CYBERTEQ
JF-Expert Member
- Feb 11, 2012
- 7,341
- 4,067
wala haukuchukua siku saba....
loh, kumbe niko misinformed, zilikuwa ngapi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wala haukuchukua siku saba....
loh, kumbe niko misinformed, zilikuwa ngapi?
naona watu mnavojidanganya kwenda kuishi huko, hata uchukue hela zote zilizopo duniani uwape NASA na kampuni zinazo-deal na space kama Space X hawana uwezo wa kukupeleka, Mars tu jirani yetu kumfikia miaka zaidi ya 20 sasa ni mahangaiko tu...
Afu kuipata kwenye hiyo telescope itabaki kua nothing more than in papers na sio real proof kua maisha yanaweza kuexist huko, utaambiwa safari inatumia miaka milioni kufika ndo utachoka kama miaka yote hiyo bado utakua mzima... subirini kama yatatokea maajabu warp drive ifanikiwe bac sayari kama hiZo zitafikika sema sio kila mtu, the privileged tu ndo watagusa chini ya asilimia 0.01 ya dunia nzima
Huwa najiuliza Kama ikitokea ikaonekana kuna watu wengine wanaishi kwenye sayari nyingine, sijui vitabu vya dini vitajitetea vp? Sidhani Kama kuna sehemu yoyote kwenye misahafu hiyo inayoeleza kuna binadamu wengine sayari nyingine.
mhh..Aiseh.. sasa hapo Mars tu, ukienda huwezi rudi... imagine another planet from another system...
Kuna theory na proof nyingi kua kitu chochote hakiwezi kwenda speed zaidi ya mwanga.. kwamba kikifika hiyo optimum speed bac kitu kitahitaji infinite energy.. kama ni hivo manake hata tukifanikiwa kukimbia hiyo speed bac hatutotoka kabisa milky way galaxy maana itatumia miaka 1600 kusafiri hadi kufika kwenye edge.. Warp drive sasa ndo inakuja, ukitreat space n time kama kitu kimoja, unaweza bend space kwa vitu kama wormholes ukaweza kusafiri toka upande moja hadi mwingine sio kwa speed ya mwanga lakini kwa kua umebend space yani mfano rahisi 100km ukazibend zikawa 2km manake ukawahi kufika.. sasa inafanya kazi kama hivi.. hii theory ndo wanasayansi walisuggest miaka mingi na wanaifanyia research, kwenye baadhi ya movies kama star trek ukiangalia utaona zile space ships zao wanatoka upande moja kwenda upande mwingine wa galaxy kwa haraka sana kutumia njia hii...Wrap drive ndo nini kiongozi?..
Mkuu, mpangilio naomba radhi nisijibu hapa kwa kuwa ni mpana na nitauweka mada tofauti nipatapo wasaa. Naomba nijitahidi kuelezea maguvu kwa njia nyepesi sana na fupi.
Kuna maguvu mengi tunayoyajua na kubwa kama gravity ni Law kwa kuwa tunaijua uzuri na tunaipima bila shida. Lakini hizi nguvu kubwa zaidi ni hypothesis, bado hamna kitu firm kutokana na ukubwa wa issue yenyewe. Natumia lugha nyepesi na kuita nguvu (inaweza ikawa kitu kingine) maana sipati mamneno mazuri ya kuelezea.
Nikiziweka nguvu hizi katika percentages kutokana na recent studies ni kwamba kubwa kabisa ni Dark energy (cosmological constant) hatuijui vizuri ila ipo. Yani uwiano wa elimu au information tusizonazo/tusiyojua kuhusu hii kitu ni mkubwa sana kulinganisha na ule wa yale machache tunayojua. Kwa nini hatuijui? Ni ngumu kupima, kuiona, kuishika, kuinua yani tunaona matokeo yake tu. Kwa nini ipo? kwa sababu tuna ushahidi wa kutosha jinsi universe inavyo-expand na kuna nguvu inayofanya hii process (expansion). Ni kubwa kiasi gani, ni takribani 68% ya kila kitu kilicho ulimwenguni au katika universe.
Nguvu ya pili au kitu cha pili cha ajabu ambacho kipo inaitwa Dark matter. Hii ipo ila haiwezi kuonekana kwa kuwa kila kitu hata mwanga unapenya kati yake yani hai-interact na kitu chochote. Hii ndio inashikilia universe kwa kuwa isingekuwepo basi ile dark energy ingetutawanya ndani ya sub-second. Ulimwengu ukiangaliwa kwa ujumla unaonekana kuwa na umbo kama nyuzi (web) zilizoshikana hii kitu inadhaniwa kuwa behind this phenomena. Hii ni asilimia takribani 27 (27%) ya kila kitu ulimwenguni.
Alafu ndio tuna matter hii tunaijua na sisi, mawe, maji, gas, sayari, nyota na chochote kinachooneka ndio part yake. Hii ni asilimia takribani 5 tu ya kila kitu katika universe.
Kwa hiyo kila kitu kinachoonekana katika universe ni asilimia tano tu ya kile tusichokiona lakini kipo kwa hakika kutokana na yale tunayoona kama matokeo yake.
Kutokana na jinsi tusivyojua mengi kuhusu hii area ni vigumu kuelezea kwa hakika umuhimu au usalama wake kwa sisi lakini jinsi tulivyo ni matokeo ya kuwapo kwa hizi kitu ama sivyo universe na mambo yake hakika yasingekuwa hivi.
Ina maana huko hata Airtel haishiki?Sasa tutawasiliana na ndugu zetu vipi wakifika huko!