Mi mzee wangu si mtu wa kukaa na mimi na kuongea na mimi kwa sana ila anaongeaga kwa ufupi sana. Wakati namaliza chuo naanza kazi akaniambia mwanangu usiwahi kuoa nilishangaa la pili alilo niambia akaniambia mwanangu USITHUBUTU KUMUOA MWANAMKE ALIYE KUZIDI KIPATO mzee wangu akanyanyuka akaingia ndani na kusikiliza zilipendwa kesho yake akaenda morogoro matombo kulima ndizi zake.
Leo hii kupitia ugomvi wa jide na gadner ndio nimegundua kwa nini mzee aliongea vile, gadner alivyokuwa clouds alikuwa analipwa mshahara, alikuwa analipwa kupitia matangazo, alikuwa MC na alikuwa anaandaa matamasha yake yy mwenyewe kwa hiyo kwa kifupi alikuwa anaingiza ela tena ndefu tu, nawashangaa hawa wanao mwita gadner MARIO.
Kosa kubwa la gadner alilolifanya ni KUACHA KAZI CLOUDS na kwenda kuendeleza kazi za mke wake na yy kusahau kuijenga kesho yake, huu ulikuwa upendo mkubwa sana kujitoa kwa ajili ya mwengine na kujisahau ww mwenyewe na kweli gadner alikuwa bega kwa bega kummanage mke wake ktk shughuli zake.
Leo hii gadner ameachaana na mke wake hajadai hata senti tano yoyote mahakamani, ila kama ingekuwa kafanyiwa jide ungesikia taasisi za wanawake zikilalamika na vipindi wangemtengenezea ili wagawane mali iliyopatikana ktk kipindi cha miaka 15 gadner akamua kukaza na kuanza moja upya kama mwanaume.
Jide kama kawaida yake hakumwacha hivi hivi na nyimbo za kejeli, ingawa hakumtaja ktk nyimbo hizo ila maneno na video ukiungaisha na yule jamaa aliyeondoka na CD unapata picha halisi, ila jamaa bado kakaa kimya. Japokuwa wanaume wameubwa na kidaka tonge (koromeo) kwa ajili ya kuvumilia na ndio maana sisi wanaume tuna mengi sana mioyoni mwetu Kutokana na matatizo tunayoyafanyiwa wanawake ila sometime Kuna ukomo gadner nae binadam anaumia,kweli gadner aliteleza lkn nae hakumtaja jina.
Kwanza nashukuru gadner yupo huru jide aliubaka uanamme wake, alishindwa kuijenga kesho yake, gadner naona alivyokuwa na jide alikuwa kama zezeta ila sasa yupo huru. Sio huyo tu gadner mi hapa mtaani Kuna wazee wawili wanafikia miaka zaidi ya hamsini, ukiwaona hawa wazee kama mazezeta wapo wapo wanawategemea wako zao, mmoja mke wake ana saluni mwengine mke wake yupo bank kuu mi tangu nasoma O-Level mpaka namaliza chuo sijawahi kuona wakifanya cha maana wana kazi ya kuzurula tuu leo wakiachwa hawana pa kuanzia bora gadner anapo pakuanzia.
WANAUME TUTAFUTE VYETU KUEPUKA UZEZETA, DHARAU KUTOKA KWA MWANAMKE ALAFU UKIWA NA CHAKO UNAKUWA NA SAUTI NA HUU NDIO UANAUME GADNER SASA HIVI YUPO HURU KWANI AMERUDISHA UANAUMME WAKE KWA KUFIGHT KWA AJILI YA MAISHA YAKE NA FAMILIA YAKE.