Kivumishi Kielezi
JF-Expert Member
- Nov 1, 2019
- 1,028
- 2,451
Tangu zoezi la haya machanjo lianze, wajuvi tuliona kuna usanii mwingi na maigizo ndani yake.
Ukiachana na kituko cha wale manesi bandia walioshika sindano kama penseli tena bila gloves na tahadhari zingine za kiafya, leo hii kumezuka kitimbi kingine.
Mmojawapo wa 'wahubiri wa chanjo', Daktari Sospeter Bulugu, leo hii ameonekana akipepesuka na kutaka kuanguka akiwa kwenye kongamano la kuhubiri chanjo kwenye moja ya video iliyorekodiwa.
Baadae ikasikika sauti ya Waziri Dorothy Gwajima akitaka tukio lile lisirushwe na vyombo vya habari kwa sababu eti 'litaipaka tope' chanjo.
Baada ya mabishano ya hapa na pale, wengine wakisema kwamba Daktari Sospeter alitaka kuanguka kutokana na madhara ya chanjo, Wizara ya Afya imekuja na kanusho kwamba Daktari Sospeter hajachanjwa na hajawahi kuchanjwa.
Lakini cha ajabu Daktari huyu alikuwa kwenye kongamano la kuhubiri watu wakadungwe chanjo.
Na inawezekanaje watu wanaowashawishi watu wakadungwe michanjo ya Covid wao wenyewe hawataki kudungwa?