Wanaotafuta Utajiri wa Punje za Mahindi na Jogoo, Imekaaje Hii?

Wanaotafuta Utajiri wa Punje za Mahindi na Jogoo, Imekaaje Hii?

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Nikiwa kwenye basi katika harakati za kuitafuta shs, tumesimama kuchimba dawa eneo linaonekana kama kijiji baada ya makambako kuelekea mafinga, ni eneo flani inaonekana kuna vyoo vya mtu binafsi ila abilia hatulipi na sijui nani anayehudumia hivyo vyoo!.

Nikiwa ndani ya chumba natoa oil chafu ya mwilini kwa nyuma nasikia majibizano makali tu kutoka kwa watu wawili, kutokana na majibizano yao nikagundua mmoja ni mganga na mwingine ni mteja.

Jamaa aliyekuwa anafoka alikuwa anadai inakuwaje jogoo akala punje 3 za mahindi kisha kuondoka wakati hakuwa na chakula kwa muda?.

Sikusikia jibu kutoka upande wa pili ila baadaye jamaa inaonekana ni mteja akaomgeza "jogoo wangu niliyekuja naye mpaka sasa bado anakula punje za mahindi ila wako amekula 3 na kuondoka, kwa nini?"

Ila kwa sababu tulipewa dakika 5 za kuchimba dawa sikuweza kufuatilia au kujua kilichoendelea katika kujiuliza nimeileta ili wale wadau wa Jogoo na punje za mahindi mje mtujuze ni nini hiki?.

Niliwahi sikia utajiri wa punje za mahindi kuwa jogoo anapokula punje kadhaa basi huo ndiyo uhai wa utajiri wako kulingana na alivyokula but imekuwaje kukawa na jogoo wawili tofauti, yaani wa mteja na wa witchcraft. na huyo wa mganga akala tatu na kusepa ila wa mteja akaendelea kula?
 
Utajiri wa laana huo kwa wakunga wa pande hizo. Mwisho wao ni mbaya sana nabwanaanguka ghafla katikati ya lundo la utajiri.

Kuna tajiri mmoja wa pande hizo hapa daslam,alikalia meza ndogo ya kioo ikavunjika na kumjeruhi kidoleni mkono ✋. Kapelekwa hospitali siku ya pili kafariki. Vitu vya ajabu kabisa,jamaa alikuwa na malori hakuna mfano
 
Duhh.... Hatari sanaaa.
 
Hahah kamshindisha na njaa jogoo kampeleka law mganga kaishia Kula punje tatu tu, it means miaka mi3 ya uboss
Hapana, hapo kuna jogoo wawili (kutokana na mazungumzo ya wale watu) huyu wa mganga alikuwa punje 3 but yule wa mteja alikuwa akiendelea kula.

Hapo ndipo sikupaelewa why jogoo wawili?.
 
Utajiri wa laana huo kwa wakunga wa pande hizo. Mwisho wao ni mbaya sana nabwanaanguka ghafla katikati ya lundo la utajiri.

Kuna tajiri mmoja wa pande hizo hapa daslam,alikalia meza ndogo ya kioo ikavunjika na kumjeruhi kidoleni mkono [emoji113]. Kapelekwa hospitali siku ya pili kafariki. Vitu vya ajabu kabisa,jamaa alikuwa na malori hakuna mfano
Alafu ndo amepoteaga mazima Yule broh hakuna hata anaposikika Tena utadhani hakuwaga milionea daah. Amekufa gafla na kumbukumbu zake zimepotea kwa haraka mnooo.
 
Utajiri wa laana huo kwa wakunga wa pande hizo. Mwisho wao ni mbaya sana nabwanaanguka ghafla katikati ya lundo la utajiri.

Kuna tajiri mmoja wa pande hizo hapa daslam,alikalia meza ndogo ya kioo ikavunjika na kumjeruhi kidoleni mkono [emoji113]. Kapelekwa hospitali siku ya pili kafariki. Vitu vya ajabu kabisa,jamaa alikuwa na malori hakuna mfano
Malori yasiyokuwa na mfano.. [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom