Ni Mengi huyu huyu alikuwa akionyesha video za vita Sierra Leone kupitia ITV ili awatishe wananchi wasiwapigie kura vyama vya upinzani kwenye uchaguzi wa mwaka 2000. Alikuwa akiconvince wananchi kuwa kupigia kura upinzani ni sawa na kukaribisha vita, na athari za vita ndizo alizokuwa akionyesha kwenye hizo sinema za bure.
Sinema hizi za vita pia zilionyeshwa maeneo ya vijijini ambapo TV zilikuwa hazipatikani kipindi hicho ili kuondoa kabisa imani ya wananchi kwa vyama vya upinzani. Kwa kweli alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwani kura walizopata wapinzani zilipungua ukilinganisha na walizopata 1995, wakati ambapo mwaka 2000 wapinzani walitegemewa wapate kura zaidi ya walizopata 1995.
Mengi huyu huyu mtakatifu....alirudisha nyuma nguvu za vyama vya upinzani na hivyo kutoa mwanya wa ufisadi kukita mizizi katika nchi pendwa Tanzania. Laiti upinzani ungepata nafasi ya kutawala kipindi cha 2000-2005, ufisadi usingekuwepo.
Bwa ha ha haha... ukisikia kuishiwa hoja.
