1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,201
- 9,529
Ulimsikia Mbunge na kada wa CCM toka kanda ya Ziwa ,mh.Musukuma kipambana ili Wamatumbi wanaoitwa Wamachinga wasipatiwe maeneo rasmi ya biashara ? Anapambana na kuwatetea ili wajenge vibanda vya biashara kwenye mitaro ya barabarani ?Palikua na agenda gani ya kuwaacha Vijana wenye nguvu wa Kimatumbi wakimbilie DSM na kuacha ardhi yao yenye utajiri mkubwa namna hiyo? Ardhi ya Lindi na Mtwara inakimbiliwa na wafugaji toka kanda ya ziwa na Manyara na Arusha.[emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827]
Jiulize Mbenge kutoka kwa wafugaji wasio na ardhi ,Mbunge mfanyabiashara ya madini ,Mbunge ambaye wanapiga kura wake kuna wakati walikua wanahamasishana kufyatua watoto na kuongeza wake wengi!!
Hivi ni kweli Huyo Mbunge anauchungu na Wamatumbi toka mchinga palipojaa Jipsam na Korosho?
Tujiulize Wakati wamachinga walipoanza Kurudi Vijijini kulima korosho ,mbona hakuwatetea wasiporwe pesa zao za Korosho ? Serikali ilipokwapua pesa za Korosho na Musukuma na Polepole walikaa kimya na kusababisha zao lao LA Korosho liporomoke na kukosa soko mpaka Leo na kusabisha wamachinga warudi Kwenye hifadhi za barabara kuuza midoli toka China na pipi toka China huku wakizidi kukuza uchumi wa China kwa kukwepa kodi rasmi na kusababisha Wafanyabiashara toka Kongo na Sudani kusini kukimbilia Kampala baada ya kuziba kila mahali na kufanya jiji kuwa kama eneo la vibaka na wababaishaji.
Wakati huo huo awamu ya NNE ilipoanzisha miradi mikubwa ya Gesi, viwanda ,vikubwa vya Saruji walilenga kuwavutia vijana wa kimatumbi maarufu kama wamachinga warudi kwao kuendeleza ardhi yao yenye utajiri mkubwa sana Afrika na duniani. Ardhi ambayo inapaswa kuwa kivutio kikubwa cha watalii kwani ndilo eneo lililothibitika mpaka sasa kuwa waliishi Mijusi wakubwa sana Karene nyingi zilizopita. Na moja ya mabaki ya mijusi hao ipo mpaka Leo kule Ujeruman. Badala ya serikali kupambana ili mabaki hayo yarejeshwe Tanzania wao wanapambana na watu wanaovaa tisheti za Katiba mpya na kuwatelekeza kwa kudhibiti zao la Korosho lisije likawanufaisha Wakulima na kuvuruga Uwekezaji kwenye Gesi na Viwanda vya Sariji. Matokeo yake Wamatumbi wamekimbilia kuishi na kufanya biashara mitaroni DSM . Wakati huo wafugaji wanaotoka kwenye jimbo la Musukuma na wafanyabishara wa madini wanakimbilia kwa kasi kubwa sana Lindi na Mtwara ambapo kuna ardhi nzuri na kubwa.
Tchaaaah!
Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app