Wanasheria nisaidieni, Baba Mzazi anazidi kuuza mali

Heri ungekuwa wewe ndo umekufa akabaki yule aliyekufa, huna faida
 
Dogo jinga weye jitambue weye!
Umri wa miaka 42 bado unaishi kwa baba yako kweli?

Kwa umri wako na elimu yako ungepaswa sasa uwe unamsaidia baba na mama yako kujikimbu kimaisha kama fadhili ya kukulea na kukosomesha na sio kudai eti 'mgao wako'!

Unataka kumrithi baba yako kabla hajafariki dunia? Mali za baba yako ni zake binafsi na ana haki ya kuzitumia atakavyo. Wewe tafuta zako, na kamwe usithubutu kufikiria kumtoa uhai ili upate vya bure...itakula kwako!
 
Kwa umri huo umeshindwa kujitambua inatakiwa uolewe.
Umeshindwa hata kupiga market ya maembe sokoni,unasubiria urithi.
 
Kuna possibility kuwa unatania tu kuchangamsha au ni kweli, kama unachangamsha unawafunza watu walio na fikra kama unavyoeleza, ila kama ni ukweli we ni mpumbavu
 
Huyu naye anaichezea sana hii nchi. Sijui kwanini Mungu aliamua tuishi nchi moja na watu wa namna hii...

Labda nijiaminishe huu ni utani tu.
 
Mkuu, mimi ni Mwanasheria. Bila kumung'unya maneno naomba nikwambie tu ukweli kwamba huna haki yoyote juu ya mali ya/za wazazi wako.

Labda niende mbali zaidi kwa kukueleza kwamba hata baba angeandika wosia na akaandika hiyo nyumba ni mali yako; kabla hajafa huwezi kuidai hiyo nyumba kwasababu bado inakuwa ni mali ya baba na/au mama, wosia unaanza kufanya mwosia (aliyeandika wosia) atakapofariki.

In the contrary, baba akikupa mali kama zawadi (gift), baada tu ya kuandaliwa na kusainiwa kwa document inayoitwa DEED OF GIFT ndiyo nyumba inakuwa mali yako hata kama baba bado yuko hai. Wosia na Deed of Gift visichanganywe.

Tafuta mali zako mwenyewe kama baba na/au mama yako walivyotafuta zao. Otherwise, hukawii kuja kumtoa roho huyo baba yako siku za usoni. Usiseme hukuonywa.
 
Nlidhan una miaka 12 kumbe 42? Malalamiko ya kitoto yanatolewa na mtu mzima , rubbish
 
Mada zako zote humu JF unalalamika kuhusu Baba yako kuuza nyumba zake. Halafu wewe umri wako ni miaka 42 ila unadai wewe bado mdogo. Hebu sema ukweli, je hadi leo huna mke na watoto wako au bado upo tegemezi? Kubwa zima unalilia mali ya babako? Tafuta vyako vinginevyo mtatoana roho kwa mali isiyokuwa yako.
 
Acha auze si Mali zake

Ulimsaidia kutafuta

Miaka 42 bado unategemea cha mzazi

Wenzako Miaka 16 tu tulianza kusebenza

Ova
 
Kwa mawazo haya, huyu jamaa atakuwa BAVICHA
 
Aisee umenishangaza sana, yaani 42yrs Graduate bila aibu bado unaishi kwa baba yako? Na huyo baba yako anauza mali kwa sababu ya tabia yako ya kudai mali ambayo hujaitolea jasho,
Tafuta shughuli ya kufanya achana na Baba yako na mali zake.
Unapo toka povu kumbuka huyo ninbaba yake mzazi ambaye ana jukumu la kuhakikisha mtoto wake anaishi katika mazingira mazuri wakati wote pasipo kujali umri,

Tujifunze kwa wenzetu mataifa ya asia ambao hawajali swala la umri wa watoto wao bali wao hukumbatiana kuhakikisha wote wanaishi maisha bora na wengi wanafanikiwa sana katika hilo.

Mohammed dewij leo ni tajiri mkubwa afica kwa sababu ya mali za wazazi wake alizo zikuta na yeye na kizazi chake hawataishi maisha ya dhiki kwa sababu wanaamini katika kusaidiana na kutunza mali ambayo itarithishwa hata vizazi vijavyo.

Ndio maana nchi nyingi za africa umaskini hauta isha kwa sababu tuna aminishana kwamba jukumu la mzazi ni kuzaa tu na sio kuhakikisha huyo aliye mzaa anaishi maisha bora.
 
Ana hiari kukupa urithi. 42 yrs kakuvumilia sana.
 
Si nilisikia kuna mzee huko Arusha aliamua kubomoa nyumba kabisa.
Nadhani aliyendika uzi huu analeta stori tu. Anataka kujua kama anaweza kupata urithi kwa baba yake.
Urithi wa elimu aliokwisha kupatia unatosha, kukugawia mali zake ni hiari yake tu.
Kama ni kweli, at 42 bado unakula na kulala kwa baba - hao dogos unawapata kweli? Una uwezo wa kuwasomesha mashairi wakakukubali kweli? Nahisi una matatizo zaidi
 
Punguani wewe,si utafute za kwako??? Mwanaume mzm umekalisha wowowo kwa baba yako inasubiri urithi,we wanao utawarithisha nn ukiwa umri huo inakaa kwa baba yako????
 
Tafuta zako, kwanza miaka 42 unatafuta nini kwenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…