Wanaowatetea machinga kuondolewa maeneo yasiyo rasmi kwa biashara wana uelewa mdogo

Wanaowatetea machinga kuondolewa maeneo yasiyo rasmi kwa biashara wana uelewa mdogo

Kila kitu kina mpangilio katika maisha.. Huwezi kufanya kinyume na mpangilio na ukijaribu kufanya hivyo matokeo yake ni zogo na kupaganyika.

Kwenye hili la machinga lilikosa mpangilio..Na likafugwa na wanasiasa kwa maslahi binafsi ya kisiasa.. Sasa kama tumeamua kurudi kwenye mpangilio lawama zinatoka wapi?

Hata majumbani mwetu.. Tuna mipangilio ya kila kitu kitanda kina sehemu yake, choo, vyombo viatu nguo vyakula nknk.. Miili yetu nayo ina mipangilio macho yakae wapi, mikono, miguu nknk havijarundikwa tu sehemu moja.. Mifano ni mingi sana.

Sasa tunapata wapi uthubutu wa kutetea watu wanafanya biashara sehemu zisizo rasmi?
Kwenye njia za waenda kwa miguu
Kwenye mitaro ya maji
Kwenye vituo vya kupumzikia
Kwenye maeneo ya wazi
Kwenye vituo vya magari njiani
Mbele ya maduka ya wengine nknk

Tuna kitu kinaitwa mipango miji... Hii ndio huamua miji iweje
Wapi sehemu za makazi
Wapi sehemu za biashara
Wapi sehemu za michezo
Wapi sehemu za kupumkizia
Wapi sehemu za starehe
Wapi sehemu za ibada
Wapi sehemu za huduma za jamii nknk
Sehemu za zilizotengwa kwa shughuli fulani zibaki hivyo kwa shughuli tazamiwa..ukianza kuchanganya unaharibu na kuleta zogo

Uchafuzi wa mazingira ni pamoja na kuweka vitu mahali pasipopaswa viwepo... Usafi wa miji ni pamoja na kuwa na mpangilio kwenye kila jambo...Je watetezi wa machinga wanajua yote haya?
Tazama picha hizi za jiji bila vibanda vya machinga! Je mji hauvutii!?View attachment 1980673View attachment 1980674
IFm unaendesha sasa
 
Siamini kama haya unayamaanisha, bila shaka unatania.
Basi Itapendeza TARURA/TANROAD wanapojenga Barabara, wasiweke service road , wala peavings , WAWEKE MABANDA Pembezoni mwa Barabara zote nchini yakae tu hata kama hakuna wahitaji maana wanyonge wanatakiwa wafanye Biashara Humo!
 
Well Said;
Itapendeza *TARURA/TANROAD wanapojenga Barabara, wasiweke service road , wala peavings , WAWEKE MABANDA PEMBEZONI mwa Barabara zote nchini yakae tu hata kama hakuna wahitaji maana wanyonge wanatakiwa wafanye Biashara Humo!

Hawa watu wana familia, WAACHWE WAFANYE LOLOTE so long as wanapata kipato cha kulisha familia

Pia; Serikali iwache wanyonge wote waliochukua MAENEO YA HIFADHI ZA TAIFA, ni ajabu eti Mtu unaishi Morogoro huna ardhi wakati kuna mbuga ya Mikumi imekaa tu.

Kila mtu aachwe atafute maisha yake, hawa matajiri wao wanaishi, Njiro, Shanty-town, Masaki, Kisota na Uzunguni, Gangilonga hawajui adha ya sisi wanyonge!

Wasiweke service roads? Nini kazi ya service roads?
Yes machinga wanatafuta riziki na ni sehemu kubwa ya jamii yetu. Hakuna namna nzuri ya kufanya mambo ya biashara mpaka kila eneo la wazi, barabarani, na kila sehemu kuwe na watu wanafanya biashara?
 
Huu ndio ukweli wote. Tatizo kuna wahuni wanataka kutafuta urahisi wa maisha kwa njia haramu. Huwezi kujenga nyumba barabarani kwa kigezo kwamba wewe ni mnyonge. Kwa namna hii kuna siku hawa wangejimilikisha maeneo ya watu ama ya umma na hakuna mtu angewasemesha. Turudi kwenye utaratibu wa mwanzo wa machinga anayetembea, akikua na kuwa na mtaji mkubwa usiofaha kutembea basi aingie kwneye level ya mfanyabiasha mdogo na akodi frem afanye biashara katika mfumo rasmi.
Wamachinga hawajawahi kuwa tatizo katika nchi hii.

Machinga anabeba na kutembeza biashara zake hapa na pale.

Huyu anayejenga mabanda barabarani kuziba barabara, mabanda juu ya mitaro ya maji ni mtu gani huyu?

Huyu anayepanga duka zima barabarani ni nani?

Huyu sio machinga aondoke mara 1, machinga halisi wabakie waendelee kutembeza bidhaa zao
 
Umesema kweli tupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu kupanga bidhaa hilo ni Utashi binafsi, ndio maana kuna nyumba ya Tajiri isiyo na mpangilio mzuri vilevile. Kwa hiyo hatuna mipangilio mizuri au mibaya kwa sababu ya Utajiri au Umaskini

Kuna Machinga wanajua kutumia Space zao vizuri na njia wanaacha utawapenda yaani;

Machinga huwa na mpangilio usiovutia pale palipo na Hot Bussiness yaani Wateja wa kutosha mbele, nyuma na Pembeni huku ndio kungewekewa marekebisho kiasi

Hivi sio kweli kuwa lengo la Hawa watu kuhamishwa ni kwa sababu inabidi wakae mahali Biashara zao ziwe updated kwenye mifumo ya Kodi?

Au ndo kusafisha Jiji ili livutie? Tuweni na Utu, watu wana familia, watoto wapo shule wanasoma na mahitaji Mengine Mengi

Tujiandae kwa Wizi wa kutumia Magari na Ulinzi kudumaa kwenye Majiji na miji iliyo wazi.

Ni kwa sababu watu wamekuwa na umakini mkubwa sana wa kuendesha wawapo Town na watu wakiwa wengi Mahali, ndio Ulinzi wenyewe wa Nchi yetu.
Wende Machinga Complex,maeneo mengi wametengewa,hawataki kwenda.Hapo wanapopaona kuna biashara,hao wenye Frem,pia ulichukuwa mda mpaka kuzoeleka na kupata wateja.Na wamachinga waende maeneo waliotengewa,wateja watawafuata huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni na sekeseke na kuondolewa vibanda vyenu machinga sehemu zilizopo mijini.

Swali nalo jiuliza kuhusu vitambulisho vya wamchinga.

Vilikuwa na muongozo au malengo gani ambayo mwisho wa siku kuwa vurugu na hatima isiyojulikana kwa wimbi la wanaojitafutia kipato
View attachment 1980784
huu ni utapeli wa Bwn Jiwe hicho kitambulisho hakina jina mahususi la mtoaji,anuani na mawasiliano mengine, pia hicho kitambulisho hakina jina/taarifa binafsi za huyo mjasiriamali,anuani,aina ya biashara etc. Hapa ndipo tatizo lilipoanzia kwenye suala la wamachinga na wajasiriamali
 
UCHAFU ni kitu au hali yoyote iliyopo/kilichopo mahali pasipo stahili mfano vyombo vya chakula kuhifadhi chooni au chupi kuvaa kichwani.
Kifupi Mimi binafsi nadhani ni muda muhafaka kwa serikali kufanya kitu sahihi atukatai umuhimu wa wamachinga ukizingatia wanaendesha maisha kwa shughuli hizo lakini isiwe kigezo cha UMACHINGA kufanyika kiholela na kila mahali lazima vigezo na masharti yazingatiwe tunahitaji wamachinga lakini usafi na mpangilio wa miji ni muhimu katika kuboresha afya na mazingira ya jamiii.
 
Kila kitu kina mpangilio katika maisha.. Huwezi kufanya kinyume na mpangilio na ukijaribu kufanya hivyo matokeo yake ni zogo na kupaganyika.

Kwenye hili la machinga lilikosa mpangilio..Na likafugwa na wanasiasa kwa maslahi binafsi ya kisiasa.. Sasa kama tumeamua kurudi kwenye mpangilio lawama zinatoka wapi?

Hata majumbani mwetu.. Tuna mipangilio ya kila kitu kitanda kina sehemu yake, choo, vyombo viatu nguo vyakula nknk.. Miili yetu nayo ina mipangilio macho yakae wapi, mikono, miguu nknk havijarundikwa tu sehemu moja.. Mifano ni mingi sana.

Sasa tunapata wapi uthubutu wa kutetea watu wanafanya biashara sehemu zisizo rasmi?
Kwenye njia za waenda kwa miguu
Kwenye mitaro ya maji
Kwenye vituo vya kupumzikia
Kwenye maeneo ya wazi
Kwenye vituo vya magari njiani
Mbele ya maduka ya wengine nknk

Tuna kitu kinaitwa mipango miji... Hii ndio huamua miji iweje
Wapi sehemu za makazi
Wapi sehemu za biashara
Wapi sehemu za michezo
Wapi sehemu za kupumkizia
Wapi sehemu za starehe
Wapi sehemu za ibada
Wapi sehemu za huduma za jamii nknk
Sehemu za zilizotengwa kwa shughuli fulani zibaki hivyo kwa shughuli tazamiwa..ukianza kuchanganya unaharibu na kuleta zogo

Uchafuzi wa mazingira ni pamoja na kuweka vitu mahali pasipopaswa viwepo... Usafi wa miji ni pamoja na kuwa na mpangilio kwenye kila jambo...Je watetezi wa machinga wanajua yote haya?
Tazama picha hizi za jiji bila vibanda vya machinga! Je mji hauvutii!?View attachment 1980673View attachment 1980674
Mkuu sisi ni wanyonge..
IMG_20211020_181212.jpg
 
Naunga mkono hoja sio kwamba wana uelewa mdogo bali ni VICHAA.

Machinga watoke waende sehemu rasmi....Sehemu zipo nyingi sana za kufanya biashara zao ukiacha zile walizotengewa!! Fremu zimejaa kibao zipo wazi hazina wapangaji ,mmachinga ana mtaji wa milioni 5 anashindwa kweli kupanga fremu ya elfu 50 kwa mwezi? Siku hizi biashara zinafanywa online wajiongeze!

Hata kama wameomba kukutana na SSH ,naomba Mh SSH komaa hivyo hivyo hawa jamaa wasirudi kwenye mitaro ,kwenye njia za watembea kwa miguu na service roads! Jiji limependeza baada ya kutoka ,walikuwa wanachafua majiji ,waende sehemu mlizowapangia.
 
Wamachinga hawajawahi kuwa tatizo katika nchi hii.

Machinga anabeba na kutembeza biashara zake hapa na pale.

Huyu anayejenga mabanda barabarani kuziba barabara, mabanda juu ya mitaro ya maji ni mtu gani huyu?

Huyu anayepanga duka zima barabarani ni nani?

Huyu sio machinga aondoke mara 1, machinga halisi wabakie waendelee kutembeza bidhaa zao
Kuna watu waliwekeza kwenye ujenzi was vibanda na kuvipanga barabarani kusubiria Kodi.
 
Kiukweli Dar inanuka na huwezi kulijua hili mpaka ukae nje muda mrefu na siku urudi bongo! Siku ukitua pale airport ndio utajua

Nimeliona hili kwa kweli
Natamani miji yote iwe kama Moshi kwa usafi
Na hapo naona wafagiaji wataonekana kuliko mwanzo walikuwa hawawezi hata kufanya usafi kwani itabidi umnyanyue mmachinga na lundo lake la bidhaa ndio usafi ufanyike

Ila sasa jiji litapendeza

Daa nimekumbuka yaliyowakuta watoto huko Brazil wale waliokuwa wanalala mitaani walivyouwawa na serikali eti wanawakimbiza watalii wasije Rio

It was bad sijui kwanini nimekumbuka tukio lile la kutisha
 
Back
Top Bottom