Tetesi: Wanasheria tusaidieni.

Tetesi: Wanasheria tusaidieni.

Mbunge Luswe

Member
Joined
Jan 23, 2018
Posts
56
Reaction score
23
Salam wakuu.
Ikitokea mtu akahukumiwa kwa kosa la mauaji, hukumu ya miaka 30 jela. Na akatumikia yote. Siku anatoka jela ghafla akamuona mtu aliye tuhumiwa kuwa aliimuua, akapata hasira na kumpiga hadi kumuua. Kisheria hii inakuwaje?? Atahukumiwa tena au??
Karibu wakuu.
 
Duu ila kweli ngoja wanasheria waliweke wazi kweli maana duuu inauma Sana 30 yrs!!
 
Salam wakuu.
Ikitokea mtu akahukumiwa kwa kosa la mauaji, hukumu ya miaka 30 jela. Na akatumikia yote. Siku anatoka jela ghafla akamuona mtu aliye tuhumiwa kuwa aliimuua, akapata hasira na kumpiga hadi kumuua. Kisheria hii inakuwaje?? Atahukumiwa tena au??
Karibu wakuu.
Sasa akihukumiwa tena ina maana atakua amehukumiwa vifungo viwili wakati alieuliwa ni Mmoja tu,
Hapo inabidi abaki uraiani
 
kidunia utafanya kama alivyofanya amitabh bachchan kwenye andhah kanoon, kisheria tuwangoje wanasheria.
 
Salam wakuu.
Ikitokea mtu akahukumiwa kwa kosa la mauaji, hukumu ya miaka 30 jela. Na akatumikia yote. Siku anatoka jela ghafla akamuona mtu aliye tuhumiwa kuwa aliimuua, akapata hasira na kumpiga hadi kumuua. Kisheria hii inakuwaje?? Atahukumiwa tena au??
Karibu wakuu.
Haya ni maswali ya story za vijiweni haya! Ila kukuelimisha ni hivi: Anapotoka kama amemwona yule mtu aliyedhaniwa kuwa aliuawa inatakiwa yeye afungue kesi ili Jamhuri imlipe fidia kwa muda aliopoteza akiwa jela bila kosa! Na kama uvumilivu utamshinda na akiamua kujichukulia sheria mkononi basi atakamatwa tena na atafanyiwa kesi mpya ya mauaji japo kwenye hukumu ya pili anaweza kupunguziwa adhabu kulingana na mazingira aliyotenda kosa! Hiyo itategemea mazingira ya kuua.
Marekani imehatokea mara nyingi watu wakatumikia jela miaka zaidi ya ishirini na baadae ikaja kuonekana kumbe hawakuwa na hatia. Wengi walilipwa fidia kubwa na serikali.
 
Hukumu za mauahi huwa hazitolewi mapema. Zina mchakato mrefu sana ili khniridhisha kuwa aliyedaiwa kuuawa ameuawa.
 
Back
Top Bottom