Wanasheria wa Reginald Mengi wakutana na waandishi wa habari na Kumjibu Rostam Aziz

Wanasheria wa Reginald Mengi wakutana na waandishi wa habari na Kumjibu Rostam Aziz

Status
Not open for further replies.
Anasema hakuhusika "katika mchakato wa maamuzi ya kuwekeza kwenye kampuni ya Interchem kwa kuwa alipogundua hilo alijiuzulu." Hakuhusika kwa kuwa alipogundua alijiuzulu, maana yake nini, ulikuwepo hukuwepo?

Alipogundua alijiuzulu, alipogundua nini? Na kabla ya kujiuzulu uenyekiti alifanya nini kuhusu hilo dili lililomnufaisha mwenyekiti? Uliliacha tu dili bovu, unethical, la kisifadi, halafu ukakimbia ili usiache fingerprints, sio?

Sio wote wajinga babu Mengi bana.

Maamuzi ya Bodi yaendapo kinyume na maadili na hekima ya mwenyekiti wa bodi ikamtuma kuachaia ngazi uenyekiti, hata fisi mchoyo anaweza ona wivu wa hekima ya mwenyekiti huyo wa bodi, sembuse wewe na mimi????

Ni kipi uonacho hakina hekima kwa mengi kujiuhuzuru baada ya mambo kwenda mrama ndani ya Bodi?

Huenda, nasema huenda wewe unaendana Alinacha nilizo zitaja hapo juu au unaota kuja faidi kifisadi au baba mama mjomba pia shangazi yako pengine anafaidi kifisadi au wewe mwenye unafaidi kifisadi hivi niandikapo.

Mengi anatumia majina yake katika kila kampuni anyofungua hata zile zilizo filisika zina majina yake au walau anaacha Trail.

Sasa huyu Bamasinde Rostam ambaye kwa mdomo wake mwenyewe alisema, alipata mtaji kutokana na Biashara ya Babu zake iloanza 1852 ya kuuza Roho za wanaigunga utumwani huko Uarabuni, ana biashara ngapi zilizo kwenye jina lake ambazo zina jumla ya Wafanyakazi wasio pungua 6000 ukiwatoa Maafisa wa Polisi, Majaji na Mahakimu, Maofisa wa TRA,Maofisa wa Usalama wa Taifa, Maofisa wa Ikulu ikiwa ni pamoja na Rais Kikwete mwenyewe kwenye Pay List yake ya Mitunduruni( Mwituni)??

Usitulazimishe kununua mbuzi kwa mlio wake, tuonyeshe mbuzi mwenyewe.
 
DSC06609.JPG

Mafisadi je mnajua hili ni gari la wagonjwa, mmeuwa wengi bado lile la kijijini kwetu lenye mzazi na mtoto mchanga mtalia, halafu wanasema kuna amani amani gani, ya umasikini heri katusha hizi zingetua kwa mkuu wa kaya, nasikia zinaenda 25km na wasihamishe kambi ili siku nyingine yafike ikulu.
 
- Dilunga hii hoja uliyoirukia unahitaji facts kwanza mkuu maana hoja ni fact by itself, sasa nenda NICO kwanza kapate facts

- Ni vyema ukaenda NICO kwanza,usije ukawa mjinga bure mkuu!

Sasa hivi unanambia niende NICO. Lakini mwanzoni ulikaribisha majibu na hoja na maswali.

Haya wakuu tuambieni ni wapi kuna kasoro hapa na haya majibu ya Mengi? Wapi kuna uongo?

Sasa unamtema, unamtupa Mzee wako Mengi, unasema huna majibu, unataka niende kuuliza NICO.

Mengi kaishiwa bana. Watu wanaisha, hata kina Mogella ilifika mahali wakaisha wakaanza kuhamia Yanga.

Mengi kaishiwa mpaka ana resort kusema maji yake ni spring water kumbe sio? Mpaka Waziri Khan akamwambia Mengi acha kudanganya wateja. Duuu
 
DSC06609.JPG

Mafisadi je mnajua hili ni gari la wagonjwa, mmeuwa wengi bado lile la kijijini kwetu lenye mzazi na mtoto mchanga mtalia, halafu wanasema kuna amani amani gani, ya umasikini heri katusha hizi zingetua kwa mkuu wa kaya, nasikia zinaenda 25km na wasihamishe kambi ili siku nyingine yafike ikulu.

Siyo hivyo tu,

Ningekupo, ningetumia MM na Ujuzi wangu kidogo wa Uchaka na kugeuza katush 2 3 zilekee Ikulu ili zikitua pale uwanjani kwao nao waonje Tamu ya Shida.

In short, Idont wish, I want them Dead
 
Sasa hivi unanambia niende NICO. Lakini mwanzoni ulikaribisha majibu na hoja na maswali.

Sasa unamtema, unamtupa Mzee wako Mengi, unasema huna majibu, unataka niende kuuliza NICO.

Mengi kaishiwa bana. Watu wanaisha, hata kina Mogella ilifika mahali wakaisha wakaanza kuhamia Yanga.

Mengi kaishiwa mpaka ana resort kusema maji yake ni spring water kumbe sio? Mpaka Waziri Khan akamwambia Mengi acha kudanganya wateja. Duuu

Ameishiwa vipi ... hujaonesha kuishiwa kwake zaidi ya kutoa generalized statement kuwa kaishiwa!
 
Interchem ni kampuni ya nani? Yaani kweli hata hapo bodi ilipo-shortlist kampuni za kuwekeza, mwenyekiti alikuwa hana habari? Kama kujitoa ni kbla ya mchakato kutokana na potential conflict of interest! Kama alikuja gundua after the fact kuwa kampuni ambayo yeye ni mwenyekiti imeamua kuwekeza katika kampuni ambayo tunaambiwa anahusika nayo, basi tatizo ni kubwa kuliko tunavyoambiwa. Kama hahusiki na hiyo kampuni ya Interchem, basi kwa nini alijiuzulu baada ya mchakato"? Kukamilisha mchakato si kuingia mkataba. Kwa nini, badala ya kujiuzulu asitumie nguvu zake kama mwenyekiti kuzuia uwekazaji huo?

Amandla......
 
Tofauti ya kujiuzulu na kusisitisha mkataba hapa ni ipi? Ni kingekuwa tofauti (matokeo ya tendo) kwenye kusitisha mkataba zaidi ya kujiuzulu? Unaweza kufafanua zaidi?
 
... mawaliki wake wamesema one thing only kwamba alipogundua alijuzulu, sasa wewe na mimi mpaka sasa hatujui alipogundua nini na alisema nini kwenye barua yake ya kujiuzulu ni vyema tungepata facts kwanza toka NICO

Sawa, basi kama hujui nini kilijili, kama huna facts, huna clue, unasema hujui kwa nini alijiuzulu, basi usijifanye ku wonder kwamba hakuongopa, hana kasoro, hujui. Hujui.

Haya wakuu tuambieni ni wapi kuna kasoro hapa na haya majibu ya Mengi? Wapi kuna uongo?

Alipogundua alijiuzulu, alipogundua nini?

Kama wewe mwenyekiti hukujua, basi ni nani anaamua NICO iingie hisa wapi, ngapi na kwa nini?

Mwenyekiti ulifanya nini kabla ya kujizulu ulipogundua dili la kifisadi, dili hasara?

Hukuhusikwa kwa kuwa ulijiuzulu, kwa hiyo ulipojiuzulu ndio ufisadi ukafanyika?

Field Marshall, unaweza kunambia nikaulize NICO, sawa, basi usijifanye kukaribisha maswali na hoja; na wewe hujui, umesema hujui. Hujui.
 
Anasema hahusiki kwa kuwa alipogundua alijiuzulu.

Ufisadi umefanyika kabla hujajiuzulu. Kitendo cha kujiuzulu hakisemi lolote kuhusu kile kilichofanyika kabla hujajiuzulu. Kwa hiyo huwezi kusafishika kwa kusema sikuhusika kwa kuwa nilipogundua nilijiuzulu.

Na ulipogundua ulijiuzulu, ulipogundua nini?

Wewe Mwenyekiti, utatuambiaje hujui chombo chako kinanunua hisa za nani, ngapi, kwa maamuzi ya ofisa gani? Na ulipogundua ulifanya nini na hili dili bovu kabla hujajiuzulu? Sio kila Mtanganyika ni Mdanganyika babu Mengi.

Bado hujaeleza ambacho hujakielewa hapa. Kwamba kujiuzulu kulitokea baada ya kugundua au vinginevyo?! kilichoshindwa kueleweka hapo ni kipi?
 
Sasa hivi unanambia niende NICO. Lakini mwanzoni ulikaribisha majibu na hoja na maswali.

Sasa unamtema, unamtupa Mzee wako Mengi, unasema huna majibu, unataka niende kuuliza NICO.

Mengi kaishiwa bana. Watu wanaisha, hata kina Mogella ilifika mahali wakaisha wakaanza kuhamia Yanga.

Mengi kaishiwa mpaka ana resort kusema maji yake ni spring water kumbe sio? Mpaka Waziri Khan akamwambia Mengi acha kudanganya wateja. Duuu

Kipi hapa kinaleta mzengwe?

Hata kama mengi anajibu kuhusu NICO sidhanio kwamba ana mamlaka ya kutoa jibu hilo kwa sababu yeyey si msemaji wa NICO.

Ukiuliza swali huwezi kuchagua au kupanga ujibiwe nini. Ukipewa jibu ambalo huridhiki unauliza swali jingine au unatoa kauri kwamba huridhiki na jibu kwa sababu ambazo unazitaja vile vile.

Tafsiri ya kuishiwa inaweza kuwa sahihi tu ukiijengea hoja.

Kwenye Bishara kuna lugha za kibiashara.
Ukiambiwa hiki ni kinywaji cha kizazi cha leo ( Coca cola) wakati kinywaji hicho kiligunduliwa kabla babu wa babu hajazaliwa unaamini tu kama unapenda kuamini.

Lakini kama uko Chuo Kikuu unafundisha hydrology ukisema maji ya chemchem una maana chemchem. Ukisema maji ya mto Rufiji una maana hiyo pia.

Lakini Yote 9........10 Kwa Mara ya kwanza kabisa katika Historia ya Ufisadi Mzee Mengi kaweza kumchokonoa na kumlambisha pilipili Nunda wetu namba 1 Rostam Aziz akiwa ndani ya mwenye pango lake na kumfanya atoe Kiwiliwili chake chote nje, Baada kujifunika Blangeti la ukimya kwa masaa kibao.
 
Sawa, basi kama hujui nini kilijili, kama huna facts, huna clue, unasema hujui kwa nini alijiuzulu, basi usijifanye ku wonder kwamba hakuongopa, hana kasoro, hujui. Hujui.

Alipogundua alijiuzulu, alipogundua nini?

Kama wewe mwenyekiti hukujua, basi ni nani anaamua NICO iingie hisa wapi, ngapi na kwa nini?

Mwenyekiti ulifanya nini kabla ya kujizulu ulipogundua dili la kifisadi, dili hasara?

Hukuhusikwa kwa kuwa ulijiuzulu, kwa hiyo ulipojiuzulu ndio ufisadi ukafanyika?

Field Marshall, unaweza kunambia nikaulize NICO, sawa, basi usijifanye kukaribisha maswali na hoja; na wewe hujui, umesema hujui. Hujui.

Kujichanganya kwingi lakini point unayoiongelea huiweki wazi. Naona wewe unajaribu kuona kisichopo kwenye maandishi hayo huku wewe mwenyewe ukijaribu kuvuna visivyopandwa!

Kilichosemwa hapo kiko wazi, wewe ndio inabidi ujieleze vyema ili ueleweke
 
Hii kampuni ya NICO ina ishu nyingi sana, nakumbuka kuna thread ilianzishwa na wana JF wote tuliungana kusema kuwa something stinks maana hata walio na hisa za NICO sasa wanaambiwa hawawezi kuuza, akina Felix Mosha na Reginald Mengi wameshafaidika, na wametimiza malengo eti leo tunaambiwa Mengi alijiuzulu?! He should have taken the blame for the failure of NICO na uwekezaji wake mbovu in Interchem and other problems. Leo hii Felix Mosha yuko bodi ya NMB, si ni ufisadi pia?
Sidhani kutomtetea Mengi ni kumtetea Rostam, maana ushahidi upo kuwa nachukia ufisadi wa Rostam na uzembe wa JK, lakini siwezi kumtetea Mengi....
 
aisee, kama kweli haya majibu aliyotoa wakili wa Mengi ni kweli, kuna uwezekano mkubwa Rostam kaingizwa tundu la ******,naogopa sumu sasa....
 
Hii kampuni ya NICO ina ishu nyingi sana, nakumbuka kuna thread ilianzishwa na wana JF wote tuliungana kusema kuwa something stinks maana hata walio na hisa za NICO sasa wanaambiwa hawawezi kuuza, akina Felix Mosha na Reginald Mengi wameshafaidika, na wametimiza malengo eti leo tunaambiwa Mengi alijiuzulu?! He should have taken the blame for the failure of NICO na uwekezaji wake mbovu in Interchem and other problems. Leo hii Felix Mosha yuko bodi ya NMB, si ni ufisadi pia?
Sidhani kutomtetea Mengi ni kumtetea Rostam, maana ushahidi upo kuwa nachukia ufisadi wa Rostam na uzembe wa JK, lakini siwezi kumtetea Mengi....

Sidhani kama kuna kokote kule umelazimishwa kumtetea Mengi hapa.
 
Tofauti ya kujiuzulu na kusisitisha mkataba hapa ni ipi? Ni kingekuwa tofauti (matokeo ya tendo) kwenye kusitisha mkataba zaidi ya kujiuzulu? Unaweza kufafanua zaidi?

Unapojiuzulu unaruhusu menejimenti waingie mkataba uliokuwa ukiupinga. Unapobaki kama mwenyekiti una uwezo mkubwa wa kuzuia menejimenti kuingia katika mkataba au kuwekeza mahali usipotaka. Kumbuka kuwa kwa kawaida menejimenti hawawezi kuingia mkataba au kuwekeza bila baraka za bodi. Menejimenti wanipelekea bodi ripoti za mchakato pamoja na maoni yao ili bodi watoe baraka ( kama ni hicho wanachokitaka) ili waingie kwenye mkataba au wanunue hisa. Wa kikuaidi una nguvu za kuishinikiza bodi yako iwachukulie hatua ya kuingia mkataba usio na maslahi kwa kampuni yako! Anachotaka kutuambia Mkuu ni kuwa alisusa alipoona mambo yanaenda mrama! Hii bado imekaa vibaya.

Amandla......
 
wadau, hivi TBC waliamua ku-edit makusudi au? kumbe kaka KUBENEA alimchana!!! bravo KUBENEA, mpelekeni mahakamani kwanza, kavunja sheria za magazeti!! Mkuchika naamini unalifahamu hili, ukichuna jiuzulu!!
 
nilitegemea nikute vijembe, kuwa je Mengi mbona hajajibu tuhuma???? lakini wapi, katunywesha maji yasiyo, kaua UNICO n.k nikajiuliza huyu kaamua kupambana au kuna jambo, kumbe biashara LOL

Uone Wadangayika tulivyo bendera fuata upepo, yaani asiyeona huitwa ana kengeza.

Si Mengi si Rostam, wote mafisadi.
Wote wanatafuta sympathy ya wananchi kwa kuonyesha nani fisadi zaidi ya mwenzie. Fisadi ni fisadi tu, awe Nyangumi , papa, ngisi, pweza, kibua au dagaa mchele.

It is better to tell the truth and be rejected, than to hold it back and be accepted - by WoS.
 
hii kampuni ya nico ina ishu nyingi sana, nakumbuka kuna thread ilianzishwa na wana jf wote tuliungana kusema kuwa something stinks maana hata walio na hisa za nico sasa wanaambiwa hawawezi kuuza, akina felix mosha na reginald mengi wameshafaidika, na wametimiza malengo eti leo tunaambiwa mengi alijiuzulu?! He should have taken the blame for the failure of nico na uwekezaji wake mbovu in interchem and other problems. Leo hii felix mosha yuko bodi ya nmb, si ni ufisadi pia?
Sidhani kutomtetea mengi ni kumtetea rostam, maana ushahidi upo kuwa nachukia ufisadi wa rostam na uzembe wa jk, lakini siwezi kumtetea mengi....

mengi sio mungu wa biashara, kwa hiyo ukifanya investment siku ingine zinakuwa nzuri siku ingine zinakuwa mbaya hiyvo ndio biashara ilivyo
mbona uwasifu kwa kuhakikisha aslimia fulani ya nmb inabakia tz..
 
Interchem ni kampuni ya nani?
Ni yake na kaka yake.

"InterChem, which was founded in 1987, is a Tanzanian pharmaceutical manufacturing company and was owned jointly by Reginald Mengi and his brother Benjamin Mengi, who is the chairman of the firm.

InterChem Pharma Ltd, the Moshi-based pharmaceutical firm owned by media mogul Reginald Mengi’s younger brother Benjamin, has been placed under receivership over a large debt accrued from Barclays Bank Tanzania Ltd.

The firm, which three years ago acquired a $6 million loan for setting up an anti-retroviral (ARV) drug manufacturing plant in Tanzania, will go under the hammer next year.

Bank sources told The EastAfrican in Dar es Salaam last week that the firm acquired additional investment from Barclays under a debenture agreement and mortgaged its plant in Moshi to the bank.

Barclays Bank Tanzania has already appointed Charles Rwechungura and Dr Alex Nguluma to be receivers and managers of the firm, which faces a mountain of debt owed to various creditors.

According to Mr Rwechungura and Dr Nguluma, the firm’s assets and business are being offered for sale by competitive tender to recover the loan.

The two receiver managers were on December 27, 2008, expected to take possession of all properties owned by the firm under the bank’s instructions after the company failed to honour its debts.

The bank source said that InterChem Pharma Ltd also borrowed some $10 million from the bank and other sources for setting up a penicillin-products manufacturing facility within a maximum period of two years.

The project envisaged expansion of the existing tablets and capsule line, establishing a new penicillin plant (liquids, dry powder, tablets, and capsules) as well as establishing a new line for the production of tabs and capsules for HIV.

Foreign collaboration was sought in the form of joint-venture partnership, buy-back arrangement and/or equipment purchase to facilitate implementation of the project.

The company was incorporated in 1983. It manufactures liquids, tablets, capsules, creams, ointments, dry powders, external preparations and veterinary medicines.
"
 
Unapojiuzulu unaruhusu menejimenti waingie mkataba uliokuwa ukiupinga. Unapobaki kama mwenyekiti una uwezo mkubwa wa kuzuia menejimenti kuingia katika mkataba au kuwekeza mahali usipotaka. Kumbuka kuwa kwa kawaida menejimenti hawawezi kuingia mkataba au kuwekeza bila baraka za bodi. Menejimenti wanipelekea bodi ripoti za mchakato pamoja na maoni yao ili bodi watoe baraka ( kama ni hicho wanachokitaka) ili waingie kwenye mkataba au wanunue hisa. Wa kikuaidi una nguvu za kuishinikiza bodi yako iwachukulie hatua ya kuingia mkataba usio na maslahi kwa kampuni yako! Anachotaka kutuambia Mkuu ni kuwa alisusa alipoona mambo yanaenda mrama! Hii bado imekaa vibaya.

Amandla......

Haya ya kususa ni maoni yako binafsi na sio ukweli wa kilichotokea. Unachofanya hapa ni speculation tu maana unajaribu kueleza kitu unachotaka au ulichotegemea kuwa kingetokea bila kuwa na facts kama kilitokea au la.

Una maelezo zaidi ya hili au uko tayari kuweka qualification kwenye maandishi yako kuelezea kuwa haya ni maoni yako binafsi na wala sio kile kilichotokea NICO?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom