Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio tuu uelewa wao ni mdogo lakini pia ni wajinga au wanataka kuwatumia kisiasa.Kila kitu kina mpangilio katika maisha.. Huwezi kufanya kinyume na mpangilio na ukijaribu kufanya hivyo matokeo yake ni zogo na kupaganyika.
Kwenye hili la machinga lilikosa mpangilio..Na likafugwa na wanasiasa kwa maslahi binafsi ya kisiasa.. Sasa kama tumeamua kurudi kwenye mpangilio lawama zinatoka wapi?
Hata majumbani mwetu.. Tuna mipangilio ya kila kitu kitanda kina sehemu yake, choo, vyombo viatu nguo vyakula nknk.. Miili yetu nayo ina mipangilio macho yakae wapi, mikono, miguu nknk havijarundikwa tu sehemu moja.. Mifano ni mingi sana.
Sasa tunapata wapi uthubutu wa kutetea watu wanafanya biashara sehemu zisizo rasmi?
Kwenye njia za waenda kwa miguu
Kwenye mitaro ya maji
Kwenye vituo vya kupumzikia
Kwenye maeneo ya wazi
Kwenye vituo vya magari njiani
Mbele ya maduka ya wengine nknk
Tuna kitu kinaitwa mipango miji... Hii ndio huamua miji iweje
Wapi sehemu za makazi
Wapi sehemu za biashara
Wapi sehemu za michezo
Wapi sehemu za kupumkizia
Wapi sehemu za starehe
Wapi sehemu za ibada
Wapi sehemu za huduma za jamii nknk
Sehemu za zilizotengwa kwa shughuli fulani zibaki hivyo kwa shughuli tazamiwa..ukianza kuchanganya unaharibu na kuleta zogo
Uchafuzi wa mazingira ni pamoja na kuweka vitu mahali pasipopaswa viwepo... Usafi wa miji ni pamoja na kuwa na mpangilio kwenye kila jambo...Je watetezi wa machinga wanajua yote haya?
Tazama picha hizi za jiji bila vibanda vya machinga! Je mji hauvutii!?View attachment 1980673View attachment 1980674
Kwa kero walikuwa kero na wameendelea kuwa kero kuhusu mwendelezo wa siasa za kipuuzi kama nia ni njema na kuna permanent solution.. Na hakuna cheap popularity gainings basi ni jambo jema!kwamba walikuwa kero kiasi hicho kinachpigiwa kelele au ndio siasa za kipuuzi katika mwendelezo huo!!!
Umeandika kitaalam sanaWell Said;
Itapendeza *TARURA/TANROAD wanapojenga Barabara, wasiweke service road , wala peavings , WAWEKE MABANDA PEMBEZONI mwa Barabara zote nchini yakae tu hata kama hakuna wahitaji maana wanyonge wanatakiwa wafanye Biashara Humo!
Hawa watu wana familia, WAACHWE WAFANYE LOLOTE so long as wanapata kipato cha kulisha familia
Pia; Serikali iwache wanyonge wote waliochukua MAENEO YA HIFADHI ZA TAIFA, ni ajabu eti Mtu unaishi Morogoro huna ardhi wakati kuna mbuga ya Mikumi imekaa tu.
Kila mtu aachwe atafute maisha yake, hawa matajiri wao wanaishi, Njiro, Shanty-town, Masaki, Kisota na Uzunguni, Gangilonga hawajui adha ya sisi wanyonge!
Kuhusu kupanga bidhaa hilo ni Utashi binafsi, ndio maana kuna nyumba ya Tajiri isiyo na mpangilio mzuri vilevile. Kwa hiyo hatuna mipangilio mizuri au mibaya kwa sababu ya Utajiri au UmaskiniNimetolea mfano wa nyumba tunazoishi je tunaweza kushindwa kupanga vitu vyetu ndani ya nyumba kwa kigezo cha umaskini? Je tuko tayari machinga wapange bidhaa zao mpaka milangoni kwa kigezo kuwa wanatafuta? Wazibe barabara? Wajae maeneo ya wazi?
