Fumadilu Kalimanzila
JF-Expert Member
- Dec 10, 2016
- 1,770
- 5,423
Law is an art, na sisi kama Taifa katika Sheria tumerithi doctrines mbalimbali kutoka common law na hivyo suala la kujua Kiingereza (English) haliepukiki!
Tanzania tunajenga utamaduni wa ajabu sana kwamba kama mtu fulani au kikundi fulani hakijui jambo fulani badala ya kuwekeza katika kujifunza jambo hilo basi kunajengwa mazingira ya kubadili jambo hilo kutoa nafuu kwa wasiojua jambo hilo.
Hili la kubadili sheria zetu zilizoandikwa kwa Kiingereza kwenda kuandikwa kwa Kiswahili ni mojawapo.
Ukifuatilia kwa makini miaka ya hivi karibuni hapa nchini mwetu kumekuwa na kasumba ya ajabu sana kwamba kujua Kiswahili ndio uzalendo na kutumia au kujua Kiingereza (English) siyo uzalendo!
Ukichunguza vizuri wanaopigania dhana hiyo hata Kiswahili fasaha pia hawajui.
Mimi naamini muda wote kuwa suala la kutokuwepo au kukosekana haki katika sheria zetu haliko katika lugha iliyotumika katika uandishi wa sheria zetu bali ni katika contents (maudhui) ya sheria zetu!
Mfano, sheria zetu zinapinga matokeo ya kura za Rais kupingwa Mahakamani, hivi ukiandika sheria hiyo leo kwa Kiswahili basi itabadilika na kutoa haki hiyo ya msingi inayonyimwa kwa Watanzania?
PhD za akina Mwigulu Nchemba zitumike kuleta hoja zilizofanyiwa Tafiti za kina kwenye public domain na waache kufanya kazi kwa mihemuko au kumfurahisha mtu fulani!
Tatizo kubwa tulilo nalo kwa sasa ni Watanzania wengi na hasa Viongozi kutojua kiingereza (English) kwa ufasaha!
Tutafute ufumbuzi wa tatizo hilo badala ya "kuhamisha magoli" ili kujipa ushindi wa bure!
Dunia inakwenda kwa kasi sana na wala haiwezi kutusubiri sisi Tanzania na mawazo yetu ya ajabu ajabu!
Kina Mwigulu Nchemba wanawadanganya "wanyonge" kuwa wanawapenda na wanapigania haki zao ikiwemo ili la kubadili sheria zetu kuwa kwa Kiswahili wakati wao wanasomesha watoto wao FEZA SCHOOLS (English medium) ambako wanalipa ada ya Primary School ya Tshs. 5 milioni hadi 7 milioni kwa mwaka!
(Akili za kuambiwa changanya na za kwako: by Mhe. Jakaya M. Kikwete).
Mambo mengi tumeanza kushindwa kuwasiliana na Dunia kwa sababu ya kutojua lugha kwa ufasaha.
Huwezi kusema kila jambo utabeba Wakalimani, kuna mambo mengine ni "top secrets" unahitaji kuwasiliana "one to one"!
Chukulia hata chaguzi zetu kunatokea makando kando mengi lakini wananchi, wanahabari hata baadhi ya wanasheria hawawezi ku- communicate na Dunia ili kueleza tatizo lilipo!
Ukiangalia vyombo vikubwa vya habari Duniani kama vile CNN, BBC, Aljazeera n.k vinawahoji sana watu wa Africa kutoka katika mataifa ya Nigeria, Ghana, Kenya, Uganda n.k. they are eloquent and can talk to the World!
Hapa kwetu mwananchi,mwanahabari au hata kiongozi mkubwa akihojiwa utasikia, " Zeeee,Zeeee, Zeeee, Zisi , Zisi, To meeee, To meeee, Onole (only)! Upuuzi mtupu!
Wakati fulani huko nyuma Mwl. Julius Nyerere alialikwa na akina Prof. Mugyabuso Mulokozi wa TUKI pale UDSM na ajenda zao za kutumia Kiswahili kufundishia elimu ya juu na wakazungumza Kiswahili kigumu kuliko hata Kiingereza. Kwa mshangao wao Mwl. Nyerere aliwaambia Kiingereza ndio Kiswahili cha Dunia hii.
Hivyo mimi pia nawambia akina Mwigulu Nchemba na the like tusidanganyane! ni kweli tunapaswa kujifunza Kiswahili chetu na kukienzi lakini hatupaswi ku- undermine role ya kiingereza (English) katika Dunia tuliyonayo sasa!
After all ni aibu pia kuwa na Waziri wa Sheria asiyejua chochote katika sheria. Hii inawezekana na kuonekana kawaida tu kwa Nchi kama yetu hii ambayo fundi mchomelea vyuma (Welder) anaweza pia kuwa Daktari (Tabibu) hata kama hajasomea taaluma hiyo!