Bunch of Contradictions and Logical fallacies
Kwa kuanza tu kusema "Kama huamini injili ipuuze kabisa" Vs "Injili ina nguvu ya kuwabadilisha hata wanaoipinga"
Tunashindwa tukuelewe vipi
Unashauri wapingaji wa injili waache kuisoma lakini at the same time pia unadai injili ina nguvu ya kuwabadilisha watu kupitia usomaji huo.
Sasa nachojiuliza mimi, ikiwa kweli Injili ina uwezo wa kubadilisha watu kupitia usomaji, kwanini tena uhimize watu waache kuisoma?
Na kwanini ulalamike kuona watu wakiikosoa baada ya kuisoma ilihali umedai ina uwezo wa kubadilisha watu?
Mfano wako wa Sauli “Sauli aliwapinga sana Wakristo… lakini baadaye akabadilishwa.”
Unatumia tukio la kipekee la kihistoria (ambalo huwezi kulithibitisha) kama ushahidi wa mantiki ya jumla.
Hii haiwezi kuwa sawa: Tukio la Sauli na wenzie ni la kiimani, si ushahidi wa mantiki kwamba kila anayesoma Injili bila kuamini ataishia kuokoka.
Maswali ya imani hayajibiwi kwa logic pekee yake. Biblia inasema, hekima ya Mungu, siyo ya mwanadamu.
Ndiyo maana unaweza kushangaa, wewe ukawa mkristo mzuri tangu utoto wako mpaka uzee wako, ukabakia kuwa mkristo wa kawaida. Halafu aliyekuwa anaupinga ukristo tangu utoto wake mpaka ujana wake, mwishoni anakuwa mkristo, tena mwenye mamlaka na kufanya mengi katika ulimwengu wa Roho.
Namkylumbuka yule shekhe wa Zanzibar, aliyekuwa shekhe kwa miaka 21. Akaugua kwa miaka 7, kisha anasema alisikia sauti ikimwambia asome biblia sura ... (siikumbuki ile aya), mara akapona ugonjwa wake na kuamza kuitafuta biblia. Alipofungua biblia hilo fungu kwenye kitabu cha ufunuo, akakutana na maneno yale aliyosikia kwenye sauti aloyoisikia bila ya kumwona mwenye sauti. Baada ya pale nguvu zake zote zikawa kwenye biblia, akawa anahuburi kwenye makanisa ya KKKT, huku wengi wakibadilika kutokana na mafundisho yao, tena akiwavuta maelfu ya watu zaidi ya wachungaji na maaskofu.
Kwenye masuala ya kiimani, si ajabu, siku nyingine ukamkuta Covax akiwa mkristo mwaminifu, mfuasi mkamilifu ya Yesu, kuliko sisi wakristo wa tangu kale. Kwa Mungu kila jambo linawezekana, na kila jambo hufanyika kwa lengo maalum.