Wanaosema Vitabu vya Injili vina makosa/vinapingana — kwanini wanatumia muda mwingi kuvisoma?

Wanaosema Vitabu vya Injili vina makosa/vinapingana — kwanini wanatumia muda mwingi kuvisoma?

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Ni jambo la kushangaza sana kuona watu wanaosema kwamba vitabu vya Injili vina makosa, vimejaa contradiction, na haviaminiki — lakini hao hao ndio wanatumia muda wao mwingi kuvisoma, kuvichambua, na kunukuu mistari ya Injili.

Kama mtu haamini kitabu fulani, kwa nini anakisoma kwa bidii kila siku badala ya kukipuuza? Mtu anayesema Injili zimepotoshwa, lakini kila siku yuko ndani ya Mathayo, Luka, na Yohana akichambua mistari na kutunga hoja zake, hiyo ni nini kama sio dalili ya kuvutwa na Injili? Kama ni sumu, kwa nini anaendelea kuinywa kila siku? Kama ni upotevu, kwa nini kila siku yuko humo anachota hoja?

Injili ina nguvu ya kipekee ya kuwabadilisha hata wanaoipinga. Injili inaamsha dhamiri, inachoma mioyo yenye dhambi, na kuibua mapambano ya ndani kwa wale wanaoikana. Hiyo ndiyo sababu ya msingi inayowafanya wapinzani wa Injili waendelee kuisoma, hata kwa kisingizio cha kuikosoa.

Na mwisho wa siku, wale wanaoisoma kwa dhihaka mara nyingi huishia kuokolewa na Injili hiyo hiyo wanayoidharau. Ndivyo ilivyomtokea Sauli. Sauli(ambaye baadaye aliitwa Paulo) aliwapinga sana Wakristo na kupanga kuwatia gerezani, lakini baadaye akakutana na Yesu njiani — akabadilishwa, akawa Mtume anayetikisa watu wengi leo hii kwa Injili yenye nguvu. Hata humu humu, wanaoichambua Injili kwa dhihaka, watajikuta baadaye wamefunguliwa macho yao kiroho bila kutegemea. Hivyo tusishangae siku moja kusikia jenerali Covax amekuwa Mtume na kuanzisha kanisa lenye upako.

Nisisitize tena: kama kweli huiamini Injili — ipuuze kabisa kama anavyofanya Infropreneur. Lakini kama kila siku umo ndani ya Vitabu vya Injili, basi ujue tayari Injili imeanza kufanya kazi njema ndani yako. Muda si mrefu tutasikia umeokoka kama Mshana Jr ambaye mwanzoni alikuwa mpinzani wa Injili kwa kujihusisha na mambo ya uchawi, lakini sasa ameokoka. Haleluya!
 
Bila kusoma wangejuaje kama vina makosa ?
Kama wameishaona makosa mawili matatu, hakuna haja ya kuendelea kuvisoma. Isitoshe waliishashushiwa Kitabu kipya kilichoandikwa kusahihisha "makosa" ya Vitabu vya Injili. Hivyo ingependeza zaidi kama wangetumia muda mwingi kutuambia mazuri yaliyomo kwenye Kitabu hicho kipya
 
Kama wameishaona makosa mawili matatu, hakuna haja ya kuendelea kuvisoma. Isitoshe waliishashushiwa Kitabu kipya kilichoandikwa kusahihisha "makosa" ya Vitabu vya Injili. Hivyo ingependeza zaidi kama wangetumia muda mwingi kutuambia mazuri yaliyomo kwenye Kitabu hicho kipya

Sio injili tu vitabu vya dini zote vinakosolewa
 
BOnge la dada una mtu ?
Nina Yesu. Mimi ni bibi arusi wa Yesu. Nasubiri sherehe ya arusi. Nilitoa mwaliko humu, hujaupata?
 
Kwenye ule uzi mwingine wavaa kobasi tumewatusua sana mpaka wakawa wanajiuliza mbona hawa wakristo wanaujua uislamu sana

Zaman walikua wanatuweza kwasababu tulikua hatujui madudu yaliyojazana kwenye dini yao ashukuriwe mungu tukaingia madrasa, tukasoma nao, tukaishi nao bila kujua sisi wengine ni wakristo pure. Saiv tunawatusua balaa mpaka wanachanganyikiwa hawajui washike wapi na wapi wapaache pabomoke
 
Sasa utajuaje vina upuuzi bila kuvisoma?
Tumeambiwa kwamba wameshushiwa kitabu kipya, hicho kipya kimesahihisha makosa ya vitabu vya mwanzo(Taurat, Zabur na Injeel). Sasa kuna haja gani waendelee kusoma vitabu hivyo vilivyochakachuliwa?
Kwa kawaida kitabu kikifanyiwa marekebisho huwa kinaandikwa 2nd version au 3rd version. Ni ajabu kama utachagua kusoma 1st version wakati tayari kuna 3rd version.
 
Tumeambiwa kwamba wameshushiwa kitabu kipya, hicho kipya kimesahihisha makosa ya vitabu vya mwanzo(Taurat, Zabur na Injeel). Sasa kuna haja gani waendelee kusoma vitabu hivyo vilivyochakachuliwa?
Kwa kawaida kitabu kikifanyiwa marekebisho huwa kinaandikwa 2nd version au 3rd version. Ni ajabu kama utachagua kusoma 1st version wakati tayari kuna 3rd version.
Hakuna binadamu aliyeshushiwa kitabu,,, ndo maana siye walimwengu tunasoma edition zote..
 
asante kwamaada yako namimi nachangia hivi..
unacho kiona chakazi gani chamfaa mwezako, hivo kila mtu aheshimu cha mwingine.
ni aibu kubwa mtu mzima na madevu yake, mmama mzima na miziwa yake kuona hadithi alio ikariri yeye
nibora na inachekesha zaidi kuliko ya mwenzake.
 
