Uchaguzi 2020 Wanasheria, Tusaidieni. Je, kuna uwezekano wa Tundu Lissu kuenguliwa na NEC kugombea Urais kwa kutumia kigezo cha Uadilifu wa Mke wa Kaisari?

Uchaguzi 2020 Wanasheria, Tusaidieni. Je, kuna uwezekano wa Tundu Lissu kuenguliwa na NEC kugombea Urais kwa kutumia kigezo cha Uadilifu wa Mke wa Kaisari?

Ulishaonesha upo upande gani haya ya lissu hayakuhusu...0
 
Unapoamua kugombea urais, you have to choose in between kugombea urais au kuendelea kuwa mwanaharakati, you can't be both, mwanaharakati na mgombea urais. Ukichagua kuwa mgombea urais, uanaharakati unauweka pembeni, you speak, talk and behave like a president in waiting!, huwezi kusema hovyo, huwezi kutukana watu, huwezi kutoa tuhuma bila ushahidi, huwezi kuibagaza nchi yako kwenye media za mabeberu, halafu ukategemea utapitishwa tuu hivi hivi kugombea urais!.

Wasikitisha ndugu yangu,
Nilidhani mada inaomba maoni ya kisheria kama ilivyo kwenye heading yake.

Kumbe tu umeshindwa kuzuia 'mapenzi' yako kwa kwani ushaona UWEPO wa Lissu umeleta hewa mpya kwa wananchi walokuwa wamebanwa pumzi. Mafarisayo nao walikuwa hivihivi, na sio miaka mingi sana iliyopita Makaburu SA nao walikuwa hivyo hivyo.

Sasa, kama mafarisayo hamtakujaamini yatakayo tokea na kujikuta mnatunga maneno ambayo kwa zaidi ya miaka 2000, yameendelea kupuuzwa kwa kuwa ni ya kubumba ili kujitoa aibu.

Ni matumaini yangu kuwa hatimae mtakuja msikiliza Mungu na KUTUBU kwa yote mliyofanyia Lissu na watanzania wengine walioamua kusema kweli ili kuiokoa nchi yao iliyokuwa yapotezwa. AMEN
 
Kumuengua Tundu Lissu kugombea uraisi wa JMT ndio njia pekee ya ccm kushinda uchaguzi huu. Na watalisimamia hilo ili litimie.
Ila Mungu si wa ccm; ni wa wote.

.....Siyo "ili litimie" bali, labda "ili kujaribu bahati yao kulitimiliza"

Otherwise, there's no way Tundu Lissu aweza kuenguliwa iwe kisheria ama kimaadili...!!
 
CCM wakifanya hivo nitawadharau Sana. Approach waliyoichagua ya kupiga kimya ime work out. Lissu ni Kama anafukuza upepo kila anachojaribu kinabuma, Watanganyika ni Kama hawamuoni na unaweza kuona yeye na wafuasi wake wameanza kupaniki, hawapati response waliyotegemea Sasa wanaanza kutumia nguvu kubwa ikiwemo hata humu.
Isipokuwa tu Serikali inapaswa kuwa makini baada ya watu kuonekana kutokumtilia manani anaweza kufanya chochote kibaya ili mradi kutafuta millage na huruma. Jana alisema anatishiwa, wenye akili wanajua what he is going to do next!

Aliwahi kusema anatishiwa vyombo vya usalama vikadharau kilichotokea tunakifahamu. Sasa wewe ni nani useme hatishiwi wakati kila siku akina Musiba wanasema hadharani kabisa na hawaulizwi chochote. Hii nchi bwana
 
Mkuu P, mara ya mwisho ulipokuwa star tv tuongee asubuhi ulisema ukishindwa ubunge utaacha kuandika mabandiko yanayohusu politics,vipi unakumbuka lkn?
 
Pole sana. Hicho ndiyo kitu na uzee wako kama Mimi unaweza kuwaza? Mimi ni CCM damu ila at times ni lazima kuwa objective bila ushabiki uchwara. Huwa ninakuheshimu sana ila leo umekwaza bro.
 
Akienguliwa safari tupo tayari kutangulizwa Mbinguni na policeccm. Halafu Ccm ibaki na Nchi yao waliyopewa peke yao na Mungu.
Paskali kuna wakati nilikuwa nakuona kama kaShivji kadogo, lakini kwa uzi huu sasa nakuona kama mtoto aliyeko chekechea. Au ni madhara ya kazi za wajumbe?!!
 
Tulia acha kuruka ruka,Lisu is innocent until proven guilty, kwani wewe na ccm mnaona wivu gani akishinda uraisi na akafutiwa hayo mashitaka mnateseka nini


Kwa uelewa wangu mashtaka yote yanayomkabili TL, hata kama atapatikana na hatia hatakosa sifa za kugombea.

Kama Mbowe, Bulaya, Matiko, Mdee, Msigwa, Heche...wangekosa sifa za kugombea kutokana na hukumu zao, then ningekuwa na wasiwasi kwa TL.

Utakumbuka kwamba wale walikuwa na kesi mbaya kuzidi kesi ambazo TL anakabiliwa nazo ktk mahakama mbalimbali.

Kuhusu lile kosa la maadili ambalo Ndugai alimfukuza nalo ubunge, TL hakuhukumiwa na baraza la maadili hivyo amekwepa kizingiti kikubwa kuliko vyote ambavyo vingemkabili.
 
Wewe unatumika siyo bure!
Waache kumuengua anayegawa rushwa hadharani waje wamuengue Lissu?
Hakuna ushindi wa mezani hapa, kila kura lazima ipiganiwe!

Mods this is a malicious thread iondolewe
Huyu anataka kuset tune kwa watawala wafanye udhalimu kama alivyoset tune Kabendera akapata matatizo
Naomba hii mada ya kichawi iondolewe hapa!
Hata mimi nilipoona heading ya hii mada nikaona ina nia ovu nyuma yake.
 
Wajumbe wamefytau ubongo wa Mayala amebaki anaunyaunya tu..
 
Mbona Lissu kashaongelea hili kwa urefu. Hakuna sheria kama hizi
 
Paschal

Umekumbwa na nini ndugu? Soma ulichokiandika ujitathimini.

Unaomba msaada kwa wanasheria wakati huo huo wewe unatoa hukumu? Kama hukumu ulikuwa nayo, ya nn kutuuliza tena?

Umeandika kama mtu huru (unajificha) wakati huo huo ukada wako unaudhihirisha!!

Soma tena sheria, Lissu mwenyewe alishafafanua (HAFUNGWI MTU HAPA speech) aliyaeleza haya kwa ufasaha ni namna gani wanaweza kumuengua. "Makosa ya uchochezi hayamzuii mtu kugombea uraisi kwa namna yoyote ile. Iwe ameshindwa kesi au anatuhumiwa"!!

Vinginevyo umeleta bandiko hili kupima upepo kwa maagizo maalum!!
Huu uzi unachochea chuki kwenye jamii. Ni uzi uliojaa nia ovu.
 
Kwa kuuma na kupuliza hujambo ,wamekutuma kupima upepo maana Jiwe Anaogopa Sana ushindani hata wakati akiwa mbunge alikuwa anatumia hila za kila aina kuwaondosha wapinzani wake.To make your point clear and I quote 'no body is guilty untill proven guilty in the court of law '.Ccm mmezoea vya kunyonga vya kuchinja hamuvuwezi.Msijaribu huo ujinga the world is watching over.
 
Back
Top Bottom