Wanasheria wa Reginald Mengi wakutana na waandishi wa habari na Kumjibu Rostam Aziz

Wanasheria wa Reginald Mengi wakutana na waandishi wa habari na Kumjibu Rostam Aziz

Status
Not open for further replies.
Ni vizuri malumbano haya yakaachwa yaendelee ili siri nyingi tusizozijua zifunuliwe. Nadhani mwisho wa ufisadi haukombali sana.



You are right... Ninachojua kuna watu watafanyiwa umafia (am not praying for this!) na kama si hivi, basi tutarajie anguko la ajabu katika serikali ya awamu hii kabla ya uchaguzi. Something needs to be done ASAP!
 

binmgen said:
mengi hana jipya la kuongea, hana ushahidi wowote wa madai yake, ila ni kama kawaida yake ni kulialia na kutaka wananchi wawe pamoja naye wakati yeye mwenyewe ni fisadi nyangumi hapa hakuna wahindi wala wamasai fisadi ni fisadi tu! umezowea kuparamia paramia watu lakini mara hii umeparamia mbuyu, hatuwezi kukuamini maneno yako ya porojo eti kwa kuwa wewe mweusi yeye mweupe, ndio unakotupeleka huko. hadi sasa ra 3 mengi 0


uchizi si lazima uokote mkopo hata kumtamani mzazi wako...nao ni uchizi
 
HEBU SOMA KITU HICHI ALICHOANDIKA MH MAHANGA



Wewe Ngurumo unajua pia kwamba nchi na taasisi wafadhili duniani hawapeleki misaada kwa nchi ambazo serikali yake haipangi bajeti yake kwa vipaumbele vya kulenga wananchi wake (pro-people budget) wala nchi ambapo utawala bora ni zero. Lakini angalia jinsi TZ inavyopata misaada mingi kuliko nchi nyingi kutokana na vigezo hivyo kuwaridhisha wafadhili. Hivi wao wameshindwa kuona hayo mnayoyaona nyie ya utawala mbovu na kutowajali wananchi? Hapana, sikubaliani na hilo.


Tatizo ni kuwakosanisha wananchi na serikali/chama tawala kwa kushikilia mambo au jambo ambalo kwa ujumla wake halina tija kubwa sana kwa watanzania walio wengi bali lina mtazamo wa ubinafsi, chuki, wivu na uelekeo wa kisiasa.

Milton

Huyu Milton Mahanga si ndiyo nasikia Vicheche havikaziti kwake? Hi hiii hiiii.

Kwanza aseme kama hilo PhD lake ni la kweli au FEKI. Kama anatudanganya kuwa ana PhD wakati kanunua ONLINE, mengine yote yanaanza kuleta wasiwasi.

Si ndiyo huyu alibwabwaja pumba kwenye ATCL kuwa watu wana WIVU? Naona hilo la wivu analipenda sana. Kama watu wanafumbuliwa macho si kuwa wanawachonganisha. Somo lishaanza kueleweka na soon dawa yenu itapatikana.

Tanzania ni nchi TAJIRI sana. Kama tungelipata Rais mwenye akili ya KI-PUTIN basi leo hii tungelikuwa tunakula mzigo si kawaida na kuchakalika hasa kuongeza viziro kwenye account zetu banki. Naombea tupate Rais Mbabe na mtemi kama PM wa Malesia ili atunyooshe sisi Watz na kuwaonyesha wageni wote mahali pao. HATUHITAJI KUTEMBEZA BAKULI KUOMBA FEDHA. Hatutaki kuona Rais akitembea na bakuli. Kila kitu kipo Tanzania ila tumewapa wengine na sisi kwenda kuwa akina MATONYA.

Siku hiyo imekaribia.
 
Huyu Milton Mahanga si ndiyo nasikia Vicheche havikaziti kwake? Hi hiii hiiii.

Kwanza aseme kama hilo PhD lake ni la kweli au FEKI. Kama anatudanganya kuwa ana PhD wakati kanunua ONLINE, mengine yote yanaanza kuleta wasiwasi.

Si ndiyo huyu alibwabwaja pumba kwenye ATCL kuwa watu wana WIVU? Naona hilo la wivu analipenda sana. Kama watu wanafumbuliwa macho si kuwa wanawachonganisha. Somo lishaanza kueleweka na soon dawa yenu itapatikana.

Tanzania ni nchi TAJIRI sana. Kama tungelipata Rais mwenye akili ya KI-PUTIN basi leo hii tungelikuwa tunakula mzigo si kawaida na kuchakalika hasa kuongeza viziro kwenye account zetu banki. Naombea tupate Rais Mbabe na mtemi kama PM wa Malesia ili atunyooshe sisi Watz na kuwaonyesha wageni wote mahali pao. HATUHITAJI KUTEMBEZA BAKULI KUOMBA FEDHA. Hatutaki kuona Rais akitembea na bakuli. Kila kitu kipo Tanzania ila tumewapa wengine na sisi kwenda kuwa akina MATONYA.

Siku hiyo imekaribia.

Mkuu huu ni ukweli unao uma!
 
Zile zinazoitwa siri za serikali sasa ndo zinaanza kupakuliwa, Mzee Mengi tupakulie pilau hilo tunalisubiri! Umefanya kazi nzuri ya kumlazimisha bubu kusema.

Jamani hebu someni makala ya Manyerere Mtz Jumapili ya jana na linganisheni na maelezo ya RA!
 
Kweli unahasira nae sana, ukweli ni kuwa wote(Mengi na Rostam) ni MAFISADI. Sasa sijui anataka kutuambia nini sisi watanzania masikini.

.
Sio na hasira nae ila inakuwaje watu wengine wampe point mengi wakati hakuonyesha ushahidi wowote ktk madai yake kama alivyofanya mwenziwe? Ndio maana nasema hadi hivi sasa R A Ndiye anaemsaidia Raisi ktk vita hii ya ufisadi kwani tayari amepeleka ushahidi wa ufisadi MENGI ktk vyombo vya sheria wanachi waache ushabiki huyu muhindi au huyu mmasai fisadi ni fisadi tu! mengi acha kulialia kama unafilisika kubali matokeo
 
Last edited:
Nani anasema Mengi hana jipya? Ni nani nambieni? We Piddy unatoka nchi gani?

Hv Umekubaliana na upumbavu aliokuwa anasema Yule fisadi papa jana? Unakubaliana

na ile hoplessness kweli?

Umeona wapi kukopa ni ajabu? Kama kuna shida na kukopa au kulipa hilo ni tatizo la

banks zetu.

Shida ni kudanganya nchi kwa kufungua non-existing companies na kuzichukulia pesa

lukuki za nchi. Sijaona material thing katika kupayuka kwa yule mhindi. Alikuwa

anauza nyago tu huku waswahili wenzako wakimlinda mgongoni kama mfungwa.
 
duh hii si mchezo...luks like ni vita ya "mapapa" na "manyangumi".....
 
Nanianasema Mengi hana jipya? Ni nani nambieni? We Piddy unatoka nchi gani?

Hv Umekubaliana na upumbavu aliokuwa anasema Yule fisadi papa jana? Unakubaliana

na ile hoplessness kweli?

Umeona wapi kukopa ni ajabu? Kama kuna shida na kukopa au kulipa hilo ni tatizo la

bakns zetu.

Shida ni kudanganya nchi kwa kufungua non-existing companies na kuyachukulia pesa

lukuki za nchi. Sijaona material thing katika kupayuka kwa yule mhindi. Alikuwa

anauza nyago tu huku waswahili wenzako wakimlinda mgongoni kama mfungwa.

Si hilo tu sana sna kaja kutueleza kwamba si yeye peke yake fisadi kuna na wengine!, kwani hilo lina muondolea hatia ya kuwa fisadi?

Narudia tena na tena Rosatamu Azizi ni fisadi papa, ameharibu nchi yetu kwa kumuweka raisi mfukoni, kisa alikwapua hela zetu zikasaidia kumuingiza ikulu,

Anatumia hiyo turufu kumblack mail Jk, hana sauti wala analo weza fanya juu yake, Sisi wananchi wenye uchungu na pesa yetu hatuogopi cha nani wala nani, this time Fisadi RA has to face it!

Hata aajiri watu wa kuja kumpigia debe na kumsaifsha kila kona, sisi wazalendo tusio lipwa hata senti tano tutakula nao sahani moja, na tuta waamsha watu mitaani wamjue mwizi wetu, mahakama ikipindisha sheria, huwa tunazo sheria tunazo tumia kuwahukumu wezi wa kuku kule manzese, hayuko kisiwani zitamfikia tu! Tumechoka!
 
Yawezekana ili kuweza kuelewa nguvu za RA ni lazima tuchore jedwali moja hivi na kujaribu kuweka ndani yake watu ambao wanahusiana au wamehusiana moja kwa moja na RA na sasa watu hao wako madarakani au kwenye nafasi fulani za maamuzi.
a. Wale aliowafadhili na kuwasaidia kushika au kudumisha nafasi za kisiasa.

MATOKEO:

16.Mahanga - Ubunge.



Huyu ndiyo Makongoro Mahanga, ambaye imesemwa kuwa kawekwa hapo kwa nguvu ya Rostam Aziz.
 
Jamani updates kwa mlio karibu na Movenpick? Ukimwa huu unanifanya nipate shaka juu ya uhakika wa Mengi kuwa na Press conference leo!
 
Nyie ndio mnawaponza hawa wazee kwa kukazania jicho kwa jicho.

Mimi nimeangalia conference zote mbili, kwa mawazo yangu RA alijiandaa na kama ni mahakamani ametoa utetezi ambao ni more convincing kuliko Mengi. Watu wa RA walifanya kazi nzuri ya kumwandalia mashambulizi yake.

