Uchaguzi 2020 Wanasheria, Tusaidieni. Je, kuna uwezekano wa Tundu Lissu kuenguliwa na NEC kugombea Urais kwa kutumia kigezo cha Uadilifu wa Mke wa Kaisari?

Uchaguzi 2020 Wanasheria, Tusaidieni. Je, kuna uwezekano wa Tundu Lissu kuenguliwa na NEC kugombea Urais kwa kutumia kigezo cha Uadilifu wa Mke wa Kaisari?

Kwa maoni yangu mimi lay, sioni kikwazo yeye kugombea. Hata hivyo kwa mtazamo wa wanasheria hayo no mawazo ya lay person
 
Mchinjaji akiwa na nia ya kuchinja huchinja akiamini katika uwezo alionao wa kuchinja, na kisu hufuata muelekeo wa shingo ilipo ili kukamilisha lengo la mchinjaji. Mchinjwaji huwekwa tayari na kudhibbitiwa ili achinjwe. Lakini kazi kubwa ni kuchagua au kudhibiti mwelekeo wa damu itakapoangukia.
 
Wewe unatumika siyo bure!
Waache kumuengua anayegawa rushwa hadharani waje wamuengue Lissu?
Hakuna ushindi wa mezani hapa, kila kura lazima ipiganiwe!

Mods this is a malicious thread iondolewe
Huyu anataka kuset tune kwa watawala wafanye udhalimu kama alivyoset tune Kabendera akapata matatizo
Naomba hii mada ya kichawi iondolewe hapa!
Huyu katumwa na wabaya wa Lissu aje kupima upepo na kuwaandaa watu kisaikolojia.

JamiiForums ndio kituo chake cha kazi.
 
Kuna Jambo lingine pia la kuliangalia,

Nini hatma ya kesi zake zilizojaa mahakamani kwa mfano akashinda.

Ndio tuseme kuwa ataamrisha mahakama izifute ??
Kesi zitasimama mpaka pale atakapotoka madarakani!
Hii ni kwa mujibu wa sheria zilizokuwepo!Sasa hivi CCM imetunga sheria za kuwalinda wakubwa,ambapo wakubwa ni marufuku kushitakiwa kwa jambo lolote!Hivyo kesi zitafutika by default!
 
Mambo ya sheria nawaachia wana sheria ila maoni yangu hata kama vipo vigezo vya Lisu kuondolewa kugombea ni bora wamwache agombee kuliko kumpa kiki asiyostahiki maana uwezo wa kushinda kiukweli hana.
 
Pasco, hakuna kigezo chochote cha kuweza kumzuia Lissu asigombee pamoja na woga wenu.
Na kama unazungumzia maadili na usafi wa mtu ili kupitishwa kugombea , basi kuna mmoja ingebidi hadi fomu zake zilitakiwa kuchomwa moto.

Ni mwizi sana kauza mpaka nyumba za umma, muongo na hafai nafasi ya heshima, mzinzi mno kabaka mpaka shemeji zake na kuwazalisha, amefukuza watu kazi kisha wamelamba mchepuko wake nk nk.

Na ukirudi tena na vihoja vyako hapa Pasco basi nitamtaja huyu mtu
 
Paschal

Umekumbwa na nini ndugu? Soma ulichokiandika ujitathimini.

Unaomba msaada kwa wanasheria wakati huo huo wewe unatoa hukumu? Kama hukumu ulikuwa nayo, ya nini kutuuliza tena?

Umeandika kama mtu huru (unajificha) wakati huo huo ukada wako unaudhihirisha!!

Soma tena sheria, Lissu mwenyewe alishafafanua (HAFUNGWI MTU HAPA speech) aliyaeleza haya kwa ufasaha ni namna gani wanaweza kumuengua. "Makosa ya uchochezi hayamzuii mtu kugombea uraisi kwa namna yoyote ile. Iwe ameshindwa kesi au anatuhumiwa"!!

Vinginevyo umeleta bandiko hili kupima upepo kwa maagizo maalum!!
 
Mke wa kasisari anahusika vipi upatikanaji wa kaisari? kaisari hajapatikana, mke wake anahusika vipi? Ni wapi katika katiba yetu inayosema ukigombea lazima mke wako awe mtu wa maadili yasiyo na shaka? Ni wapi... Innocent till proven guilty.. hata wakimpata na hatia, mlolongo wa appeal ni mrefu, haki yaki hainyimwi wala kuzuiliwa na guilty ni mpaka pale appeal process zote zimekuwa exhausted.

Kosa la kumuondoka Lissu ni hilo tu la kukiukwa taratibu na miendeno ya maadii ya viongozi wa uma kama wanaweza kuli-prove.. wamashikie hapo tu ...

Paskali, wewe umesoma sheria na unaijua katiba ya Tanzania, labda ututajie kipengere kinacho wapa nafasi NEC ya kumuengua , sio hizi dhana za kufikilika...
 
Back
Top Bottom