Wanasheria wa Reginald Mengi wakutana na waandishi wa habari na Kumjibu Rostam Aziz

Wanasheria wa Reginald Mengi wakutana na waandishi wa habari na Kumjibu Rostam Aziz

Status
Not open for further replies.
Wana-JF naomba nijibiwe: Inakuwaje mtu (mfanyabiashara?) anaishi hapa nchini, anakuwa tajiri mkubwa (bilionea kwa level ya Bongo) lakini hana hata kampuni moja au biashara? Kuna nini hapo jamani?

Kwa nini wengine hawafanyi hivyo? Yeye tu RA ndiye anajulikana kufanya namna hiyo! Hivi TRA, BRELA, na mamlaka zingine husika hazioni kama hili halikai sawsawa?

Kufuatana na press conference yake ya jana, RA hana hata kampuni moja ya kwake -- ambako kuna jina lake Rostam AbdulRasul Aziz -- hana. Caspian hakuna jina lake, Afritainer hakuna jina lake. Kagoda hakuna jina lake, Richmond hakuna jina lake, New Habari hakuna jina lake! Anafanya nini hapa shughuli inayomfanya kuwa bilionea?

Jana alipoonyeshwa kwamba New habari ilichapisha na kusambaza matoleo mawili ya Rai Alhamisi iliyopita -- yote yenye namba 814 -- aliruka akasema hajui chochote. Magazeti hayo moja lilikuwa linamkandia Mwakyembe, na jingine Reginald mengi -- wote hao mahasimu wake. Anakataa hajui kitu chochote!!!

Watanzania, tusikurupuke kusemasema mabo yasiyo na msingi, hili suala la kuwa na bilionea asiye na biashara yoyote inashtua -- inawezekana labda ni kinara wa unga.
 
wise men never argue with fools

umaskini wako usikufanye kuja ktk jukwaa hili na kuanza kutuambia kila tajiri mzalendo ni fisadi,unaposema noni ni fisadi unatakiwa kutuambia huo ufisadi kaufanya wapi na wapi,sio kupayuka tu,kwani kuwa na share kubwa kwenye kampuni ni kosa?tueleze ufisadi wa noni
 
MmmH!Jina la Rostam Aziz limesumbua sana, limetajwa sana!Huyu jamaa ana nini Hasa, je tuhuma zote hizo ni visingizio?Time will tell and evil shall never triumph over righteuosness!
 
acha uwongo wewe....humjui peter noni.

Nakwambia hivi, namfahamu Noni ile mbaya!!!! Ni wewe tu sikufahamu hapa!!!! Ni mwizi na nikuambie hivi....kuna kipindi walitofautiana na Balali katika Bingo la EPA, na Balali alichofanya ili kumkomoa ni kumchomoa katika directorate Noni aliyokuwa anaongoza na kumweka bench kama director asiye na kitengo maalumu (nafikiri walikuwa 6 ambao Balali aliwaweka Bench). Unataka zaidi ya Noni??? Mengine ni private and dirty mno hayafai katika mjadala huu. For more detail calll me through mya mobile!!!!! Ha ha ha ha ha!!! Take it it easy. Inaelekea wewe ni ndugu yake au ni una ubia katika mipango yake!!!

Kwa mtu anayemfahamu Peter Noni, atashangaa kama utamtetea kuwa si fisadi!!! He is fisadi, angalao kama si papa basi ni nyangumi!!!!
 
Hakuna sababu ya hasira wakuu wakati ufisadi wa fisadi papa unafahamika wazi, tusitoane kwenye mada jamani hebu kuleni elimu ya bure kidogo hapa:-

Jedwali la RA: Nani hayumo? Mzee Mwanakijiji
user_offline.gif
28th April 2009, 06:06 PM

Kuna wimbo mmoja uliimbwa na kwaya ya Bulyankulu Barabara ya 13 uitwao "Samson". Sehemu ya wimbo huo nikikumbuka inasema:

"Tafadhali niambie asili ya nguvu zako, tafadhali niambie waweza kufungwa na nini?" alilalamika mwanamke wa Kifilistina. Sasa, simlinganishi RA na Samson Mnadhiri wa Mungu ila kwenye hili suala la nguvu ambazo inaonekana hazidhibitiki!

