Mtimti
JF-Expert Member
- Feb 23, 2008
- 942
- 647
Wise men never argue with fools
we ndio mpumbafu unaedandia treni kwa mbele..!paka wee
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wise men never argue with fools
we ndio mpumbafu unaedandia treni kwa mbele..!paka wee
wise men never argue with fools
acha uwongo wewe....humjui peter noni.
Jedwali la RA: Nani hayumo? Mzee Mwanakijiji28th April 2009, 06:06 PM![]()
Kuna wimbo mmoja uliimbwa na kwaya ya Bulyankulu Barabara ya 13 uitwao "Samson". Sehemu ya wimbo huo nikikumbuka inasema:
"Tafadhali niambie asili ya nguvu zako, tafadhali niambie waweza kufungwa na nini?" alilalamika mwanamke wa Kifilistina. Sasa, simlinganishi RA na Samson Mnadhiri wa Mungu ila kwenye hili suala la nguvu ambazo inaonekana hazidhibitiki!
Nikiwa nafikiria hilo nikakumbuka mambo ya kuchora majedwali ambamo unaweka makundi ya vitu mbalimbali na ndipo wazo limenijia. Yawezekana ili kuweza kuelewa nguvu za RA ni lazima tuchore jedwali moja hivi na kujaribu kuweka ndani yake watu ambao wanahusiana au wamehusiana moja kwa moja na RA na sasa watu hao wako madarakani au kwenye nafasi fulani za maamuzi.
a. Wale aliowafadhili na kuwasaidia kushika au kudumisha nafasi za kisiasa.
Kundi hili litakuwa na wale wote ambao aliwasaidia wakati wa kampeni au kuwafadhili na kuwasaidia kushika nafasi za kisiasa. Wabunge, Wagombea wa Urais n.k Yaani hapa ni jumla ya wanasiasa ambao wamepata ufadhili kwa RA.
MATOKEO:
1. Jakaya M. Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2.Benno Malisa - (a) - Makamu Mwenyekiti- TAIFA, UVCCM
3.Sofia Simba - (a) - Mwenyekiti Taifa- UWT(CCM)
4. Prof. Juma Kapuya - Waziri wa Kazi & Maendeleo ya Vijana (Mbunge Urambo Magharibi)
5. Adam Malima - (a) - Naibu Waziri, NISHATI NA MADINI (Mbunge, Mkuranga)
6. Emmanuel Nchimbi, alikuwa Mwenyekiti wa Vijana, sasa Naibu Waziri Ulinzi
7. Dr. Peter Kafumu, aliacha kugombea Ubunge Igunga kumpisha Rostam, sasa Kamishna wa Madini
8.
9. Abdulaziz - RC.
10. Lukuvi - RC.
11.J Mongella - DC.
12. Membe - Ubunge, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje
13.Mzindakaya - Ubunge.
14.Nyami - Ubunge.
15.Sita - Ubunge & U-spika.
16.Mahanga - Ubunge.
17. Guninita - CCM Mkoa.
14. Kamala - Ubunge.
15. Marmo - Ubunge.
16. PETER SELUKAMBA (a) Mbunge Kigoma Mjini
17. SIRAJU KABOYONGA (a) Mbunge Tabora Mjini
18. John Mwakipesile--RC Mbeya--[a]
19. Yusuf Makamba--Mbunge na Katibu Mkuu CCM [a]
b. Wale ambao wamewahi kuwa watumishi wake kwenye Vodacom.
Akiwa ni mmoja wa wenye hisa kubwa pale Vodacom (ingawa nasikia alikuwa na mpango wa kuuza hisa hizo) kuna watu ambao wamewahi kufanya kazi Vodacom au kupewa mkataba wa kazi Vodacom. Watu hao wengine wameenda na kuwa na nafasi za kisiasa (yawezewa kuwa kwenye "a" hapo juu). Kama mtu anatokea kwenye "a" na anatokea kwenye "b" basi wawekwe vile vile.
MATOKEO:
1.Pius Msekwa - Vodacom B. - Makamu wa Mwenyekiti CCM (Bara)
2. William Ngeleja - Vodacom - Waziri wa Nishati na Madini
3. Dr. Idris Rashid (Vodacom) - Mkurugenzi Mtendaji Tanesco
c. Wale ambao wametumika kwenye vyombo vyake vya habari
Hawa ni wale ambao kwa namna moja au nyingine wamewahi kuwa na ubia pamoja au utumishi wa vyombo hivyo vya habari na sasa hivi wako kwenye nafasi fulani fulani za kisiasa au za kiserikali. Hapa ninawaondoa watumishi ambao wanafanya kazi tu kwenye vyombo vyake vya habari. Msisitizo ni wale waliovuka toka kwenye vyombo vya habari kwenda kwenye serikali au siasa.
MATOKEO
- Badra Masoud, Afisa Mawasiliano Tanesco, alikuwa Mhariri HCL
- Salva Rweyemamu, Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu, alikuwa Mhariri HCL
-
d. Wale wenye ushirikiano wa kibiashara.
