Wanasema kuna mtu alipeleka maneno ya uongo eti Ummy kasikika anamsengenya Mama

Wanasema kuna mtu alipeleka maneno ya uongo eti Ummy kasikika anamsengenya Mama

kaputula

Senior Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
173
Reaction score
226
Kwa asili wanawake wanasengenya na ni wambea haijalishi ni rais. Ukimsengenya rais au akipelekewa umbea kwa rais basi kama ni mteule wake ujue ndio mwisho wako.

Nimesema hivyo maana kuna mtendaji mzuri kama Ummy Mwalimu ametemwa uwaziri na sasa amepigwa pin asigombee ubunge. Sio Tanga mjini tu wanashangazwa na mambo yanamtokea mpendwa wao Ummy hata watanzania wengi wanashangaa. Watanzania wanamkumbuka Ummy kwa utendaji uliyotukuka awamu ya 5 katika wizara ya afya.

Umakini wake na utendaji bora. Mama alimuamini pia hadi kwa ghafla alivyomtema huku wananchi wakishangaa na bila kutolewa sababu yoyote. Kuna vyeo wanabadilishwa kila mara hadi wananchi wanastasjabu. Maandamano yaliyotokea Tanga mjini wanaccm kupinga mbunge wao kukatwa asiwe mgombea yanathibitisha sifa nilizomtolea Ummy.

Sasa kuna maneno maana watu kama hawaoni sababu watatengeneza maneno. Wanasema kuna mtu alipeleka maneno ya uongo eti Ummy kasikika anamsengenya Maza. Loo Mungu tuhurumie.🤔😎
 
Ummy tangu lini alikuwa mtendaji mzuri?

Kuna tofauti ya utendaji mzuri na uchawa mzuri.

Ummy katika uongozi wake ndio CAG alitoa ripoti uwepo wa kesi zaidi ya 40 za wanaume kuutapeli mfuko wa bima ya afya wa taifa NHIF baada ya kuonyesha wameandikiwa procedure ya Caesarean Section sasa tangu lini mwanaume akafanyiwa CS ??

Kwa kashfa kama ile ilitakiwa akae pembeni tena mbali kabisa.

Tukija katika mjadala katika mtazamo mwingine watu wanapokuwa wanapigania reforms mnaona kama ni za CHADEMA pekee ila reforms ni za muhimu ndio maana hadi jana Polepole kaona sasa umuhimu wa kuondoa kinga ya mashtaka ya rais .

Tanzania mamlaka ya urais yanabidi yapunguzwe na kinga ya mashtaka iondolewe.

Mtikila alipigania mgombea huru na hadi akafanikiwa kushinda ila CCM wakaweka giza mbele , sasa leo hii tungekuwa na wagombea huru si huyo Ummy angeepukana na fedheha za kukodi watu wakaandamane kuonyesha wameumizwa na angali anakubalika bado?

Tungekuwa na reforms za kikatiba na uchaguzi leo hii rais asingekuwa na uwezo ku-jeorpadize maamuzi yote ya kamati bali ilitakiwa kuwepo na michujo ya wazi ambayo ingeepusha kadhia kama hizi mtu kutumia ugomvi binafsi kutoa maamuzi?

Kila mtu atafikiwa hata asipodai reforms jana na leo ni Kigwangalla na Ummy next ni nani sote hatujui.

No reforms no election , kataa wahuni.
 
Wengine wanasema chanzo ni hiki
FB_IMG_1756099262159.jpg
 
Kwa asili wanawake wanasengenya na ni wambea haijalishi ni rais. Ukimsengenya rais au akipelekewa umbeakwa rais basi kama ni mteule wake ujue ndio mwisho wako.

Nimesema hivyo maana kuna mtendaji mzuri kama Ummy Mwalimu ametemwa uwaziri na sasa amepigwa pin asigombee ubunge. Sio Tanga mjini tu wanashangazwa na mambo yanamtokea mpendwa wao Ummy hata watanzania wengi wanashangaa. Watanzania wanamkumbuka Ummy kwa utendaji uliyotukuka awamu ya 5 katika wizara ya afya.

Umakini wake na utendaji bora. Mama alimuamini pia hadi kwa ghafla alivyomtemwa huku wananchi wakishangaa na bila kutolewa sababu yoyote. Kuna vyeo wanabadilishwa kila mara hadi wananchi wanastasjabu. Maandamano yaliyotokea Tanga mjini wanaccm kupinga mbunge wao kukatwa asiwe mgombea yanathibitisha sifa nilizomtolea Ummy.

Sasa kuna maneno maana watu kama hawaoni sababu watatengeneza maneno. Wanasema kuna mtu alipeleka maneno ya uongo eti Ummy kasikika anamsengenya Maza. Loo Mungu tuhurumie.🤔😎
JF,kijiwe sogozi cha mtandaoni
 
Back
Top Bottom