Wanasheria wa Reginald Mengi wakutana na waandishi wa habari na Kumjibu Rostam Aziz

Status
Not open for further replies.
Ni Mengi huyu huyu alikuwa akionyesha video za vita Sierra Leone kupitia ITV ili awatishe wananchi wasiwapigie kura vyama vya upinzani kwenye uchaguzi wa mwaka 2000. Alikuwa akiconvince wananchi kuwa kupigia kura upinzani ni sawa na kukaribisha vita, na athari za vita ndizo alizokuwa akionyesha kwenye hizo sinema za bure.

Sinema hizi za vita pia zilionyeshwa maeneo ya vijijini ambapo TV zilikuwa hazipatikani kipindi hicho ili kuondoa kabisa imani ya wananchi kwa vyama vya upinzani. Kwa kweli alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwani kura walizopata wapinzani zilipungua ukilinganisha na walizopata 1995, wakati ambapo mwaka 2000 wapinzani walitegemewa wapate kura zaidi ya walizopata 1995.

Mengi huyu huyu mtakatifu....alirudisha nyuma nguvu za vyama vya upinzani na hivyo kutoa mwanya wa ufisadi kukita mizizi katika nchi pendwa Tanzania. Laiti upinzani ungepata nafasi ya kutawala kipindi cha 2000-2005, ufisadi usingekuwepo.

Bwa ha ha haha... ukisikia kuishiwa hoja.
 
- Mkuu Dilunga yaani haya hata Rostam hayajui, sasa hebu weka source mkuu maana this is serious. Weka source ya hii mkuu!

FMEs!
Almost kila kitu alichosema Rostam kuhusu mengi kilikuwa correct but not accurate... Sababu ni kwamba Rostam haku-update data zake as of December 2008 angetuletea say May 2008... Tungempeleka Mengi Lupango.
Jambo rahisi ni kwamba Mengi si msafi.
Mengi alijiuzulu Mwenyekiti wa Investment Comittee, swali je alikuwa kwenye board au hapana.
 
Mkuu FMES,
Nimesikitishwa sana na uchambuzi wako kwenye swala hili.
Mengi ni Fisadi Nyangumi kwa nini?
Pesa ya Import Suport ni ya Zamani sana... Alilipa mwaka jana alikuwa akisubiria nini?
Si mwaka jana ndio serikali ilianza kuzifuatilia tena kwa kutaka kuwa na mkusanya madeni?
je serikali isingefanya hivyo mengi si angechikichia.
Hana lolote.

- Mkuu Kasheshe, ahsante kwa ujumbe wako, ila nina swali moja tu kwako eti Rostam ameajiri wapi wananchi 6000? Maana Brela hakuna kampuni hata moja yenye jina lake, naomba msaada wako tafadhali!

FMEs!
 
Almost kila kitu alichosema Rostam kuhusu mengi kilikuwa correct but not accurate... Sababu ni kwamba Rostam haku-update data zake as of December 2008 angetuletea say May 2008... Tungempeleka Mengi Lupango.
Jambo rahisi ni kwamba Mengi si msafi.
Mengi alijiuzulu Mwenyekiti wa Investment Comittee, swali je alikuwa kwenye board au hapana.
It is either correct and accurate or not correct and therefore not accurate. You cannot have it bothways.
 
Mkuu FMES,
Nimesikitishwa sana na uchambuzi wako kwenye swala hili.
Mengi ni Fisadi Nyangumi kwa nini?
Pesa ya Import Suport ni ya Zamani sana... Alilipa mwaka jana alikuwa akisubiria nini?
Si mwaka jana ndio serikali ilianza kuzifuatilia tena kwa kutaka kuwa na mkusanya madeni?
je serikali isingefanya hivyo mengi si angechikichia.
Hana lolote.
Waliotaka kuchikichia wapo na mpaka sasa hawajazirudisha, na list hiyo imejaa baadhi ya wabunge na hata mawaziri akiwemo RA. Wale ambao wana nia ya kuzilipa wamefanya hivyo regardless lini. Hivyo ili hoja zako ziwe na mashiko, ni lazima uonyeshe ni vipi mtu asiye na nia kulipa afanye hivyo tangu mwaka jana, na mwenye aendelee kulipa kidogo kidogo au kutolipa kabisa!!
 
Almost kila kitu alichosema Rostam kuhusu mengi kilikuwa correct but not accurate... Sababu ni kwamba Rostam haku-update data zake as of December 2008 angetuletea say May 2008... Tungempeleka Mengi Lupango.
Jambo rahisi ni kwamba Mengi si msafi.
Mengi alijiuzulu Mwenyekiti wa Investment Comittee, swali je alikuwa kwenye board au hapana.

- Rostam alikuwa correct, lakini not accurate mkuu wangu Kasheshe kwa kweli hapa ninahitaji kurudi shule tena, yaani kweli tuna sheria Tanzania ya kuwapeleka lupango wanoshutumiwa na shutuma ambazo ni correct but not accurate? Ohhh my God help me!

FMEs!
 
Angalau yeye amelipa. Fisadi Rostum hata kukiri tu kuwa alichukua hela za EPA kupitia Kagoda hakubali. Wala hana mpango wa kulipa. Anajidai hajawahi kukutana na marehemu Ballali. What a liar!
Tuwekee bandiko la kuonyesha Rostam ni shareholder wa Kagoda, au board member wa Kagoda au Dowans..
Acha porojo kaka!
 
It is either correct and accurate or not correct and therefore not not accurate. You cannot have it bothways.

Jasusi,
Nimekupata, hawa mawakili wa mashetani, naona wameanza kutoa mapovu...ni upimbi tu wa kufikiri.
 
Almost kila kitu alichosema Rostam kuhusu mengi kilikuwa correct but not accurate... Sababu ni kwamba Rostam haku-update data zake as of December 2008 angetuletea say May 2008... Tungempeleka Mengi Lupango.
Jambo rahisi ni kwamba Mengi si msafi.
Mengi alijiuzulu Mwenyekiti wa Investment Comittee, swali je alikuwa kwenye board au hapana.

Umetumia kipimo gani kuonyesha kuwa almost alichosema Rostam kuhusu Mengi ni correct? uthibitisho upo?
 
Mkuu FMES,
Nimesikitishwa sana na uchambuzi wako kwenye swala hili.
Mengi ni Fisadi Nyangumi kwa nini?
Pesa ya Import Suport ni ya Zamani sana... Alilipa mwaka jana alikuwa akisubiria nini?
Si mwaka jana ndio serikali ilianza kuzifuatilia tena kwa kutaka kuwa na mkusanya madeni?
je serikali isingefanya hivyo mengi si angechikichia.
Hana lolote.
.

Hapa wewe ndio unyesikitisha. Tuambie basi timeline aliyotakiwa kuwa amelipa. Hii inakuwaje ni kashfa wakati unakiri kalipa alichokuwa akidaiwa? Jasusi kahitimisha mengi hajakataa madeni na mnaonyesha kalipa na kamaa kuna mengineyo anaendelea kulipa. Rostam anaikana Kagoda kama anavyokana makampuni yake yote
 
Tuwekee bandiko la kuonyesha Rostam ni shareholder wa Kagoda, au board member wa Kagoda au Dowans..
Acha porojo kaka
!

- Mkuu Kasheshe wewe ni taifa kubwa acha hasira, Rostam ameajiri wapi wafanyakazi 6000 aliodai jana? Na ni kina nani hao aliowaajiri?

- Ukitaka ya Rostam na Dowans, nenda kwenye kamati ya bunge ya Mwakyembe, alikoitwa lakini akakimbia hayo unayoyauliza yapo kule mkuu!

FMES!
 
NICO si kampuni ya watu maskini! Ukweli usipotoshwe! Maskini wa Tanzania hawawekezi kwenye hisa! Majority (more than 50%) shareholders wa NICO ni watu werevu kama akina Lipumba na institutional investors! Hawa walikuwa na uwezo wa kumshitaki mengi au hata kumfire kama angekuwa amefanya hayo mafioso! Ni maajabu kuwa RA anatuchukulia watanzania wote hatuna hata elimu ya uchumi/biashara/finance!

RA ametuibia na ana jinai. Hizo za Mengi ni issues za madai tu! Hazituhusu watanzania kwa ujumla wetu! Waache NBC Holding nk na walioliwa na Mengi wamshitaki!
 
FMES,
Unajua hata mwizi akikamatwa ready-handed akafikishwa mahakamani akasomewa mashtaka kitu cha kwa kwanza ni kusema "siyo kweli" Hii aina ya watu wa kasheshe ni kasheshe kweli kwa waelewesha ni sawa na kumwimbia kiziwi. Atazi kukwambia uimbe tena na tena.
 
Quote:

Tuwekee bandiko la kuonyesha Rostam ni shareholder wa Kagoda, au board member wa Kagoda au Dowans..
Acha porojo kaka
!

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe 31 Disemba 2007 siku ilipowasilisha taarifa yake kwako, Kamati Teule ilikuwa imewahoji jumla ya mashahidi 75 na kuuliza maswali 2717 na kuzipitia nyaraka na kumbukumbu 104. Mashahidi 4 kati ya hao walikuja kwa hiari yao bila kupelekewa hati za kuitwa. Mashahidi 7 waliitwa mara mbili. Mashahidi wawili, Ndugu Daniel Yona na Mhe. Rostam Aziz, (Mb) walipelekewa hati za kuitwa mbele ya Kamati Teule lakini hawakufika kwa maelezo kwamba walikuwa nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, Ndugu Daniel Yona alitakiwa na Kamati Teule atoe maelezo kuhusu msingi wa uamuzi wake wa kuipa Richmond Development Company LLC, haki maalum ya kipekee (exclusive right) ya miezi 18 kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza mwaka 2004 wakati huo akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Maelezo ya ziada ya mradi huu nitayatoa baadaye.

Mheshimiwa Spika, vilevile Mhe. Rostam Aziz alitakiwa atoe maelezo kuhusu uhusiano wake na Kampuni za Richmond Development Company LLC na Dowans Holdings S.A baada ya mashahidi kadhaa kudai kuwa ana uhusiano nazo.
Aidha, alitakiwa na Kamati Teule aeleze kwa nini anwani ya barua pepe ya kampuni yake ya Caspian Construction Ltd ilitumiwa na Dowans. Kamati Teule ilitaka vilevile kupata ufafanuzi kutoka kwake kuhusu baadhi ya wafanyakazi wa kampuni yake wanaosemekana kuwa ni watumishi vilevile wa Dowans Holdings S.A.
 
Kumkoma nyani giladi!
 
Laiti hizo pesa zote za EPA, NBC, CIS tungelikopeshwa sisi wauza nyanya, walipa kodi, uchumi wa nchi yetu ungesogea mbele kidogo.

Bahati mbaya pesa wamepewa Mapapa na Manyangumi, leo yanajifanya eti yanatupenda sisi Sato na Sangara, uwizi mtupu, wanataka kutumeza.

Wewe jifanye rafiki wa papa au nyangumi, wakipata njaa, utageuka kitoweo. Heri mimi sijasema!
 
NICO si kampuni ya watu maskini! Ukweli usipotoshwe! Maskini wa Tanzania hawawekezi kwenye hisa! Majority (more than 50%) shareholders wa NICO ni watu werevu kama akina Lipumba na institutional investors! Hawa walikuwa na uwezo wa kumshitaki mengi au hata kumfire kama angekuwa amefanya hayo mafioso! Ni maajabu kuwa RA anatuchukulia watanzania wote hatuna hata elimu ya uchumi/biashara/finance!

RA ametuibia na ana jinai. Hizo za Mengi ni issues za madai tu! Hazituhusu watanzania kwa ujumla wetu! Waache NBC Holding nk na walioliwa na Mengi wamshitaki!

Kwani share zinauzwa kiasi gani? kama share moja ni shilingi 1000, share 300 zitakuwa ni kiasi cha shilingi laki 3 ambazo ni wastani wa kupanda mbegu DECI. Ukisema maskini Bongo hawanunui share, angalia wateja wakubwa wa DECI ni akina nani kama sio hao maskini unaowakandia kuwa hawawezi kuwekeza.
 
NICO si kampuni ya watu maskini! Ukweli usipotoshwe! Maskini wa Tanzania hawawekezi kwenye hisa! Majority (more than 50%) shareholders wa NICO ni watu werevu kama akina Lipumba na institutional investors! Hawa walikuwa na uwezo wa kumshitaki mengi au hata kumfire kama angekuwa amefanya hayo mafioso! Ni maajabu kuwa RA anatuchukulia watanzania wote hatuna hata elimu ya uchumi/biashara/finance!

RA ametuibia na ana jinai. Hizo za Mengi ni issues za madai tu! Hazituhusu watanzania kwa ujumla wetu! Waache NBC Holding nk na walioliwa na Mengi wamshitaki!

- NICO ni shirika la Mosha, mzee mmoja mjanja mjanja sana nimeishi naye sana NY, alijaribu ubunge akashindwa na kupoteza hela nyingi sana huku NICO ndiko alikozirudisha zote, Mengi hukumjua mwanzoni ila naamini alija mshitukia later na kubwaga manyanga!

Respect.

FMEs!
 
Laiti hizo pesa zote za EPA, NBC, CIS tungelikopeshwa sisi wauza nyanya, walipa kodi, uchumi wa nchi yetu ungesogea mbele kidogo.

Bahati mbaya pesa wamepewa Mapapa na Manyangumi, leo yanajifanya eti yanatupenda sisi Sato na Sangara, uwizi mtupu, wanataka kutumeza.

Wewe jifanye rafiki wa papa au nyangumi, wakipata njaa, utageuka kitoweo. Heri mimi sijasema!

Kwa mapenzi ya 'nyangumi' ni bora zaidi kwangu hasa nikikumbuka maneno ya biblia kuwa alimmeza Yohane na kumtapika baada ya siku tatu. Lakini sioni mahala kokote kwenye biblia au kwenye kashfa za mafisadi ambako PAPA anaweza kukula na kukutapika, akikumeza ndio imetoka, na sisi hapa hatukubali mpaka kieleweke. Narudia kwenye mpambano huu, namkubali zaidi 'Nyangumi' kuliko PAPA RA.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom