Monstgala
JF-Expert Member
- Aug 25, 2009
- 1,079
- 1,036
Mkuu,sidhani kama umejibu swali langu ....!!
Mkuu Eiyer, ndio sikujibu partly kwa kuwa nili-assume kwa kuonesha tofauti ya umbali na muda basi lazima ungenielewa kwamba kuna tofauti nyingi za kimazingira ingawa inaweza kukaribiana kwa kufanana na dunia lakini si kwa kila kitu. Kuna vigezo vinavyotupa hali hii katika dunia mojawapo ni kuwa katika right place with right conditions (katika solar system). Tofauti kidogo tu ya chochote kuanzia place in terms of distance tuliyopo kutoka pale jua lilipo au tofauti ya size na luminosity ya jua inaweza kubadilisha mambo makubwa ambayo yanauwezesha uhai wa kawaida kwetu.
Mfano Kepler-186f ni kubwa kidogo kwa size ukilinganisha na Earth hii tayari inaleta tofauti katika atmosphere, kwa kuwa atmosphere ya Kepler-186f ni nene zaidi ya sayari yetu. Hapo tayari unaweza kuona kutakuwa na tofauti ya aina ya mawingu ambayo yana-play part kubwa katika kuzuia radiations kutoka kwenye host star kwa dunia mfano ni cirrus clouds. Alafu pia Kepler 186f inazunguka karibu sana na host star yake ambayo ingawa ni ndogo kwa size zaidi ya jua letu lakini ni active na radioactive activities zake ni zaidi ya za jua letu. Bado scientists wanajaribu kuisoma vizuri kuona mambo mengine mengi ambayo katika Earth ni natural processes kutokana na kuwepo katika right place with right conditions.