Wewe ndio mnafiki nunber mojasio kosa la machinga,kosa ni letu kutotambu mipango.
hapa ilikuwa simple tu,wapewe mipaka na sandard za vibanda,ili maisha yaendelee tu.
leo hii tunajifanya kuchukia mabati na bishara kila sehem wakati dsm yote ni uchafu uchafu tu kutokea angani!!!unafiki hautatufikisha popote.
Fata utaratibu..ona sasa unatoa povu tu.sio kosa la machinga,kosa ni letu kutotambu mipango.
hapa ilikuwa simple tu,wapewe mipaka na sandard za vibanda,ili maisha yaendelee tu.
leo hii tunajifanya kuchukia mabati na bishara kila sehem wakati dsm yote ni uchafu uchafu tu kutokea angani!!!unafiki hautatufikisha popote.
Utawala huu Wasipoliewewa hili, basi chaos is innevitable.Lakini Ndugu Mshana Jr, one of the main elements in development work for the poor groups is to give them self-confidence and freedom to decide themselves.
Kwa hofu wanayopewa Hawa watu na Mamlaka, kovu la Manyanyaso haya ya Moyo litakuwepo kwa Muda mrefu kweli kweli
They are not Rich ni Maskini Hawa watu
Kifupi wengi wao Umachinga ni Alternative Bora zaidi baada ya mambo Mengi kuwadundia nchini Mwao
Sasa kwa sababu ipi wasingesubiri Tanzania iliyopiga hatua kwenye kuzalisha AJIRA, PRICE stability pamoja na Country Economic GROWTH hapo kwanza Machinga wenyewe wangepungua katikati ya Miji.
Huu sio wakati sahihi Ndio maana tunasema SI SAWA
Fata utaratibu..ona sasa unatoa povu tu.
#MaendeleoHayanaChama
Wewe ndio mnafiki nunber moja
Pathetic
Jeshi la Polisi tupo imara...jaribuni muoneTujiandae kwa Wizi wa kutumia Magari na Ulinzi kudumaa kwenye Maji yaliyo wazi.
Kwa kero walikuwa kero na wameendelea kuwa kero kuhusu mwendelezo wa siasa za kipuuzi kama nia ni njema na kuna permanent solution.. Na hakuna cheap popularity gainings basi ni jambo jema!
Mji unapumua sasa.. Ulikuwa umelemewa
'Waachwe wafanye watakavyo ili wapate riziki', hilo si sawa. Kama ni sawa basi hatuna sababu ya kuwepo mahakama, hakuna sababu kuwepo na sheria. Unataka tuishi kama wanyama, survival of the fittest. Sheria zetu nyingi ni mbovu na ndio kinasikika kilio cha kutaka katiba. Wanasiasa wanazitumia vibaya hata sheria chache nzuri zilizopo kwa manufaa yao, kama kuvuruga sheria ya mipango miji. Tufike mahala tukatae kuishi ujima.Well Said;
Itapendeza *TARURA/TANROAD wanapojenga Barabara, wasiweke service road , wala peavings , WAWEKE MABANDA PEMBEZONI mwa Barabara zote nchini yakae tu hata kama hakuna wahitaji maana wanyonge wanatakiwa wafanye Biashara Humo!
Hawa watu wana familia, WAACHWE WAFANYE LOLOTE so long as wanapata kipato cha kulisha familia
Pia; Serikali iwache wanyonge wote waliochukua MAENEO YA HIFADHI ZA TAIFA, ni ajabu eti Mtu unaishi Morogoro huna ardhi wakati kuna mbuga ya Mikumi imekaa tu.
Kila mtu aachwe atafute maisha yake, hawa matajiri wao wanaishi, Njiro, Shanty-town, Masaki, Kisota na Uzunguni, Gangilonga hawajui adha ya sisi wanyonge!
Uchafu wa mazingira ulikuwa wa kiwango cha juu mno chupa za mikojo na mifuko yenye vinyesi ilitupwa popote panapoonekana panafaa kutupwaSio umeelemewa tu bro
Mji ulikuwa na harufu ya kinyesi na mikojo ya watu wanaoshinda hapo bila kuwa na sehemu ya kujisaidia zaidi ya mifuko na chupa za maji tupu
Unashangaa harufu kila sehemu na uchafu ndio usiseme halafu wanaolipia usafi ni wengine
Acha wapambane na hali yao
Nakazia Jiji limepumua