Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Kila kitu kina mpangilio katika maisha.. Huwezi kufanya kinyume na mpangilio na ukijaribu kufanya hivyo matokeo yake ni zogo na kupaganyika.
Kwenye hili la machinga lilikosa mpangilio..Na likafugwa na wanasiasa kwa maslahi binafsi ya kisiasa.. Sasa kama tumeamua kurudi kwenye mpangilio lawama zinatoka wapi?
Hata majumbani mwetu.. Tuna mipangilio ya kila kitu kitanda kina sehemu yake, choo, vyombo viatu nguo vyakula nknk.. Miili yetu nayo ina mipangilio macho yakae wapi, mikono, miguu nknk havijarundikwa tu sehemu moja.. Mifano ni mingi sana.
Sasa tunapata wapi uthubutu wa kutetea watu wanafanya biashara sehemu zisizo rasmi?
Kwenye njia za waenda kwa miguu
Kwenye mitaro ya maji
Kwenye vituo vya kupumzikia
Kwenye maeneo ya wazi
Kwenye vituo vya magari njiani
Mbele ya maduka ya wengine nknk
Tuna kitu kinaitwa mipango miji... Hii ndio huamua miji iweje
Wapi sehemu za makazi
Wapi sehemu za biashara
Wapi sehemu za michezo
Wapi sehemu za kupumkizia
Wapi sehemu za starehe
Wapi sehemu za ibada
Wapi sehemu za huduma za jamii nknk
Sehemu za zilizotengwa kwa shughuli fulani zibaki hivyo kwa shughuli tazamiwa..ukianza kuchanganya unaharibu na kuleta zogo
Uchafuzi wa mazingira ni pamoja na kuweka vitu mahali pasipopaswa viwepo... Usafi wa miji ni pamoja na kuwa na mpangilio kwenye kila jambo...Je watetezi wa machinga wanajua yote haya?
Tazama picha hizi za jiji bila vibanda vya machinga! Je mji hauvutii!?