Wanasheria wa Reginald Mengi wakutana na waandishi wa habari na Kumjibu Rostam Aziz

Wanasheria wa Reginald Mengi wakutana na waandishi wa habari na Kumjibu Rostam Aziz

Status
Not open for further replies.
so Mengi hakufika Mkutanoni..kawatuma wanasheria sio....as per michuzi blog? akina Lunyungu waliosema wao wataiwakilisha JF hadi sasa hawajasema lolote...
 
so Mengi hakufika Mkutanoni..kawatuma wanasheria sio....as per michuzi blog? akina Lunyungu waliosema wao wataiwakilisha JF hadi sasa hawajasema lolote...

Inaonyesha hivyo, lakini nilicho kifurahia ni kumtaka aseme hizo hao watu alfu 6000 na kodo anazo jidai analipa ni wapi na kwa kampuni ipi? Hapo ndo patamu, kwani kutoweka jina lako kwenye kampuni ukaghushi na kuweka majina hewa ya kina KYOMUHENDO huo sio ufisadi? huyu Fisadi papa this time kakamatika!
 
nilitegemea nikute vijembe, kuwa je Mengi mbona hajajibu tuhuma???? lakini wapi, katunywesha maji yasiyo, kaua UNICO n.k nikajiuliza huyu kaamua kupambana au kuna jambo, kumbe biashara LOL
 
Inaonyesha hivyo, lakini nilicho kifurahia ni kumtaka aseme hizo hao watu alfu 6000 na kodo anazo jidai analipa ni wapi na kwa kampuni ipi? Hapo ndo patamu, kwani kutoweka jina lako kwenye kampuni ukaghushi na kuweka majina hewa ya kina KYOMUHENDO huo sio ufisadi? huyu Fisadi papa this time kakamatika!
.

Mkuu huu ufisad wa kutumia majina yasiyo, ya wajomba, wadogo n.k hauko kwa RA tu, nawafahamu maprofessor wengi wana-own daladala kwa majina ya ndugu zao.

Swali ni je, tuna sheria katika nchi yetu ya kuzuia hali hiyo?? maana tukisema ni fisad kwa sababu hii naona haiji, wengi wamo humu. Yeye ni fisadi kwa sababu ameiba fedha za umma na sio anatumia majina yasiyo!
 
"Alisema miaka ya 1800 babu zake waliuza watumwa wakapata fedha nyingi, halafu yeye aliiba EPA na akasema anao kina Sophia Simba, Mkuchika nk serkalini wanomtuma wapi achukue fedha ndio maana alisema alinunua HBC hakwenda hata kuona nini alinunua mpaka kama wiki mbili alipopata habari hakuna anayejua huko kukoje.Huyu ndiye RA aliyewahi kuwa mweka hazina wa CCM kwenda kurekebisha vitabu vya deep green, kagoda, tanggold na meremeta. hili ndio chimbuko la utajiri wake awe na kampuni la nini.|

________________________________

Kinepi-nepi:

Umenena ndugu yangu. Ni kama wiki mbili au tatu hivi ndiyo inasemekana "wafanya kazi wake" walimuona anatinga hapo Sinza Shekilango kuona alichonunua.

Isitoshe, Septemba mwaka jana ilipokuwa inafanyika re-launching ya magazeti ya New Habari pale Kempinski RA alikuwapo, lakini hakutambulishwa kama Mwenye kampuni, bali ni kama Mbunge wa Igunga. Katika hafla hiyo alimtumia mzee mmoja wa CCM, Peter Kisumo (bila shaka kwa malipo) na kumtambulisha kuwa yeye ndiye Mwenyekiti wa New habari -- kwa mshangao wa wanahabari wengi wa kampuni hiyo waliyokuwapo.

Swali: Anajifificha-ficha kwa sababu gani? Leo hii New habari ikikumbwa na jambo kubwa, hujuma, kukwepa kodi nk ataruiruka maili mia kuwa siyo kampuni yake! na badala yake mamlaka husika itakuwa inapiga danadana kuchukua hatua kwa mhusika.
 