Naomba ni copy na kufanya marekebisho kwa uliyoyandika kwa kubadilisha neno INJILI na kuweka QURAN na kubadilisha majina ya watu/wahusika ili kuendana na muktadha uliopo.

Ni jambo la kushangaza sana kuona watu wanaosema kwamba kitabu cha Quran kina makosa, kimejaa contradiction, na hakiaminiki — lakini hao hao ndio wanatumia muda wao mwingi kuisoma, kuichambua, na kunukuu mistari ya Quran.

Kama mtu haamini kitabu fulani, kwa nini anakisoma kwa bidii kila siku badala ya kukipuuza? Mtu anayesema Quran imepotoshwa, lakini kila siku yuko ndani ya Quran akichambua mistari na kutunga hoja zake, hiyo ni nini kama sio dalili ya kuvutwa na Quran? Kama ni sumu, kwa nini anaendelea kuinywa kila siku? Kama ni upotevu, kwa nini kila siku yuko humo anachota hoja?

Quran ina nguvu ya kipekee ya kuwabadilisha hata wanaoipinga. Quran inaamsha dhamiri, inachoma mioyo yenye dhambi, na kuibua mapambano ya ndani kwa wale wanaoikana. Hiyo ndiyo sababu ya msingi inayowafanya wapinzani wa Quran waendelee kuisoma, hata kwa kisingizio cha kuikosoa.

Na mwisho wa siku, wale wanaoisoma kwa dhihaka mara nyingi huishia kuokolewa na Quran hiyo hiyo wanayoidharau. Ndivyo ilivyomtokea Omar Kattab (ambaye baadaye alikuwa Caliph) alimpinga sana Muhammad na Waislam na kupanga kumuua Muhammad, lakini baadaye akakutana dada na shemeji yake wanasoma QUran, akawapiga sana, kisha akaiona scroll yenye aya kwenye Surat Taha — akabadilika ghafla, akasilimu akawa Khalifa mkubwa aliyesambaza Uislam na kuulinda kwa utajiri na mali zake tu anayetikisa watu wengi leo hii kwa Quran yenye nguvu. Hata humu humu, wanaoichambua Quran kwa dhihaka, watajikuta baadaye wamefunguliwa macho yao kiroho bila kutegemea.

Nisisitize tena: kama kweli huiamini Quran — ipuuze kabisa. Lakini kama kila siku umo ndani ya QUran, basi ujue tayari QUran imeanza kufanya kazi njema ndani yako. Muda si mrefu tutawasikia wengine kama ilivyokuwa kwa al Farsi, Mfalme Najash wa Ethiopia, Mchungaji Tami Al Dari, Minister Yusuf Estes (US), Cat Stevens (US), Malcolm X (el Shabazz), na wengineo wengi. Takbir!
 
Bunch of Contradictions and Logical fallacies

Kwa kuanza tu kusema "Kama huamini injili ipuuze kabisa" Vs "Injili ina nguvu ya kuwabadilisha hata wanaoipinga"
Tunashindwa tukuelewe vipi

Unashauri wapingaji wa injili waache kuisoma lakini at the same time pia unadai injili ina nguvu ya kuwabadilisha watu kupitia usomaji huo.

Sasa nachojiuliza mimi, ikiwa kweli Injili ina uwezo wa kubadilisha watu kupitia usomaji, kwanini tena uhimize watu waache kuisoma?

Na kwanini ulalamike kuona watu wakiikosoa baada ya kuisoma ilihali umedai ina uwezo wa kubadilisha watu?

Mfano wako wa Sauli “Sauli aliwapinga sana Wakristo… lakini baadaye akabadilishwa.”
Unatumia tukio la kipekee la kihistoria (ambalo huwezi kulithibitisha) kama ushahidi wa mantiki ya jumla.

Hii haiwezi kuwa sawa: Tukio la Sauli na wenzie ni la kiimani, si ushahidi wa mantiki kwamba kila anayesoma Injili bila kuamini ataishia kuokoka.
 
Sasa utajuaje vina upuuzi bila kuvisoma?


Kama umegundua vina upuuzi, vipuuze. Si havina maana kwako?

Si umeona wakristo wengi walivyopuuza quran? Baadhi ya wakristo, wamewahi kusikia tu mstari mmoja wa quran au maisha ya aina fulani ya mtume, baada ya pale, hawana muda na quran wala mtume wa waislam. Na wao huona wanapoteza muda wao kuongelea chochote kuhusiana na quran.

Ila kama ulikuwa muislam, na kuna sauti inakuita uwe mkristo, hapo upo sahihi kabisa kuisoma biblia, kupata ufafanuzi wa biblia kwenye maeneo ambayo yanakutatiza, n.k. Lakini kama huna mpango wa kuwa mkristu, wala hutaki kusikia ujumbe wa Kristo Masiha, Yesu aliye njia pekee ya kufika kwa Baba, basi huna haja ya kuhangaika na Bibilia, wakati wewe siyo wake, na hupo kwenye ufalme wake. Yesu anasema kuwa walio wake anawajua, nao huisikia sauti yake.
 
Back
Top Bottom