-asili (Mother Nature).
Úchawi na Imani za kidini ni dhana potofu ambazo zinakwamisha maendelo ya ustawi katika jamii.