Kundi jingine ni la wale ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa na mahusiano ya kibiashara na RA au makampuni yake mengine na hawa nao wametoka huko na sasa wana nafasi serikalini (idara, wizara au wakala mbalimbali). Na nafasi zao kwenye idara hizo.
Jinsi ya kufanya:
Bila kuweka maelezo mengi, linatajwa
Jina (Salva Rweyemamu);
kundi lake (c)
na nafasi yake ya sasa (Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais).
Nitaendelea kuupdate tunayoyapata labda tunaweza kuona pattern ya aina fulani hivi ikijitokeza. Ukiweza kuweka na some kind of the story behind ya chaguo lako that will help too to make sense.
Baada ya hapo tutachora majedwali ya watu wengine wawili halafu tutaona hiyo picha inayotokea inatuonesha nini. Yawezekana kuna kitu ambacho tumekimiss kwa muda mrefu juu ya RA na nadharia niliyonayo yaweza kuthibitika kisayansi juu ya "asili ya nguvu yake".
Kama huna lolote unalojua; sit down and enjoy!
Nakwambia hivi, namfahamu Noni ile mbaya!!!! Ni wewe tu sikufahamu hapa!!!! Ni mwizi na nikuambie hivi....kuna kipindi walitofautiana na Balali katika Bingo la EPA, na Balali alichofanya ili kumkomoa ni kumchomoa katika directorate Noni aliyokuwa anaongoza na kumweka bench kama director asiye na kitengo maalumu (nafikiri walikuwa 6 ambao Balali aliwaweka Bench). Unataka zaidi ya Noni??? Mengine ni private and dirty mno hayafai katika mjadala huu. For more detail calll me through mya mobile!!!!! Ha ha ha ha ha!!! Take it it easy. Inaelekea wewe ni ndugu yake au ni una ubia katika mipango yake!!!
Kwa mtu anayemfahamu Peter Noni, atashangaa kama utamtetea kuwa si fisadi!!! He is fisadi, angalao kama si papa basi ni nyangumi!!!!
majibu
kukopa sio dhambi, na wala kampuni kufilisika sio dhambi
RA jana amethibitisha kwamba mengi hela zake ni mikopo benki na hii ndio njia kuu inayotumiwa na wafanyabiashara wote duniani
je source ya hela za RA ni hipi?
au huu ni utajiri wa Peter Noni?
je RA anauhusiano gani na Peter Noni?
we ndio mpumbafu unaedandia treni kwa mbele..!paka wee
Hakuna sababu ya hasira wakuu wakati ufisadi wa fisadi papa unafahamika wazi, tusitoane kwenye mada jamani hebu kuleni elimu ya bure kidogo hapa:-
Hiyo jeuri unaitoa wapi ndugu? We ndo Peter Noni? Kama we siye Noni, kwa nini unapanic hivi?
Kama siyo Noni, basi nakushauri ukae kimya tu, wenye data watakupa...vinginevy huwezi kuusemea moyo wa mwingine!
mwaka gani noni alikuwa director asiye na kitengo maalum?kama alikuwa kwenye deal moja na balali kwa nini mpaka leo yupo uraiani wakati wafanyakazi wengine wa BOT wana kesi?huna haja ya kumwonea huruma fisadi,kama noni ni fisadi we mlime tu.!sina haja ya kukupigia wakati najua nje ndani kuhusu NONI
Ni wangapi wameiba pesa na EPA na ushahidi upo lakin iwapo uraiani??? RA ni mojawapo!!! Noni ni mmojawapo. Na wengine wengi!!!!Kwani yale makampuni yote yaliyochota pesa za epa wana kesi??? Fikiri kwanza kabla ya kuandika!!! I am well connected with a number of issues, icluding sensitive ones!!!!!!!!
Hiyo credit hastaili. sema wananchi wameamuka wanakaba mpaka penati. JK anatuyeyusha tu hana lolote
Majibu:
1. Chanzo cha pesa za Rostam= Biashara ya utumwa waliofanya babu zake, ujangili (Meno ya Tembo), Kagoda (EPA), Richmond, Dowands Caspian Constructions, NHC (haijasajiliwa BRELA)
2. Uhusiano wa RA na Peter Noni= RA na Peter Noni walikuwa na share (35 %) Vodacom wameziuza kwa pamoja kwa kampuni iitwayo Mirambo (hatujui mmiliki wake amabaye naye ameomba kibali kwa TCRA aziuze kwa mwekezaji wa nje kitu ambacho hakikubaliki kisheria kwani sheria hairuhusu kampuni kumilikiwa 100 % na wageni)???????? Na pia walishirikiana vizuri kuiba pesa BoT za EPA ndo maana Peter Noni bado ni mkurungezi pale BoT
kumbe unaongelea hisia?..nakuomba tusiivuruge hii thread,kafungue thread kuhusu noni kisha useme hilo kampuni alilofungua noni kuchota mamilioni ya EPA..tutakutana huko,hapa sio mahala pake!