Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
so Mengi hakufika Mkutanoni..kawatuma wanasheria sio....as per michuzi blog? akina Lunyungu waliosema wao wataiwakilisha JF hadi sasa hawajasema lolote...
.Inaonyesha hivyo, lakini nilicho kifurahia ni kumtaka aseme hizo hao watu alfu 6000 na kodo anazo jidai analipa ni wapi na kwa kampuni ipi? Hapo ndo patamu, kwani kutoweka jina lako kwenye kampuni ukaghushi na kuweka majina hewa ya kina KYOMUHENDO huo sio ufisadi? huyu Fisadi papa this time kakamatika!
...mkutano wa mengi leo unatakiwa kuzuiwa na vyombo vya usalama ..kwa kuwa unaaingiza nchi kwenye malumbano yasiyoisha .....muda wa mengi kuanza kusumbuliwa na dola wazi umefika ..uvumilivu wao umefika kikomo...
sio mengi tu hata rostam hatakiwi kuzungumza tena....wote wameongea sasa waachie polisi na mahakama zifanye kazi...wasigawe wananchi..
katika taratibu za kawaida za usalama ndio hivyo...sasa ndio tutajuwa kama kweli rais ameapa kulinda usalama wa wananchi au la...hatuwezi kuwa na taifa la kiumbea umbea wa kusutana kama wake wenza ...miaka mitano yote tumekalia kusutana tu hakuna kinachofanyika .... we are tied with this weak gorvernment....watuache tufanye kazi!!
.
Mkuu huu ufisad wa kutumia majina yasiyo, ya wajomba, wadogo n.k hauko kwa RA tu, nawafahamu maprofessor wengi wana-own daladala kwa majina ya ndugu zao.
Swali ni je, tuna sheria katika nchi yetu ya kuzuia hali hiyo?? maana tukisema ni fisad kwa sababu hii naona haiji, wengi wamo humu. Yeye ni fisadi kwa sababu ameiba fedha za umma na sio anatumia majina yasiyo!
.
Mkuu huu ufisad wa kutumia majina yasiyo, ya wajomba, wadogo n.k hauko kwa RA tu, nawafahamu maprofessor wengi wana-own daladala kwa majina ya ndugu zao.
.Swali ni je, tuna sheria katika nchi yetu ya kuzuia hali hiyo?? maana tukisema ni fisadi kwa sababu hii naona haiji, wengi wamo humu.
.Yeye ni fisad kwa sababu ameiba fedha za umma na sio anatumia majina yasiyo!
. Kasema wazi tena kwa kujitapa kuwa watanzania 6,000 kawaajiri na anawalipa viruzi - je ni kwenye shughuli gani kama Caspian hakuna jina lake, Afritainer hakuna jina lake, Kagoda hakuna jina lake, Richmond hakuna jina lake, Dowans hakuna jna lake na New Habari hakuna jina lake!
Mengi kalikoroga, Rostam kalinywa !!
.Kutoka mwananchi
Na Boniface Meena
1. Tuhuma zilizojibiwa na wanasheria hao ni kuhusu fedha za Import Support, kampuni ya Anche Mwedu Limited, utajiri wa Mengi, ukwepaji ulipaji kodi, fedha za misaada na kuwekeza katika biashara, uwekezaji wa kampuni ya NICO kwenye kiwanda cha Interchem Pharma Limited na kuwaita wengine ni wauaji.
3. Kuhusu fedha za Import Support, Ngalo alisema deni la fedha za import support zimeshalipwa tangu mwaka 2008 hivyo Mengi hana deni kama hilo huku wakionyesha kivuli cha hundi walizolipia deni hilo.
4. Kuhusu kampuni ya Anche Mwedu Limited alisema suala hilo liliamuliwa mahakamani katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupitia hukumu iliyosomwa Septemba 30 mwaka 2008 na dai la NBC kupitia Consolidated Holding Cooperation kwenye kesi hiyo lilikataliwa na mahakama kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kuthibitisha deni hilo.
5. Kesi hiyo ya madai nambari 197 ya mwaka 1993 ilifunguliwa na Anche Mwedu Limited dhidi ya Benki Kuu, kampuni za Societe General De Surveilanche S.A, SGS India Private Ltd, Consolidated Holding Corporation, Benki ya NBC na kampuni nyingine ya J.G. Vacuum Flasks Ltd.
