Wanaotafuta Utajiri wa Punje za Mahindi na Jogoo, Imekaaje Hii?

Wanaotafuta Utajiri wa Punje za Mahindi na Jogoo, Imekaaje Hii?

Haya mambo yanafanyika sana Congo na West Africa hata Malawi na Msumbiji. Hapa Tanzania watu wanay-afanye kwa siri.

West Africa unaingia kwenye secret society na unaweka nadhiri. Chochote unachotaka unafanyiwa. Si biashara tu hata vyeo kazini.

Inabidi utoe kafara kila mwaka na kila unapofanikiwa jambo lako. Unaweza kukumkuta bwana mdogo ametoka chuoni juzi baada ya mwaka ni boss mkubwa kabisa.
 
Nikiwa kwenye basi katika harakati za kuitafuta shs, tumesimama kuchimba dawa eneo linaonekana kama kijiji baada ya makambako kuelekea mafinga, ni eneo flani inaonekana kuna vyoo vya mtu binafsi ila abilia hatulipi na sijui nani anayehudumia hivyo vyoo!.

Nikiwa ndani ya chumba natoa oil chafu ya mwilini kwa nyuma nasikia majibizano makali tu kutoka kwa watu wawili, kutokana na majibizano yao nikagundua mmoja ni mganga na mwingine ni mteja.

Jamaa aliyekuwa anafoka alikuwa anadai inakuwaje jogoo akala punje 3 za mahindi kisha kuondoka wakati hakuwa na chakula kwa muda?, Sikusikia jibu kutoka upande wa pili ila baadaye jamaa inaonekana ni mteja akaomgeza "jogoo wangu niliyekuja naye mpaka sasa bado anakula punje za mahindi ila wako amekula 3 na kuondoka, kwa nini?"

Ila kwa sababu tulipewa dakika 5 za kuchimba dawa sikuweza kufuatilia au kujua kilichoendelea katika kujiuliza nimeileta ili wale wadau wa Jogoo na punje za mahindi mje mtujuze ni nini hiki?.

Niliwahi sikia utajiri wa punje za mahindi kuwa jogoo anapokula punje kadhaa basi huo ndiyo uhai wa utajiri wako kulingana na alivyokula but imekuwaje kukawa na jogoo wawili tofauti, yaani wa mteja na wa witchcraft. na huyo wa mganga akala tatu na kusepa ila wa mteja akaendelea kula?
Haha hahah tukutane Gamboshi. Maisha hayana short cut, ukilazimisha unakufa mapema sana
 
Haya mambo yanafanyika sana Congo na West Africa hata Malawi na Msumbiji. Hapa Tanzania watu wanay-afanye kwa siri.

West Africa unaingia kwenye secret society na unaweka nadhiri. Chochote unachotaka unafanyiwa. Si biashara tu hata vyeo kazini.

Inabidi utoe kafara kila mwaka na kila unapofanikiwa jambo lako. Unaweza kukumkuta bwana mdogo ametoka chuoni juzi baada ya mwaka ni boss mkubwa kabisa.
Ndio maana binafsi nasema tufae kuwa real. Inakufaa nini kuwa mchawi while busy kunena kwa lugha church? Bora huo muda ungekua busy kukusanya fisi na kusafisha vitendea kazi vyako.
 
Haya mambo yanafanyika sana Congo na West Africa hata Malawi na Msumbiji. Hapa Tanzania watu wanay-afanye kwa siri.

West Africa unaingia kwenye secret society na unaweka nadhiri. Chochote unachotaka unafanyiwa. Si biashara tu hata vyeo kazini.

Inabidi utoe kafara kila mwaka na kila unapofanikiwa jambo lako. Unaweza kukumkuta bwana mdogo ametoka chuoni juzi baada ya mwaka ni boss mkubwa kabisa.
Nigeria na ghana au sio...wewe umeangalia movie za wanaijeria ndio unaleta hapa
 
Maana yake yule jogoo wa mganga ndio Dawa Ni mwakilishi wa mganga ndo utajiri utakaoishi nao huku duniani na yule jogoo wako anakuwakilisha wewe kwenye upande wako wa pili baada ya kupata hzo pesa katika kipindi utakachokuwa unakirudisha kulipa hzo pesa.

Hvyo utapata utajiri duniani kwa muda mfupi Ila utaenda kutumikia kurudisha hzo pesa kwa muda mrefu Sana huko upande wa pili (ndio tafsiri ya jogoo wako kuendelea kula hzo punje bila kuacha).
 
Utajiri wa laana huo kwa wakunga wa pande hizo. Mwisho wao ni mbaya sana nabwanaanguka ghafla katikati ya lundo la utajiri.

Kuna tajiri mmoja wa pande hizo hapa daslam,alikalia meza ndogo ya kioo ikavunjika na kumjeruhi kidoleni mkono ✋. Kapelekwa hospitali siku ya pili kafariki. Vitu vya ajabu kabisa,jamaa alikuwa na malori hakuna mfano
baada ya hapo biashara zake ziliendaje?
 
Nahisi labda umekosea kuwasilisha,kwa nilivyousikia utajiri huo ungesema wa jamaa kala punje 3 kaacha halafu wa mganga bado anaendelea kula hapo, sawa jamaa lazima apanic.
Usihisi..we ndo umekosea ...jamaa yuko sahihi..ingawa story yake eti wakawa wanabishana nyuma yake sio kweli...hakuna mganga na mteja eti wakaongeleaa Mambo yao Tena issue ngumu Kama ya utajiri mbele za watu..Kwanza mara nyingi eneo la kuku kula punje Ni mbali na kilinge cha mganga
 
Inatakiwa Jogoo ale punje 40 hahaaaa hapo lazima ukubali agano....maana utakula bata la kufa mtu ndani ya miaka 40 then after 40 yrs kwishnery pateli.
Haijawahi kutokea kula ata punje 10...wenye bahati 8-5...mganga Ni dalali ndio maana hukuti ampe ndugu yake utajiri wa hivo yeye anategemea ufanikiwe umpe fadhila...na Yule jogoo Ni jini ndio unaeingia nae mkataba...na ndo Mana akishakula punje anapotea ..akishapotea jua anakua mwilini mwa muhusika Sasa kumtimizia mahitaji yake ya utajiri..na ikifika siku huyohuyo ndo atamuondoa...that's why Kuna wahuni miaka ya nyuma walikua wanaenda kutegua kigoma hiyo ya deadline ya kufa...
 
Hata Kama umeshikwa na dhiki kiasi gani usijekubali kuchukua huo ujinga..Ni Bora tu ukachukua catalyst za ku accelerate Mambo yako yaende upate rizki ya kuishi...
hizo catalyst ndiyo anazo jongoo. akishameza hizo punje za mahindi ndipo anarelease hizo catalyst za utajiri kwa kipindi maalum. Baada ya hapo unakufa, technically anakuchukua ukamtumikie kutajirisha wahanga wengine.

Hakuna utajiri mzuri kama unaotokana na kufanya kazi kwa bidii. Huwi na pressure, huzuni wala wasiwasi
 
Back
Top Bottom