Nikiwa nafikiria hilo nikakumbuka mambo ya kuchora majedwali ambamo unaweka makundi ya vitu mbalimbali na ndipo wazo limenijia. Yawezekana ili kuweza kuelewa nguvu za RA ni lazima tuchore jedwali moja hivi na kujaribu kuweka ndani yake watu ambao wanahusiana au wamehusiana moja kwa moja na RA na sasa watu hao wako madarakani au kwenye nafasi fulani za maamuzi.

a. Wale aliowafadhili na kuwasaidia kushika au kudumisha nafasi za kisiasa.

Kundi hili litakuwa na wale wote ambao aliwasaidia wakati wa kampeni au kuwafadhili na kuwasaidia kushika nafasi za kisiasa. Wabunge, Wagombea wa Urais n.k Yaani hapa ni jumla ya wanasiasa ambao wamepata ufadhili kwa RA.

MATOKEO:
1. Jakaya M. Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2.Benno Malisa - (a) - Makamu Mwenyekiti- TAIFA, UVCCM
3.Sofia Simba - (a) - Mwenyekiti Taifa- UWT(CCM)
4. Prof. Juma Kapuya - Waziri wa Kazi & Maendeleo ya Vijana (Mbunge Urambo Magharibi)
5. Adam Malima - (a) - Naibu Waziri, NISHATI NA MADINI (Mbunge, Mkuranga)
6. Emmanuel Nchimbi, alikuwa Mwenyekiti wa Vijana, sasa Naibu Waziri Ulinzi
7. Dr. Peter Kafumu, aliacha kugombea Ubunge Igunga kumpisha Rostam, sasa Kamishna wa Madini
8.
9. Abdulaziz - RC.
10. Lukuvi - RC.
11.J Mongella - DC.
12. Membe - Ubunge, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje
13.Mzindakaya - Ubunge.
14.Nyami - Ubunge.
15.Sita - Ubunge & U-spika.
16.Mahanga - Ubunge.
17. Guninita - CCM Mkoa.
14. Kamala - Ubunge.
15. Marmo - Ubunge.
16. PETER SELUKAMBA (a) Mbunge Kigoma Mjini
17. SIRAJU KABOYONGA (a) Mbunge Tabora Mjini
18. John Mwakipesile--RC Mbeya--[a]
19. Yusuf Makamba--Mbunge na Katibu Mkuu CCM [a]

b. Wale ambao wamewahi kuwa watumishi wake kwenye Vodacom.
Akiwa ni mmoja wa wenye hisa kubwa pale Vodacom (ingawa nasikia alikuwa na mpango wa kuuza hisa hizo) kuna watu ambao wamewahi kufanya kazi Vodacom au kupewa mkataba wa kazi Vodacom. Watu hao wengine wameenda na kuwa na nafasi za kisiasa (yawezewa kuwa kwenye "a" hapo juu). Kama mtu anatokea kwenye "a" na anatokea kwenye "b" basi wawekwe vile vile.

MATOKEO:
1.Pius Msekwa - Vodacom B. - Makamu wa Mwenyekiti CCM (Bara)
2. William Ngeleja - Vodacom - Waziri wa Nishati na Madini
3. Dr. Idris Rashid (Vodacom) - Mkurugenzi Mtendaji Tanesco

c. Wale ambao wametumika kwenye vyombo vyake vya habari
Hawa ni wale ambao kwa namna moja au nyingine wamewahi kuwa na ubia pamoja au utumishi wa vyombo hivyo vya habari na sasa hivi wako kwenye nafasi fulani fulani za kisiasa au za kiserikali. Hapa ninawaondoa watumishi ambao wanafanya kazi tu kwenye vyombo vyake vya habari. Msisitizo ni wale waliovuka toka kwenye vyombo vya habari kwenda kwenye serikali au siasa.

MATOKEO

- Badra Masoud, Afisa Mawasiliano Tanesco, alikuwa Mhariri HCL
- Salva Rweyemamu, Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu, alikuwa Mhariri HCL
-

d. Wale wenye ushirikiano wa kibiashara.
Kundi jingine ni la wale ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa na mahusiano ya kibiashara na RA au makampuni yake mengine na hawa nao wametoka huko na sasa wana nafasi serikalini (idara, wizara au wakala mbalimbali). Na nafasi zao kwenye idara hizo.

Jinsi ya kufanya:
Bila kuweka maelezo mengi, linatajwa
Jina (Salva Rweyemamu);
kundi lake (c)
na nafasi yake ya sasa (Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais).

Nitaendelea kuupdate tunayoyapata labda tunaweza kuona pattern ya aina fulani hivi ikijitokeza. Ukiweza kuweka na some kind of the story behind ya chaguo lako that will help too to make sense.

Baada ya hapo tutachora majedwali ya watu wengine wawili halafu tutaona hiyo picha inayotokea inatuonesha nini. Yawezekana kuna kitu ambacho tumekimiss kwa muda mrefu juu ya RA na nadharia niliyonayo yaweza kuthibitika kisayansi juu ya "asili ya nguvu yake".

Kama huna lolote unalojua; sit down and enjoy!
 
Nakwambia hivi, namfahamu Noni ile mbaya!!!! Ni wewe tu sikufahamu hapa!!!! Ni mwizi na nikuambie hivi....kuna kipindi walitofautiana na Balali katika Bingo la EPA, na Balali alichofanya ili kumkomoa ni kumchomoa katika directorate Noni aliyokuwa anaongoza na kumweka bench kama director asiye na kitengo maalumu (nafikiri walikuwa 6 ambao Balali aliwaweka Bench). Unataka zaidi ya Noni??? Mengine ni private and dirty mno hayafai katika mjadala huu. For more detail calll me through mya mobile!!!!! Ha ha ha ha ha!!! Take it it easy. Inaelekea wewe ni ndugu yake au ni una ubia katika mipango yake!!!

Kwa mtu anayemfahamu Peter Noni, atashangaa kama utamtetea kuwa si fisadi!!! He is fisadi, angalao kama si papa basi ni nyangumi!!!!

mwaka gani noni alikuwa director asiye na kitengo maalum?kama alikuwa kwenye deal moja na balali kwa nini mpaka leo yupo uraiani wakati wafanyakazi wengine wa BOT wana kesi?huna haja ya kumwonea huruma fisadi,kama noni ni fisadi we mlime tu.!sina haja ya kukupigia wakati najua nje ndani kuhusu NONI
 
majibu

kukopa sio dhambi, na wala kampuni kufilisika sio dhambi
RA jana amethibitisha kwamba mengi hela zake ni mikopo benki na hii ndio njia kuu inayotumiwa na wafanyabiashara wote duniani

je source ya hela za RA ni hipi?
au huu ni utajiri wa Peter Noni?
je RA anauhusiano gani na Peter Noni?

Majibu:
1. Chanzo cha pesa za Rostam= Biashara ya utumwa waliofanya babu zake, ujangili (Meno ya Tembo), Kagoda (EPA), Richmond, Dowands Caspian Constructions, NHC (haijasajiliwa BRELA)

2. Uhusiano wa RA na Peter Noni= RA na Peter Noni walikuwa na share (35 %) Vodacom wameziuza kwa pamoja kwa kampuni iitwayo Mirambo (hatujui mmiliki wake ambaye naye ameomba kibali kwa TCRA aziuze kwa mwekezaji wa nje kitu ambacho hakikubaliki kisheria kwani sheria hairuhusu kampuni kumilikiwa 100 % na wageni)???????? Na pia walishirikiana vizuri kuiba pesa BoT za EPA ndo maana Peter Noni bado ni mkurungezi pale BoT
 
Last edited:
we ndio mpumbafu unaedandia treni kwa mbele..!paka wee

Hiyo jeuri unaitoa wapi ndugu? We ndo Peter Noni? Kama we siye Noni, kwa nini unapanic hivi?

Kama siyo Noni, basi nakushauri ukae kimya tu, wenye data watakupa...vinginevy huwezi kuusemea moyo wa mwingine!
 
Hakuna sababu ya hasira wakuu wakati ufisadi wa fisadi papa unafahamika wazi, tusitoane kwenye mada jamani hebu kuleni elimu ya bure kidogo hapa:-

Mkuu wangu FM ES, umekuna penyewe haswa, hebu wape live na huyo Kafumu wa Madini ni kuwa aliahidiwa kabisa kuwa amwachie jamaa na atahakikisha anapata kitu kizuri.

Huyo Benno Malisa tena alikuwa anajidai waziwazi kabisa kuwa atapata uenyekiti na RA alimpa mil. 20 kwa ajili ya kampeni na nyongeza kukingana na mahitaji ya kampeni yalivyokuwa yanahitajika.

Badra yuko kwenye chain ya viongozi wengi sana. I am happy she decided to remain single kwa kipindi nilichokuwa namfahamu, sijui kwa sasa maana hakuna mume ataweza vumilia zali la huyu bibie!!!!!! Ni hatari!!!!!!

Yaani 70% hapo nina wasifu wao!!!!! Ila tu Sitta mwondoe katika list ya mwakani!!!! RA hataki hata kumuona sasa, na ametangaza kumwangusha kabisa kiti cha ubunge!!!!!! Ni mpango mkakati huo, hivyo vijana wa SITTA wa campaigh muwe makini sana, kuna mchezo mchafu sana RA na Mafisadi wanataka kuucheza dhidi ya SITTA. I love him, if not liking him!!!
 
"Wana-JF naomba nijibiwe: Inakuwaje mtu (mfanyabiashara?) anaishi hapa nchini, anakuwa tajiri mkubwa (bilionea kwa level ya Bongo) lakini hana hata kampuni moja au biashara? Kuna nini hapo jamani?

Kwa nini wengine hawafanyi hivyo? Yeye tu RA ndiye anajulikana kufanya namna hiyo! Hivi TRA, BRELA, na mamlaka zingine husika hazioni kama hili halikai sawsawa?

Kufuatana na press conference yake ya jana, RA hana hata kampuni moja ya kwake -- ambako kuna jina lake Rostam AbdulRasul Aziz -- hana. Caspian hakuna jina lake, Afritainer hakuna jina lake. Kagoda hakuna jina lake, Richmond hakuna jina lake, New Habari hakuna jina lake! Anafanya nini hapa shughuli inayomfanya kuwa bilionea?

Jana alipoonyeshwa kwamba New habari ilichapisha na kusambaza matoleo mawili ya Rai Alhamisi iliyopita -- yote yenye namba 814 -- aliruka akasema hajui chochote. Magazeti hayo moja lilikuwa linamkandia Mwakyembe, na jingine Reginald mengi -- wote hao mahasimu wake. Anakataa hajui kitu chochote!!!

Watanzania, tusikurupuke kusemasema mabo yasiyo na msingi, hili suala la kuwa na bilionea asiye na biashara yoyote inashtua -- inawezekana labda ni kinara wa unga."

_________________________________

Zak:

Mimi nakubaliana nawe kwamba hii ya kuwa bilionea bila shughuli/kampuni/biashara yoyote haikai barabara -- ni namna ya kutaka kufanya hujuma. RA angekuwa msafi kama vile anataka watu wamuamini, basi angekuwa muwazi zaidi katika shughuli zake.

Halafu inasemekana hata hizo kampuni ambazo inasemekana ni zake -- Caspian, New Habari etc -- baadhi yake majina ya wanaoonekana wamiliki ni feki. maana yake ni kwamba ikifanyika hujuma/wizi au jinai nyingine katika kampuni hizo hakuna wa kukamata!
 
Hiyo jeuri unaitoa wapi ndugu? We ndo Peter Noni? Kama we siye Noni, kwa nini unapanic hivi?

Kama siyo Noni, basi nakushauri ukae kimya tu, wenye data watakupa...vinginevy huwezi kuusemea moyo wa mwingine!

hakuna jeuri wala kupanic,unapoweka tuhuma basi lazima uzithibitishe sio kutype tu kwa sababu flani kasema..hakuna mtu aliepanic..
 
mwaka gani noni alikuwa director asiye na kitengo maalum?kama alikuwa kwenye deal moja na balali kwa nini mpaka leo yupo uraiani wakati wafanyakazi wengine wa BOT wana kesi?huna haja ya kumwonea huruma fisadi,kama noni ni fisadi we mlime tu.!sina haja ya kukupigia wakati najua nje ndani kuhusu NONI

Ni wangapi wameiba pesa na EPA na ushahidi upo lakin iwapo uraiani??? RA ni mojawapo!!! Noni ni mmojawapo. Na wengine wengi!!!!Kwani yale makampuni yote yaliyochota pesa za epa wana kesi??? Fikiri kwanza kabla ya kuandika!!! I am well connected with a number of issues, icluding sensitive ones!!!!!!!!
 
kumbe unaongelea hisia?..nakuomba tusiivuruge hii thread,kafungue thread kuhusu noni kisha useme hilo kampuni alilofungua noni kuchota mamilioni ya EPA..tutakutana huko,hapa sio mahala pake!
 
Jamani mnataka Rais azungumzie nini juu ya hayo malumbano? hata shule kuna kaka wa zamu/kiranja mkuu, mwalimu wa zamu/malezi, second master sasa kila tukio lazima head master aje azoze?
Sidhani kama Tz itaenda kubaya kwa ajili ya hayo malumbano ila ndio nafasi ya wa-TZ kujua kilichokuwa kinapikwa hasa huko jikoni,wengi wetu tulikuwa tunaona kinachokuja mezani tu...sasa mnataka JK akafunge mrango wa kitchen ili tusiende chungulia?
Acha wa endelee kusasambuana, at the end of the day tutajua ubwabwa ni upi na ukoko ni upi.... Ndani ya haya majungu na marungu tutapa facts au a new lead...hata Richmond, IPTL zilianza kama uvumi....
 
Hiyo credit hastaili. sema wananchi wameamuka wanakaba mpaka penati. JK anatuyeyusha tu hana lolote

Wananchi na Media ndio wameamua kuwakaba mafisadi. Mkulu hajawafanya chochote, ndio maana badala ya kujibu hoja specifically kuhusu tuhuma za Richmond/Dowans, EPA ya BoT, Radar, NSSF & PSPF, Kagoda, Ndege ya Rais etc mafisaid hao wanajaribu kujificha kwenye kichaka kichovu kwa kusingizia kuwa eti kuwataja ni ubaguzi.

Kama alivyosema Baba wa Taifa (RIP), kuhusu makaburu wa South Africa, hatuwachukii mafisadi hao kutokana na rangi zao, bali kutokana na matendo yao ya kutunyonya kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wakubwa, ambao wamethubutu kuwatetea mafisadi papa hao.

Pia vyombo vya habari vya UMMA vinawatetea! Kweli wamewashika viongozi wetu.

Kazi ipo mazee.

Can't wait for the Court proceedings to start!
 
Majibu:
1. Chanzo cha pesa za Rostam= Biashara ya utumwa waliofanya babu zake, ujangili (Meno ya Tembo), Kagoda (EPA), Richmond, Dowands Caspian Constructions, NHC (haijasajiliwa BRELA)

2. Uhusiano wa RA na Peter Noni= RA na Peter Noni walikuwa na share (35 %) Vodacom wameziuza kwa pamoja kwa kampuni iitwayo Mirambo (hatujui mmiliki wake amabaye naye ameomba kibali kwa TCRA aziuze kwa mwekezaji wa nje kitu ambacho hakikubaliki kisheria kwani sheria hairuhusu kampuni kumilikiwa 100 % na wageni)???????? Na pia walishirikiana vizuri kuiba pesa BoT za EPA ndo maana Peter Noni bado ni mkurungezi pale BoT

Excellently said, rmashauri. I believe mtimti atasoma hii na atajua kwa nini nasimama kidete kusema kuwa NONI ni fisadi. Ziko evidence nyingi sana na si za share 35% za vodacom tu. Kwani Rostam atakubali NONI aende afunguliwe kesi, wakati wa utetezi si atamtaja?? Kwani unafikiri kwa nini Malegesi naye hajapelekwa mahakamani??? Utetezi ake ni tata!!!! Again, mtimti si wote mafisadi watapelekwa mahakamani, watapelekwa tu wale ambao hawana close tie na ssm = Rostam Aziz!!!!
 
Mengi na Rostam wanaexpose tuu ujinga wao hapa . Trust me we are not going to benefit anything from the ongoing debate. Mengi has the burden of proof , he was the one who raised this issue . If Mheshimiwa will fail to substantiate his claim then he will liable of defaming one's character.
 
kumbe unaongelea hisia?..nakuomba tusiivuruge hii thread,kafungue thread kuhusu noni kisha useme hilo kampuni alilofungua noni kuchota mamilioni ya EPA..tutakutana huko,hapa sio mahala pake!

Mtimti tuliza boli ndugu yangu inawezekana una mapenzi mema na Noni lakini yumkini humfahamu vizuri. Chukulia mfano huu; Peter Noni ni mmilikiwa kampuni ya Planetel ambayo ni super dealer wa Vodacom na ilikuwa inamiliki share 16 % za Vodacom na sasa ameziuza na hatujui ni kwa nini. Sasa jiulize Peter Noni alifanya biashara gani ya kupata mabilioni ya kumiliki 16 % ya VodaCom. Huu ni mfano mdogo ninaoujua. Acha kutukana calm down rafiki yangu.
 
Last edited:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom