Madela Wa- Madilu
JF-Expert Member
- Mar 24, 2007
- 3,063
- 735
Anasema hakuhusika "katika mchakato wa maamuzi ya kuwekeza kwenye kampuni ya Interchem kwa kuwa alipogundua hilo alijiuzulu." Hakuhusika kwa kuwa alipogundua alijiuzulu, maana yake nini, ulikuwepo hukuwepo?
Alipogundua alijiuzulu, alipogundua nini? Na kabla ya kujiuzulu uenyekiti alifanya nini kuhusu hilo dili lililomnufaisha mwenyekiti? Uliliacha tu dili bovu, unethical, la kisifadi, halafu ukakimbia ili usiache fingerprints, sio?
Sio wote wajinga babu Mengi bana.
Maamuzi ya Bodi yaendapo kinyume na maadili na hekima ya mwenyekiti wa bodi ikamtuma kuachaia ngazi uenyekiti, hata fisi mchoyo anaweza ona wivu wa hekima ya mwenyekiti huyo wa bodi, sembuse wewe na mimi????
Ni kipi uonacho hakina hekima kwa mengi kujiuhuzuru baada ya mambo kwenda mrama ndani ya Bodi?
Huenda, nasema huenda wewe unaendana Alinacha nilizo zitaja hapo juu au unaota kuja faidi kifisadi au baba mama mjomba pia shangazi yako pengine anafaidi kifisadi au wewe mwenye unafaidi kifisadi hivi niandikapo.
Mengi anatumia majina yake katika kila kampuni anyofungua hata zile zilizo filisika zina majina yake au walau anaacha Trail.
Sasa huyu Bamasinde Rostam ambaye kwa mdomo wake mwenyewe alisema, alipata mtaji kutokana na Biashara ya Babu zake iloanza 1852 ya kuuza Roho za wanaigunga utumwani huko Uarabuni, ana biashara ngapi zilizo kwenye jina lake ambazo zina jumla ya Wafanyakazi wasio pungua 6000 ukiwatoa Maafisa wa Polisi, Majaji na Mahakimu, Maofisa wa TRA,Maofisa wa Usalama wa Taifa, Maofisa wa Ikulu ikiwa ni pamoja na Rais Kikwete mwenyewe kwenye Pay List yake ya Mitunduruni( Mwituni)??
Usitulazimishe kununua mbuzi kwa mlio wake, tuonyeshe mbuzi mwenyewe.