Wanaoukubali mkataba wa makubaliano na wanaoupinga nani wana haki?

Wanaoukubali mkataba wa makubaliano na wanaoupinga nani wana haki?

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
7,672
Reaction score
9,039
Ni aibu kuwa tangu tupate uhuru zaidi ya miaka 60, hatuna uwezo hata wa kuendesha bandari zetu kwa ufanisi. Najua inauma.

Hivi karibuni kumekuwa na mgawanyiko mkali baina ya watawala walioamua kubinafsisha/kuuza bandari zetu kama ni kweli na wale wanaopinga wakiwatuhumu ufisadi na kutojali mali za taifa.

Je, kama tutakuwa wakweli, si kweli kuwa nasi tumeshindwa kutokana na kujiibia na kujinufaisha wenyewe huku umma ukiendelea kutopea kwenye umaskini huku wezi wachache wakitajirika?

Nasi kama wananchi tumeshiriki dhambi hii kwa kuwaabudia vibaka na majizi yaliyotumia mali zetu za asili kama shamba la bibi huku tukiwapiga mizinga na kuwanyenyekea. Je nasi hatujashiriki dhambi hii? Je wezi wenye madaraka, na wananchi wajinga wote dhambi yao siyo moja?

Je, kati yetu na hawa tunaowalaumu kutaka kuuza na kuchezea mali zetu nani mwenye haki wakati wote ni washiriki? Leo majizi kama Rostammmm nayo yanaongea utadhani hatujui ujembuzi wao.
 
Kwanza hakuna mahala bandari inauzwa.

Sisi tunaunga mkono ukodishwaji tuna Haki Kwa sababu tunaangalia mapesa ambayo ni muhimu kwenye maendeleo na Ufanisi Ili biashara zitoke.

Hao wengine ni wazee, wengine wanategemea vya madhabahuni, wengine ni wasomi ambao akili zao zimeishia kwenye makaratasi so hawana Cha kuonesha Hadi wanazeeka au Wana usomi wao.
 
Back
Top Bottom