...mkutano wa mengi leo unatakiwa kuzuiwa na vyombo vya usalama ..kwa kuwa unaaingiza nchi kwenye malumbano yasiyoisha .....muda wa mengi kuanza kusumbuliwa na dola wazi umefika ..uvumilivu wao umefika kikomo...

sio mengi tu hata rostam hatakiwi kuzungumza tena....wote wameongea sasa waachie polisi na mahakama zifanye kazi...wasigawe wananchi..

katika taratibu za kawaida za usalama ndio hivyo...sasa ndio tutajuwa kama kweli rais ameapa kulinda usalama wa wananchi au la...hatuwezi kuwa na taifa la kiumbea umbea wa kusutana kama wake wenza ...miaka mitano yote tumekalia kusutana tu hakuna kinachofanyika .... we are tied with this weak gorvernment....watuache tufanye kazi!!

Philemon wewe uko kundi gani, papa au nyangumi? Kwa nini unataka mkutano wa mengi uzuiwe na polisi? Kwa taarifa yako mkutano umeshamalizika na nenda michuzi ukapate maswali magumu toka kwa Ngalo and Advocates kwenda kwa Rostam.
 
Kwa wale waliosoma ile miaka ya juzi kuna ile hadithi iliyoishia HERI MIMI SIJASEMA na huyo aliyesema heri mimi sijasema ndio akawa wa mwisho kuuliwa.
Anayeikumbuka aipangilie ile story.

Hii sakata itachukua wengi kama ile story.
Yetu macho na masikio
 
.

Mkuu huu ufisad wa kutumia majina yasiyo, ya wajomba, wadogo n.k hauko kwa RA tu, nawafahamu maprofessor wengi wana-own daladala kwa majina ya ndugu zao.

Swali ni je, tuna sheria katika nchi yetu ya kuzuia hali hiyo?? maana tukisema ni fisad kwa sababu hii naona haiji, wengi wamo humu. Yeye ni fisadi kwa sababu ameiba fedha za umma na sio anatumia majina yasiyo!

Ni kweli kaiba fedha za uma, lakini pia ni ufisadi wa aina yake kutoweka majina yake ili so likiibuka aruke kimanga! Si unamuona anavo kuja kifua mbele kudai hawajui kagoda na Dowans akidai nenda Brela kama kuna jina langu? Sasa kama siyo ufisadi ninini?

Na anafanyahivo kwa makusudi akijua hizo biashara zake ni wizi mtupu!

Ila anaposahau ni kwamba Watanzania wamechoka, na wameamua kutoa ushirikiano wa ushahidi wote, kuanzia yeye anavo husika na usimamizi wa hayo makampuni hadi anapochukua/kuyakopea pesa! so he has to face it ushahidi umejaa tele, hadi yule wakili (smebody laizer/weiser? sorry sikumbuki vyema jina) Kaisha sema hadharani alivo msainisha hizo pesa za EPA, sasa?

Huyu Fisadi papa Rostamu anacho jaribu kufanya ni kama mbuni, anadhani akificha kichwa yu salama, Kiluwiluwi chote kipo nje, na hakya nani this time lazima tukishughulikie. Enough is Enough!
 
.
Mkuu huu ufisad wa kutumia majina yasiyo, ya wajomba, wadogo n.k hauko kwa RA tu, nawafahamu maprofessor wengi wana-own daladala kwa majina ya ndugu zao.

Je hii ni sawa na mhindi kutumia majina hewa na anwani hewa kuandikisha kampuni kwa nia ya kuiba ? Je, hao ndugu zao maprofessor wakitenda kosa la kuiba au kuua, wataweza kupatikana ?

.Swali ni je, tuna sheria katika nchi yetu ya kuzuia hali hiyo?? maana tukisema ni fisadi kwa sababu hii naona haiji, wengi wamo humu.

Sheria zipo zinasema kujipatia mali kwa udanganyifu ni kosa na yeyote anayefanya hivyo ni fisadi. Huyu Rostam ameweza kutenda hayo kwa kuwa ama ana ubia na mamlaka husika au ameziweka mfukoni.

.Yeye ni fisad kwa sababu ameiba fedha za umma na sio anatumia majina yasiyo!

Ameiba na ametumia udanganyifu kwa kutoa data za uwongo kuandikisha kampuni hewa akishirikiana na tuliowapa dhamana ya kuendesha nchi - huu ndio hasa ugomvi mkuu. Sasa wenye nchi wanauliza kulikoni ?
CCM, hifadhi na ngome ya wahalifu, lazima ivunjwe !!
 
Kutoka mwananchi

Na Boniface Meena


MALUMBANO kati ya wafanyabiashara maarufu nchini Reginald Mengi na Rostam Aziz, yaliendelea jana kufuatia wanasheria wa Mengi, Michael Ngalo na Agapitus Nguma kujibu baadhi ya hoja zilizotolewa na Rostam juzi huku wakiacha kujibu hoja nyingine na kuongeza maswali kadhaa waliyodai yanahitaji majibu.

Katika mkutano na waandishi wa habari mwanasheria wa Mengi, Michael Ngalo wa Ngalo & Company Advocates alijibu baadhi ya tuhuma hizo kwa niaba ya Mengi na kudai kuwa wako mbioni kumfungulia kesi Rostam Aziz kutokana na tuhuma hizo wanazodai kuwa ni za uongo.

Tuhuma zilizojibiwa na wanasheria hao ni kuhusu fedha za Import Support, kampuni ya Anche Mwedu Limited, utajiri wa Mengi, ukwepaji ulipaji kodi, fedha za misaada na kuwekeza katika biashara, uwekezaji wa kampuni ya NICO kwenye kiwanda cha Interchem Pharma Limited na kuwaita wengine ni wauaji.

Tuhuma ambazo hazikujibiwa na Mengi ambazo zilitolewa na Rostam ni kuhusu kuwa na akaunti ya fedha za kigeni nje ya nchi, malipo kwa wafanyakazi wake, kuhusu kuwa na ugomvi na baadhi ya viongozi na kutaka matatizo hayo yawe ya kitaifa na tuhuma nyinginezo.

Kuhusu fedha za Import Support, Ngalo alisema deni la fedha za import support zimeshalipwa tangu mwaka 2008 hivyo Mengi hana deni kama hilo huku wakionyesha kivuli cha hundi walizolipia deni hilo.

Kuhusu kampuni ya Anche Mwedu Limited alisema suala hilo liliamuliwa mahakamani katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupitia hukumu iliyosomwa Septemba 30 mwaka 2008 na dai la NBC kupitia Consolidated Holding Cooperation kwenye kesi hiyo lilikataliwa na mahakama kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kuthibitisha deni hilo.

Kesi hiyo ya madai nambari 197 ya mwaka 1993 ilifunguliwa na Anche Mwedu Limited dhidi ya Benki Kuu, kampuni za Societe General De Surveilanche S.A, SGS India Private Ltd, Consolidated Holding Corporation, Benki ya NBC na kampuni nyingine ya J.G. Vacuum Flasks Ltd.

Kuhusu ukwepaji kodi wanasheria hao walidai kuwa si Mengi wala kampuni yake yoyote ina tuhuma za kukwepa kulipa kodi.

Kuhusu uwekezaji wa NICO, Ngalo alidai kuwa si Mengi wala kamati ya uwekezaji ya NICO ilihusika kwa namna yoyote ili katika mchakato wa maamuzi ya kuwekeza kwenye kampuni ya Interchem kwa kuwa alipogundua hilo alijiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa kamati ya uwekezaji na ujumbe na alifanya hivyo kupitia barua aliyoiandikia NICO Agosti 3 mwaka 2007. Aliwataka wanahabari kwenda NICO kuthibitisha suala hilo.


Hata hivyo Mengi kupitia mwanasheria wake aitwaye Nguma alimtaka Rostam kujibu maswali manne, la kwanza, likiwa la kutaka kujua anafanya biashara gani nchini na ataje biashara hizo anazoziendesha na pia kama kampuni zake zimesajiliwa BRELA kwa kutumia jina lake.

Pia alimtaka aeleze kama zinalipa kodi, na kuhusu kuwa hana uhusiano na Kagoda aeleze alikuwa akienda benki kujadiliana juu ya akaunti ya Kagoda alikuwa akifanya hivyo kama nani.

Kuhusu Dowans aeleze mipango ya benki kuipatia Dowans fedha za mkopo aliokuwa na aliushughulikia kama nani, na uhusiano na Richmond anawafahamu vipi wahusika wake.


Hatua hiyo ya Mengi kujibu baadhi ya tuhuma, na kutoa maswali hayo imekuja siku mbili baada ya mfanyabiashara Rostam Aziz kumlipua Mengi na kumbatiza jina la "nyangumi wa ufisadi" baada ya Mengi kumwita yeye na wenzake wanne kuwa ni mafisadi papa.

Rostam Aziz, ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara watano waliotuhumiwa na Mengi kuwa mapapa wa ufisadi, alitoa mlolongo wa tuhuma za ufisadi dhidi ya mwenyekiti huyo mtendaji wa makampuni ya IPP, na kueleza kuwa atawasilisha vielelezo kwa vyombo husika ndani ya saa 48 ili Mengi aanze kuchunguzwa.

Mapigo ya Rostam, ambayo yanazidi kupandisha joto la vita hiyo ya maneno, yametokana na tuhuma nzito ambazo Mengi alizitoa Aprili 23 wakati alipotaja wafanyabiashara watano akitaka wadhibitiwe mapema, akiwemo mbunge huyo wa Igunga.
Tofauti na Mengi ambaye hakutoa vielelezo hapo mwanzo wakati anawataja mafisadi papa hao na kusema yuko tayari kupandishwa kizimbani ili ukweli udhihirike, Rostam aliorodhesha tuhuma nyingi na kuahidi kuzikabidhi kwenye vyombo vya serikali ili hatua zichukuliwe.
 
. Kasema wazi tena kwa kujitapa kuwa watanzania 6,000 kawaajiri na anawalipa viruzi - je ni kwenye shughuli gani kama Caspian hakuna jina lake, Afritainer hakuna jina lake, Kagoda hakuna jina lake, Richmond hakuna jina lake, Dowans hakuna jna lake na New Habari hakuna jina lake!

Mengi kalikoroga, Rostam kalinywa !!​

- Nijuavyo ni kwamba Rostam anaajiri wananchi wawili tu kwa jina lake kamili, nao ni secretary wake na dereva wake tu, sasa hawa wananchi 6000 anawaaajiri katika kampuni zipi hizo maana Brela hakuna hata moja yenye jina lake? Sasa unaona hapo palivyo patamu!

Respect.

FMES!
 
Kutoka mwananchi

Na Boniface Meena


1. Tuhuma zilizojibiwa na wanasheria hao ni kuhusu fedha za Import Support, kampuni ya Anche Mwedu Limited, utajiri wa Mengi, ukwepaji ulipaji kodi, fedha za misaada na kuwekeza katika biashara, uwekezaji wa kampuni ya NICO kwenye kiwanda cha Interchem Pharma Limited na kuwaita wengine ni wauaji.

3. Kuhusu fedha za Import Support, Ngalo alisema deni la fedha za import support zimeshalipwa tangu mwaka 2008 hivyo Mengi hana deni kama hilo huku wakionyesha kivuli cha hundi walizolipia deni hilo.

4. Kuhusu kampuni ya Anche Mwedu Limited alisema suala hilo liliamuliwa mahakamani katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupitia hukumu iliyosomwa Septemba 30 mwaka 2008 na dai la NBC kupitia Consolidated Holding Cooperation kwenye kesi hiyo lilikataliwa na mahakama kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kuthibitisha deni hilo.

5. Kesi hiyo ya madai nambari 197 ya mwaka 1993 ilifunguliwa na Anche Mwedu Limited dhidi ya Benki Kuu, kampuni za Societe General De Surveilanche S.A, SGS India Private Ltd, Consolidated Holding Corporation, Benki ya NBC na kampuni nyingine ya J.G. Vacuum Flasks Ltd.

6. Kuhusu ukwepaji kodi wanasheria hao walidai kuwa si Mengi wala kampuni yake yoyote ina tuhuma za kukwepa kulipa kodi.

7. Kuhusu uwekezaji wa NICO, Ngalo alidai kuwa si Mengi wala kamati ya uwekezaji ya NICO ilihusika kwa namna yoyote ili katika mchakato wa maamuzi ya kuwekeza kwenye kampuni ya Interchem kwa kuwa alipogundua hilo alijiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa kamati ya uwekezaji na ujumbe na alifanya hivyo kupitia barua aliyoiandikia NICO Agosti 3 mwaka 2007. Aliwataka wanahabari kwenda NICO kuthibitisha suala hilo.
.

- Haya wakuu tuambieni ni wapi kuna kasoro hapa na haya majibu ya Mengi? Wapi kuna uongo?

FMEs!
 
Watu wengi wajitia hofu na kushindwa kujua wapi tuna kwenda.
Tulizeni boli huu ndo mwanzo wa mwendo kwenda kwenye uelekeo tulo elekea.

Viongozi na Wafanyibiashara kugawana kilicho cha umma ni kosa kubwa kuliko kosa lolote la jinai. Matokeo yake huleta kishindo kikubwa sana, kishindo hicho huweza ambatana na kusambaratika kwa taratibu na kuleta Vita live ya Mabomu na Risasi.

Inawezekana, nasema inawezekana Maninja kadhaa tayari wana mabofu elfu kadhaa mikoni mwao baada ya kuchoma Ghala la Silaha.

Kuna anayejua kulikuwa na Silaha kiasi gani humo ghalani?

kuna ajuaye kulikuwa na Bunduki na Risasi ngapi huko Ghalani?

Najua uchunguzi utasema Chnzo cha mlipuko ni Mshumaa si unajua tena Uchunguzi wa UwanjaWaFisi Yard (Scotland Yard) ya Tanzania? Kila siku hutupa matokeo hafifu?

Unasema chochocte utakacho au utakachoambiwa na Waziri mkuu au Rais.

Baharini avumaye ni Papa, lakini nijuavyo papa wote wana Adabu ya kutosha mbele ya nyangumi, japo mara kadhaa huweza shambulia makinda wa nyangumi kumshambulia nyangumi mwenyewe ni kuifanya bahari igeuke ndogo na kuwa na ujazo wa kikombe cha chai.

Nyangumi na Papa wote wanategemea maji(Watanzania) ili kuishi, maji pia huwategemea nyangumi na papa ili yasigeuke kaburi au dampo la vifavyo baharini.

Maji yaweza kuwepo bila nyangumi na papa, lakini papa na nyangumi kamwe hawezi ishi bila maji( huo ndo mtaji wetu WaTanzania).

Uanzapo ugomvi wa Papa na nyanguni, mwamuzi ni maji( Sisi Watanzania kama hujui jua sasa).

Sasa maji nayo yanaingiapo hofu pamoja na kuwa na karata zote dume wabaki ukijiuliza kulikoni!
Kamwa Sioni tatizo kwenye ugomvi wa Papa na Nyangumi bali tatizo ndani ya mwenye maji.(WaTZ)

Watanzania tulio wengi tuko manyanyasoni siku zote, kitufanyacho tuache kuchukua msimamo ni Matumaini yetu tulo jenga siku nyingi kwamba tukikaa kimya hakika siku inakuja nasi tutafaidi kama Papa na Nyangumi wafaidivyo.

Kwa vile hatuna uhakika tutafaidi kupitia mgongoni mwa Papa au Nyangumi tunaona ni vema kutogusa mishipa ya fahamu ya Mahasibu wawili hawa, kufanya hivyo kunaweza vuruga faidiko la kesho Kifisadi.

Ndoto za kufaidika kifisadi kwa namna moja au nyingine zimo vichwani mwa waTanzania wengi, ndoto hizi ni tatizo kubwa kuliko Ufisadi wenyewe.
Ndoto hizi za kipuuzi kuliko zile za Alinacha ndiyo nyufa akilini mwetu zifanyazo Mafisadi wa aina ya Papa na Nyangumi kupenyeza thumuni zao nduchu huku wakituahidi nyingi zinakuja tuvute subira na kukunja mapepe yetu.

Si afadhari kuuziwa mbuzi ndani ya gunia, mbuzi hutampata lakini unaweza ambulia gunia. Kuliko kuuziwa mbuzi kwa mlio???? Utafaidi nini mlio thamani yake ni thumuni ngapi??
 
Last edited:
Haya wakuu tuambieni ni wapi kuna kasoro hapa na haya majibu ya Mengi? Wapi kuna uongo?

"Kuhusu uwekezaji wa NICO, Ngalo alidai kuwa si Mengi wala kamati ya uwekezaji ya NICO ilihusika kwa namna yoyote ili katika mchakato wa maamuzi ya kuwekeza kwenye kampuni ya Interchem kwa kuwa alipogundua hilo alijiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa kamati ya uwekezaji na ujumbe na alifanya hivyo kupitia barua aliyoiandikia NICO Agosti 3 mwaka 2007. Aliwataka wanahabari kwenda NICO kuthibitisha suala hilo."

Anasema hakuhusika "katika mchakato wa maamuzi ya kuwekeza kwenye kampuni ya Interchem kwa kuwa alipogundua hilo alijiuzulu." Hakuhusika kwa kuwa alipogundua alijiuzulu, maana yake nini, ulikuwepo hukuwepo?

Alipogundua alijiuzulu, alipogundua nini? Na kabla ya kujiuzulu uenyekiti alifanya nini kuhusu hilo dili lililomnufaisha mwenyekiti? Uliliacha tu dili bovu, unethical, la kisifadi, halafu ukakimbia ili usiache fingerprints, sio?

Sio wote wajinga babu Mengi bana.
 
Anasema hakuhusika "katika mchakato wa maamuzi ya kuwekeza kwenye kampuni ya Interchem kwa kuwa alipogundua hilo alijiuzulu." Hakuhusikwa kwa kuwa alipogundua alijiuzulu, maana yake nini, hakuwepo alikuwepo?

Alipogundua alijiuzulu, alipogundua nini? Na kabla ya kujiuzulu uenyekiti alifanya nini kuhusu hilo dili lililomnufaisha mwenyekiti? Uliliacha tu dili bovu halafu ukakimbia ili usiache fingerprints, sio?

Sio wote wajinga babu Mengi bana.

ulichoshindwa kuelewa hapo ni kipi?
 
Aliwataka wanahabari kwenda NICO kuthibitisha suala hilo."


Anasema hakuhusika "katika mchakato wa maamuzi ya kuwekeza kwenye kampuni ya Interchem kwa kuwa alipogundua hilo alijiuzulu." Hakuhusika kwa kuwa alipogundua alijiuzulu, maana yake nini, ulikuwepo hukuwepo?

Alipogundua alijiuzulu, alipogundua nini? Na kabla ya kujiuzulu uenyekiti alifanya nini kuhusu hilo dili lililomnufaisha mwenyekiti? Uliliacha tu dili bovu, unethical, la kisifadi, halafu ukakimbia ili usiache fingerprints, sio?

Sio wote wajinga babu Mengi bana.


- Dilunga hii hoja uliyoirukia unahitaji facts kwanza mkuu maana hoja ni fact by itself, sasa nenda NICO kwanza kapate facts kama ulivyoshauriwa na mawakili wake Mengi, then njoo hapa uzichambue,

- Badala ya kujaribu kueneza speculations zisizokwisha, sasa tunataka kuanza kuelekea kwenye facts tu maana soon mawakili wa Mengi wameahidi wanatangulia kwenye sheria.

- Ni vyema ukaenda NICO kwanza,usije ukawa mjinga bure mkuu!

FMES!
 
haya ndiyo madai ya RA dhidi ya mengi
Jumla ya fedha zote za NBC ambazo akidaiwa Mengi kupitia kampuni yake ya Anche Mwedu Limited (AML) hadi kufikia Januari 1996 zilikuwa ni 5,863,002,196.45. Fedha hizi hadi kufikia sasa 2009 pamoja na hesabu ya riba zinafikia takriban bilioni 28.

kwa wale wataalamu wa mahesabu kutoka bil 5 mpaka bil 28 ni riba ya kiasi gani

au ndio kama yale mambo ya mbowe kakopa mil 7.5 anadaiwa mil 229.

lakini kukopa sio dhambi pia kuna bankruptcy laws
RA ni Jangiri
In 1997, a decision was taken to split NBC into three entities, namely NBC Holding Corporation, National Micro-finance Bank (NMB) and NBC (1997) Limited. source: NBC website
itakuwaje mengi asingiziwe ameua NBC wakati NMB ilikuwa ni part ya NBC wakati anakopa na NMB ndiyo inayopata faida kuliko benki zote tz???

Ogopa sana Compound Interest!! Hiyo ni riba ya kama asilimia 14% TU!!!

kwa hiyo na mimi nime compound kagoda 40bn kwa miaka minne yani kutoka 2005 mpaka sasa hivi kwa hiyo rostam anadaiwa 67bn

bwana kang unatakiwa uwe mwangalifu sana wakati una compound, kwa ajili 14% ni kubwa sana ku compound kwenye loan
mfano mzungu akichukua $200m uki compound kwa 14% unayoitaka wewe baada ya miaka 6 itakuwa $438.99m, kila mtu ange default, loan ime double within 6 yrs

kang kutoka bil 5 mpaka bil 28 ume compound 14% moja kwa moja kwa miaka 13 ambayo ni sawa na APR 43%.
APR 43% NI KUBWA SANA INGEKUWA HIVI WATU WANGEKUWA HAWACHUKUI LOANS KABISA

SIKU ZOTE WANA COMPUND APR NDOGO
 
Last edited:
ulichoshindwa kuelewa hapo ni kipi?

Anasema hahusiki kwa kuwa alipogundua alijiuzulu.

Ufisadi umefanyika kabla hujajiuzulu. Kitendo cha kujiuzulu hakisemi lolote kuhusu kile kilichofanyika kabla hujajiuzulu. Kwa hiyo huwezi kusafishika kwa kusema sikuhusika kwa kuwa nilipogundua nilijiuzulu.

Na ulipogundua ulijiuzulu, ulipogundua nini?

Wewe Mwenyekiti, utatuambiaje hujui chombo chako kinanunua hisa za nani, ngapi, kwa maamuzi ya ofisa gani? Na ulipogundua ulifanya nini na hili dili bovu kabla hujajiuzulu? Sio kila Mtanganyika ni Mdanganyika babu Mengi.
 
Anasema hahusiki kwa kuwa alipogundua alijiuzulu.

Ufisadi umefanyika kabla hujajiuzulu. Kitendo cha kujiuzulu hakisemi lolote kuhusu kile kilichofanyika kabla hujajiuzulu. Kwa hiyo huwezi kusafishika kwa kusema sikuhusika kwa kuwa nilipogundua nilijiuzulu.

Na ulipogundua ulijiuzulu, ulipogundua nini?

Wewe Mwenyekiti, utatuambiaje hujui chombo chako kinanunua hisa za nani, ngapi, kwa maamuzi ya ofisa gani? Na ulipogundua ulifanya nini na hili dili bovu kabla hujajiuzulu? Sio kila Mtanganyika ni Mdanganyika babu Mengi.

- Tafuta kwanza barua ya kujiuzulu kwa Mengi, uiweke hapa ndio uanze kutoa hukumu, mawaliki wake wamesema one thing only kwamba alipogundua alijuzulu, sasa wewe na mimi mpaka sasa hatujui alipogundua nini na alisema nini kwenye barua yake ya kujiuzulu ni vyema tungepata facts kwanza toka NICO badala ya kujaribu ku-create habari zisizo na kichwa wala miguu!

FMEs!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom