Mkuu, mpangilio naomba radhi nisijibu hapa kwa kuwa ni mpana na nitauweka mada tofauti nipatapo wasaa. Naomba nijitahidi kuelezea maguvu kwa njia nyepesi sana na fupi.
Kuna maguvu mengi tunayoyajua na kubwa kama gravity ni Law kwa kuwa tunaijua uzuri na tunaipima bila shida. Lakini hizi nguvu kubwa zaidi ni hypothesis, bado hamna kitu firm kutokana na ukubwa wa issue yenyewe. Natumia lugha nyepesi na kuita nguvu (inaweza ikawa kitu kingine) maana sipati mamneno mazuri ya kuelezea.
Nikiziweka nguvu hizi katika percentages kutokana na recent studies ni kwamba kubwa kabisa ni Dark energy (cosmological constant) hatuijui vizuri ila ipo. Yani uwiano wa elimu au information tusizonazo/tusiyojua kuhusu hii kitu ni mkubwa sana kulinganisha na ule wa yale machache tunayojua. Kwa nini hatuijui? Ni ngumu kupima, kuiona, kuishika, kuinua yani tunaona matokeo yake tu. Kwa nini ipo? kwa sababu tuna ushahidi wa kutosha jinsi universe inavyo-expand na kuna nguvu inayofanya hii process (expansion). Ni kubwa kiasi gani, ni takribani 68% ya kila kitu kilicho ulimwenguni au katika universe.
Nguvu ya pili au kitu cha pili cha ajabu ambacho kipo inaitwa Dark matter. Hii ipo ila haiwezi kuonekana kwa kuwa kila kitu hata mwanga unapenya kati yake yani hai-interact na kitu chochote. Hii ndio inashikilia universe kwa kuwa isingekuwepo basi ile dark energy ingetutawanya ndani ya sub-second. Ulimwengu ukiangaliwa kwa ujumla unaonekana kuwa na umbo kama nyuzi (web) zilizoshikana hii kitu inadhaniwa kuwa behind this phenomena. Hii ni asilimia takribani 27 (27%) ya kila kitu ulimwenguni.
Alafu ndio tuna matter hii tunaijua na sisi, mawe, maji, gas, sayari, nyota na chochote kinachooneka ndio part yake. Hii ni asilimia takribani 5 tu ya kila kitu katika universe.
Kwa hiyo kila kitu kinachoonekana katika universe ni asilimia tano tu ya kile tusichokiona lakini kipo kwa hakika kutokana na yale tunayoona kama matokeo yake.
Kutokana na jinsi tusivyojua mengi kuhusu hii area ni vigumu kuelezea kwa hakika umuhimu au usalama wake kwa sisi lakini jinsi tulivyo ni matokeo ya kuwapo kwa hizi kitu ama sivyo universe na mambo yake hakika yasingekuwa hivi.