6. Kuhusu ukwepaji kodi wanasheria hao walidai kuwa si Mengi wala kampuni yake yoyote ina tuhuma za kukwepa kulipa kodi.
7. Kuhusu uwekezaji wa NICO, Ngalo alidai kuwa si Mengi wala kamati ya uwekezaji ya NICO ilihusika kwa namna yoyote ili katika mchakato wa maamuzi ya kuwekeza kwenye kampuni ya Interchem kwa kuwa alipogundua hilo alijiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa kamati ya uwekezaji na ujumbe na alifanya hivyo kupitia barua aliyoiandikia NICO Agosti 3 mwaka 2007. Aliwataka wanahabari kwenda NICO kuthibitisha suala hilo.
Haya wakuu tuambieni ni wapi kuna kasoro hapa na haya majibu ya Mengi? Wapi kuna uongo?
"Kuhusu uwekezaji wa NICO, Ngalo alidai kuwa si Mengi wala kamati ya uwekezaji ya NICO ilihusika kwa namna yoyote ili katika mchakato wa maamuzi ya kuwekeza kwenye kampuni ya Interchem kwa kuwa alipogundua hilo alijiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa kamati ya uwekezaji na ujumbe na alifanya hivyo kupitia barua aliyoiandikia NICO Agosti 3 mwaka 2007. Aliwataka wanahabari kwenda NICO kuthibitisha suala hilo."
Anasema hakuhusika "katika mchakato wa maamuzi ya kuwekeza kwenye kampuni ya Interchem kwa kuwa alipogundua hilo alijiuzulu." Hakuhusikwa kwa kuwa alipogundua alijiuzulu, maana yake nini, hakuwepo alikuwepo?
Alipogundua alijiuzulu, alipogundua nini? Na kabla ya kujiuzulu uenyekiti alifanya nini kuhusu hilo dili lililomnufaisha mwenyekiti? Uliliacha tu dili bovu halafu ukakimbia ili usiache fingerprints, sio?
Sio wote wajinga babu Mengi bana.
Anasema hakuhusika "katika mchakato wa maamuzi ya kuwekeza kwenye kampuni ya Interchem kwa kuwa alipogundua hilo alijiuzulu." Hakuhusika kwa kuwa alipogundua alijiuzulu, maana yake nini, ulikuwepo hukuwepo?
Alipogundua alijiuzulu, alipogundua nini? Na kabla ya kujiuzulu uenyekiti alifanya nini kuhusu hilo dili lililomnufaisha mwenyekiti? Uliliacha tu dili bovu, unethical, la kisifadi, halafu ukakimbia ili usiache fingerprints, sio?
Sio wote wajinga babu Mengi bana.
In 1997, a decision was taken to split NBC into three entities, namely NBC Holding Corporation, National Micro-finance Bank (NMB) and NBC (1997) Limited. source: NBC websitehaya ndiyo madai ya RA dhidi ya mengi
Jumla ya fedha zote za NBC ambazo akidaiwa Mengi kupitia kampuni yake ya Anche Mwedu Limited (AML) hadi kufikia Januari 1996 zilikuwa ni 5,863,002,196.45. Fedha hizi hadi kufikia sasa 2009 pamoja na hesabu ya riba zinafikia takriban bilioni 28.
kwa wale wataalamu wa mahesabu kutoka bil 5 mpaka bil 28 ni riba ya kiasi gani
au ndio kama yale mambo ya mbowe kakopa mil 7.5 anadaiwa mil 229.
lakini kukopa sio dhambi pia kuna bankruptcy laws
RA ni Jangiri
Ogopa sana Compound Interest!! Hiyo ni riba ya kama asilimia 14% TU!!!
ulichoshindwa kuelewa hapo ni kipi?
Anasema hahusiki kwa kuwa alipogundua alijiuzulu.
Ufisadi umefanyika kabla hujajiuzulu. Kitendo cha kujiuzulu hakisemi lolote kuhusu kile kilichofanyika kabla hujajiuzulu. Kwa hiyo huwezi kusafishika kwa kusema sikuhusika kwa kuwa nilipogundua nilijiuzulu.
Na ulipogundua ulijiuzulu, ulipogundua nini?
Wewe Mwenyekiti, utatuambiaje hujui chombo chako kinanunua hisa za nani, ngapi, kwa maamuzi ya ofisa gani? Na ulipogundua ulifanya nini na hili dili bovu kabla hujajiuzulu? Sio kila Mtanganyika ni Mdanganyika babu Mengi.