Mengi awaachie hiyo kazi washauri na wataalamu wake kutayarisha majibu pamoja na documents zote, yeye kazi yake iwe na ku deliver.

Mkuu Mtanzania, nakuaminia kwa mambo mengi. Pamoja na imani yangu kubwa kwako, sitarajii watu wa aina yako kutaka Mengi aweke ushahidi kuhusiana na Richmond/Dowans, EPA (Kagoda), Rada, Helikopta za Jeshi, magari ya jeshi, Mchuchuma na Liganga, NSSF/PSPF, CIS na kadhalika. Nadhani ingekuwa documentary. Alichofanya Rostam ni kusoma akili za watu wengi kuwa hawana kumbukumbu kuhusiana na yote hayo (ambayo yamo JF) ikiwa ni pamoja na Ripoti ya Mwakyembe iliyomtaja kwa jina na cheo (yeye anasema haikumtaja) na pia akijua fika kwamba si watu wote wanasoma Mwanahalisi, Thisday, Kulikoni na RaiaMwema (wengi wanasoma Kiu na Ijumaa) na si wengi wanaingia JF (wanachati na kuingia Ze Utamu), kwa hiyo akasema Mengi kasema uongo na yeye ni safi na akamwaga data na KUHUTUBIA TAIFA kupitia televisheni ya taifa (kwa kulipia) tena prime time (baada ya taarifa ya habari). Hapo wananchi wengi ambao huwa wanasoma Kiu na Ijumaa na ambao wanamwamini Mengi kama mkombozi wao, watasikiia na kuuona kwamba Rostam kammaliza kwa kumwaga data.

Sina hakika kama Sophia Simba atalizungumzia hili. Hatothubutu kwa kuwa ni sehemu ya maandalizi ya alichosema RA na muendelezo wake. Hawezi kusema kwa sababu hakusema Mkapa, Lowassa, Chenge, Warioba waliposakamwa na amefurahia Mahalu, Jeetu Patel, Mramba, Mgonja, Maranda, Chenge (rada) na baadaye Warioba kwenda mahakamani na si Rostam (Kagoda),wala Tanil (rada) maana hawa ni wateule ambao hawatakiwi wachukie, maana wakichukia "Mabomu ya Mbagala yatalipukia Kempiski". Historia itatuhukumu baadaye kama ambayo sasa inatuhukumu kwa tuliyoyasema mwaka mmoja uliopita kwamba, "Nchi inayumba"

Nchi sasa inayumba
 
Atueleze leo pesa alizokopa za kuzalisha hakuna matata zimeishia wapi naona rostam hakusema hili jana pamoja na ile mitambo ya kiwanda ni serikali imemsaidia kujenga kiwanda kile akakifilisi

Kama hivi ndivyo bazee, kila mtu ni fisadi duniani. Msipotoshe maana kukopa ukiwa mfanyabiasha hauwezi kuwa ufisadi.. Mimi nina habari kuwa S. Bahresa alikopa Barclays bank zaidi ya Tzs Bil 45 zika mshinda kulipa, akaomba akopeshwe tena Tzs kama 37 hivi ili aweze kufanya biashara itakayo muwezesha kurudisha hata zile 45 za kwanza... akapata nazo anaendelea kuzilipa kwa kusuasua!!! Je na yeye ni fisadi??
Kama kweli ndio ukomo wenu wa kufikiri basi hatuna cha kuwafanya, ila kama ni mapandikizi ya mafisadi mjue hamuitendei haki nchi yenu.
 
Jamani kati ya hawa yupi ni hatari zaidi? Anayechuma hela tanzania na kutumia hapa hapa Tanzania au anayechuma hapa na kwenda kuweka nje?
kama Rostom anadai Mengi alikopa hajarudisha hiyo siyo hoja ya msingi.Kukopa ni haki ya kila mtuy na ni makubaliano kati ya benk na mteja hiyo si kuhujumu uchumi. Fidadi kama hao Mapapa ni wale wanaotumia njia za ulaghai kujipatia mali na utajiri wao.Kutumia sehemu ya kodi zetu kujinufaisha wenyewe, waache walumbane tufaidi mengi zaidi kisha wakimaliza ndiyo tutachambua mchele na pumba
 
Nadhani ni wakati muafaka wa kufuata ushauri wa Zitto Kabwe, tuunde tume ya usuluhishi, ukweli na mariadhiano ili taifa liangalie maendeleo na si mashindano ya matajiri wachache.
 
hivi mtu kama Rostam anakuwa na ujasiri gani wa kuongea yale aliyoongea?? ila pia hii ni dalili kubwa ya unafiki wa siasa zetu...watu hawataki kuonyesha true color zao...ingekuwa ile misimamo ya Mh.Pinda ndio inareflect misimamo ya serikali tungekuwa mbali sana..ila nazani system inamuelemea, nakama ingekuwa msimamo wangu huyu ndio kiongozi tunayemtaka kwa wakati huu kama jemedali wa nchi..sio chini ya mtu asiye na msimamo...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom