Wanasheria wa Reginald Mengi wakutana na waandishi wa habari na Kumjibu Rostam Aziz

Wanasheria wa Reginald Mengi wakutana na waandishi wa habari na Kumjibu Rostam Aziz

Status
Not open for further replies.
Kwa mapenzi ya 'nyangumi' ni bora zaidi kwangu hasa nikikumbuka maneno ya biblia kuwa alimmeza Yohane na kumtapika baada ya siku tatu. Lakini sioni mahala kokote kwenye biblia au kwenye kashfa za mafisadi ambako PAPA anaweza kukula na kukutapika, akikumeza ndio imetoka, na sisi hapa hatukubali mpaka kieleweke. Narudia kwenye mpambano huu, namkubali zaidi 'Nyangumi' kuliko PAPA RA.

Swala si bei ya share bali ni awareness tu na facts! Unajua NICO asilimia zaidi ya 50 nani anamiliki? Na hao wamiliki ni maskini! Na asilimia 51% ni deciding majority katika hii biashara ya shares! Mengi hajajiweka hapo amewekwa na shareholders ambao wanahiari ya kumtoa! Hapa hakuna siasa!
 
Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe 31 Disemba 2007 siku ilipowasilisha taarifa yake kwako, Kamati Teule ilikuwa imewahoji jumla ya mashahidi 75 na kuuliza maswali 2717 na kuzipitia nyaraka na kumbukumbu 104. Mashahidi 4 kati ya hao walikuja kwa hiari yao bila kupelekewa hati za kuitwa. Mashahidi 7 waliitwa mara mbili. Mashahidi wawili, Ndugu Daniel Yona na Mhe. Rostam Aziz, (Mb) walipelekewa hati za kuitwa mbele ya Kamati Teule lakini hawakufika kwa maelezo kwamba walikuwa nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, Ndugu Daniel Yona alitakiwa na Kamati Teule atoe maelezo kuhusu msingi wa uamuzi wake wa kuipa Richmond Development Company LLC, haki maalum ya kipekee (exclusive right) ya miezi 18 kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza mwaka 2004 wakati huo akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Maelezo ya ziada ya mradi huu nitayatoa baadaye.

Mheshimiwa Spika, vilevile Mhe. Rostam Aziz alitakiwa atoe maelezo kuhusu uhusiano wake na Kampuni za Richmond Development Company LLC na Dowans Holdings S.A baada ya mashahidi kadhaa kudai kuwa ana uhusiano nazo. Aidha, alitakiwa na Kamati Teule aeleze kwa nini anwani ya barua pepe ya kampuni yake ya Caspian Construction Ltd ilitumiwa na Dowans. Kamati Teule ilitaka vilevile kupata ufafanuzi kutoka kwake kuhusu baadhi ya wafanyakazi wa kampuni yake wanaosemekana kuwa ni watumishi vilevile wa Dowans Holdings S.A.


Well done mkulu, Kasheshe na RA wanadhani tumesahau. Kwani RA alikuwa cleared na tume ya Mwakyembe wakati hakuojiwa wala hakutokea kwenye kamati ya Mwakyembe? Alihitaji awe cleared na waandishi wa habari?
 
Mawakili wa Mengi naona ndio wametoa clearance za tuhuma za RA kwenye ITV bahati mbaya nimekuta wanamalizia. Aliyeona coverage yote atuwekee hapa.
 
Kwani share zinauzwa kiasi gani? kama share moja ni shilingi 1000, share 300 zitakuwa ni kiasi cha shilingi laki 3 ambazo ni wastani wa kupanda mbegu DECI. Ukisema maskini Bongo hawanunui share, angalia wateja wakubwa wa DECI ni akina nani kama sio hao maskini unaowakandia kuwa hawawezi kuwekeza.

Process ya kununua shares si kama ya DECI! Hawafuati watu nyumbani/kanisani na kwenye shares hakuna kuvuna harakaharaka kama DECI! Unadhani kilichowapeleka maskini DECI ni upeo wa kuwekeza na sio kuvuna kusikokuwa na justification ya kibiashara! DECI ulikuwa wizi na maskini waliingia mtego wa wizi!
 
Wakuu mara mmesahau tulipotoka?..
Mnakumbuka tulipoanzia na Bcstimes?..
Navyokumbuka mimi bcstimes ilikuwa jarida la kina Idd Simba na hapo ndipo tulipopata habari za kuzaliwa kwa NICO na walituma mwaliko kwa wanachama wote tuhudhurie mkutano wao uliofanyika Royal Palm...
Lakini kutokana na vigongo vya wachangiaji humu nadhani Mh. Idd Simba ilibidi atumwage kwa sababu (nilivyosikia) alifuatwa sana na vigogo kuhusiana na mijadala ya Bcstimes.....toka hapo ndipo ikazaliwa Jamboforums, kisha Jamii..lakini bila shaka nilipokuwa nikisoma ukurasa za mwanzo zilibeba sana habari zinazohusiana na DSE na NICO hivyo bila shaka ilikuwa jarida la NICO kujaribu kutuhamasisha wananchi kununua hisa huko..badala yake kama kawaida Wadangayika wengi tulijimwaga ktk ukumbi wa mjadala - SIASA.....
 
Mengi, Rostam waendeleza piga nikupige

Na Boniface Meena


MALUMBANO kati ya wafanyabiashara maarufu nchini Reginald Mengi na Rostam Aziz, yaliendelea jana kufuatia wanasheria wa Mengi, Michael Ngalo na Agapitus Nguma kujibu baadhi ya hoja zilizotolewa na Rostam juzi huku wakiacha kujibu hoja nyingine na kuongeza maswali kadhaa waliyodai yanahitaji majibu.

Katika mkutano na waandishi wa habari mwanasheria wa Mengi, Michael Ngalo wa Ngalo & Company Advocates alijibu baadhi ya tuhuma hizo kwa niaba ya Mengi na kudai kuwa wako mbioni kumfungulia kesi Rostam Aziz kutokana na tuhuma hizo wanazodai kuwa ni za uongo.

Tuhuma zilizojibiwa na wanasheria hao ni kuhusu fedha za Import Support, kampuni ya Anche Mwedu Limited, utajiri wa Mengi, ukwepaji ulipaji kodi, fedha za misaada na kuwekeza katika biashara, uwekezaji wa kampuni ya NICO kwenye kiwanda cha Interchem Pharma Limited na kuwaita wengine ni wauaji.

Tuhuma ambazo hazikujibiwa na Mengi ambazo zilitolewa na Rostam ni kuhusu kuwa na akaunti ya fedha za kigeni nje ya nchi, malipo kwa wafanyakazi wake, kuhusu kuwa na ugomvi na baadhi ya viongozi na kutaka matatizo hayo yawe ya kitaifa na tuhuma nyinginezo.

Kuhusu fedha za Import Support, Ngalo alisema deni la fedha za import support zimeshalipwa tangu mwaka 2008 hivyo Mengi hana deni kama hilo huku wakionyesha kivuli cha hundi walizolipia deni hilo.

Kuhusu kampuni ya Anche Mwedu Limited alisema suala hilo liliamuliwa mahakamani katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupitia hukumu iliyosomwa Septemba 30 mwaka 2008 na dai la NBC kupitia Consolidated Holding Cooperation kwenye kesi hiyo lilikataliwa na mahakama kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kuthibitisha deni hilo.

Kesi hiyo ya madai nambari 197 ya mwaka 1993 ilifunguliwa na Anche Mwedu Limited dhidi ya Benki Kuu, kampuni za Societe General De Surveilanche S.A, SGS India Private Ltd, Consolidated Holding Corporation, Benki ya NBC na kampuni nyingine ya J.G. Vacuum Flasks Ltd.

Kuhusu ukwepaji kodi wanasheria hao walidai kuwa si Mengi wala kampuni yake yoyote ina tuhuma za kukwepa kulipa kodi.

Kuhusu uwekezaji wa NICO, Ngalo alidai kuwa si Mengi wala kamati ya uwekezaji ya NICO ilihusika kwa namna yoyote ili katika mchakato wa maamuzi ya kuwekeza kwenye kampuni ya Interchem kwa kuwa alipogundua hilo alijiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa kamati ya uwekezaji na ujumbe na alifanya hivyo kupitia barua aliyoiandikia NICO Agosti 3 mwaka 2007. Aliwataka wanahabari kwenda NICO kuthibitisha suala hilo.

Hata hivyo Mengi kupitia mwanasheria wake aitwaye Nguma alimtaka Rostam kujibu maswali manne, la kwanza, likiwa la kutaka kujua anafanya biashara gani nchini na ataje biashara hizo anazoziendesha na pia kama kampuni zake zimesajiliwa BRELA kwa kutumia jina lake.

Pia alimtaka aeleze kama zinalipa kodi, na kuhusu kuwa hana uhusiano na Kagoda aeleze alikuwa akienda benki kujadiliana juu ya akaunti ya Kagoda alikuwa akifanya hivyo kama nani.

Kuhusu Dowans aeleze mipango ya benki kuipatia Dowans fedha za mkopo aliokuwa na aliushughulikia kama nani, na uhusiano na Richmond anawafahamu vipi wahusika wake.

Hatua hiyo ya Mengi kujibu baadhi ya tuhuma, na kutoa maswali hayo imekuja siku mbili baada ya mfanyabiashara Rostam Aziz kumlipua Mengi na kumbatiza jina la "nyangumi wa ufisadi" baada ya Mengi kumwita yeye na wenzake wanne kuwa ni mafisadi papa.

Rostam Aziz, ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara watano waliotuhumiwa na Mengi kuwa mapapa wa ufisadi, alitoa mlolongo wa tuhuma za ufisadi dhidi ya mwenyekiti huyo mtendaji wa makampuni ya IPP, na kueleza kuwa atawasilisha vielelezo kwa vyombo husika ndani ya saa 48 ili Mengi aanze kuchunguzwa.

Mapigo ya Rostam, ambayo yanazidi kupandisha joto la vita hiyo ya maneno, yametokana na tuhuma nzito ambazo Mengi alizitoa Aprili 23 wakati alipotaja wafanyabiashara watano akitaka wadhibitiwe mapema, akiwemo mbunge huyo wa Igunga. Tofauti na Mengi ambaye hakutoa vielelezo hapo mwanzo wakati anawataja mafisadi papa hao na kusema yuko tayari kupandishwa kizimbani ili ukweli udhihirike, Rostam aliorodhesha tuhuma nyingi na kuahidi kuzikabidhi kwenye vyombo vya serikali ili hatua zichukuliwe.
 
Mengi kupitia mwanasheria wake aitwaye Nguma atamfungulia mashitaka Rostam kujibu maswali manne,
1) ni kutaka kujua anafanya biashara gani nchini na ataje biashara hizo anazoziendesha na pia kama kampuni zake zimesajiliwa BRELA kwa kutumia jina lake.

2) Pia alimtaka aeleze kama zinalipa kodi,

3) na kuhusu kuwa hana uhusiano na Kagoda aeleze alikuwa akienda benki kujadiliana juu ya akaunti ya Kagoda alikuwa akifanya hivyo kama nani.

4) Kuhusu Dowans aeleze mipango ya benki kuipatia Dowans fedha za mkopo aliokuwa na aliushughulikia kama nani, na uhusiano na Richmond anawafahamu vipi wahusika wake.
 
Last edited:
Hivi ni kwa nini Rostam anadai kuwa na kampuni na kuajiri watu kibao lakini hakuna hata moja iliyo na jina lake BRELA?

Rostam naona sasa amejinasa mwenyewe.
 
Mengi kupitia mwanasheria wake aitwaye Nguma atamfungulia mashitaa Rostam kujibu maswali manne,
1) ni kutaka kujua anafanya biashara gani nchini na ataje biashara hizo anazoziendesha na pia kama kampuni zake zimesajiliwa BRELA kwa kutumia jina lake.

2) Pia alimtaka aeleze kama zinalipa kodi,

3) na kuhusu kuwa hana uhusiano na Kagoda aeleze alikuwa akienda benki kujadiliana juu ya akaunti ya Kagoda alikuwa akifanya hivyo kama nani.

4) Kuhusu Dowans aeleze mipango ya benki kuipatia Dowans fedha za mkopo aliokuwa na aliushughulikia kama nani, na uhusiano na Richmond anawafahamu vipi wahusika wake.

Kama ni kweli,

Naam, 40 hiyoooooo.. sasa hapo ndo penyewe, je Fisadi papa Rostamu atakubali kufa kibudu? ama itabidi aseme kweli tupu huyu mdudu KAGODA, na mayai yake yalienda wapi?
 
I see, am loving this war btn Fisadi Papas Vs Fisadi Nyangumi, tutajua mengi mwaka huu!
 
Mheshimiwa Spika, vilevile Mhe. Rostam Aziz alitakiwa atoe maelezo kuhusu uhusiano wake na Kampuni za Richmond Development Company LLC na Dowans Holdings S.A baada ya mashahidi kadhaa kudai kuwa ana uhusiano nazo. Aidha, alitakiwa na Kamati Teule aeleze kwa nini anwani ya barua pepe ya kampuni yake ya Caspian Construction Ltd ilitumiwa na Dowans. Kamati Teule ilitaka vilevile kupata ufafanuzi kutoka kwake kuhusu baadhi ya wafanyakazi wa kampuni yake wanaosemekana kuwa ni watumishi vilevile wa Dowans Holdings S.A.


Kwa hiyo Bunge linajua kuwa RA ana kampuni [angalau moja] yenye jina lake iliyoandikishwa kisheria BRELA kwa jina Caspian Contructions Ltd.

Au hapa Bunge lilipotoshwa bila ya kamati kuwa na facts [kwa maana kuwa Caspian Contructions Ltd siyo ya RA??

Au RA anajua kuwa Caspian Contructions Ltd haijaandikishwa kwa jina lake ndio maana anakataa kuwa hahusiki na Richmond wala Dowans??

Hapa UK kuna kitu kinaitwa Judicial Review, Tanzania kuna kitu kama hiki?
 
Rostam anajua anachofanya

Hata alipokuwa anakwenda Benki Kuu kuchota hela kwa Kagoda alijua alichokuwa akifanya ndo maana alihakikisha kuwa haachi alama yoyote ya kuja kumshika na kosa endapo watokea wanoko wakaibuka na hoja ya wizi wa hizo hela za EPA.

Kukosekana kwa saini zake kwenye mashirika yake na kuwaweka vibaraka wake kuwa signatories ni maelezo tosha kwamba RA hana mpango wa kufanya shighuli halali hapa Tanzania.

Kwaherini
 
Rostam anajua anachofanya

Hata alipokuwa anakwenda Benki Kuu kuchota hela kwa Kagoda alijua alichokuwa akifanya ndo maana alihakikisha kuwa haachi alama yoyote ya kuja kumshika na kosa endapo watokea wanoko wakaibuka na hoja ya wizi wa hizo hela za EPA.

Kukosekana kwa saini zake kwenye mashirika yake na kuwaweka vibaraka wake kuwa signatories ni maelezo tosha kwamba RA hana mpango wa kufanya shighuli halali hapa Tanzania.

Kwaherini

Tupo pamoja mkuu...nzi wanasema mke na watoto wanaishi dubai tangu mwaka jana!! Alama tosha ya mipango yake.
 
Tuwekee bandiko la kuonyesha Rostam ni shareholder wa Kagoda, au board member wa Kagoda au Dowans..
Acha porojo kaka!

Kwa taarifa ni kuwa Rostam hajaandikisha jina lake BRELA kwenye kampuni yake yoyote. Swali ni kwanini? Kodi analipaje?
 
Haya maswali ni msingi kabisa na wala sioni RA anaona tatizo gani kuyajibu tu.


4480d1241472479-mengi-kukutana-na-waandishi-wa-habari-rt.jpg
Maswali ya Mengi
 
Nilimsikia huyo wakili wa Mengi kwa mbaaaaaaaali akimtaka RA pia atolee maelezo kuhusu fungu la EPA lililoibwa likatumika kwenye uchaguzi 2005 na eti Mangula analijua hilo. Hapa ndio nikahisi kusisimka maana katriga kwa vidole kiunoni mwa CCM. Kwa hatua hii alofikia sifdhani kama Serikali ya JK itaendelea kufumbia maskio vita hii ya maneno kupitia vyombo vya habari iendelee.

Kweli baadhi ya wana wa CCM wanaoitwa machachari walionekana kumuunga mkono MENGI , lakini huko aendako tusishangae CCM ikimgeuka ghafla mara kuskia kanyamazishwa ukimya wa milele. Tukabaki kusema alikuwa... alikuwa....

Eeeh Mungu Mlinde mja wako Mengi atimize lile lilimjaa Moyoni.
 
inaonekana mengi alikuwa amejiaandaa ndio maana imemchukua siku 2 kujibu wakati rostam imechukua wiki moja yeye na sofia, mkuchika et al
 
Kwa hiyo Bunge linajua kuwa RA ana kampuni [angalau moja] yenye jina lake iliyoandikishwa kisheria BRELA kwa jina Caspian Contructions Ltd.

Au hapa Bunge lilipotoshwa bila ya kamati kuwa na facts [kwa maana kuwa Caspian Contructions Ltd siyo ya RA??

Au RA anajua kuwa Caspian Contructions Ltd haijaandikishwa kwa jina lake ndio maana anakataa kuwa hahusiki na Richmond wala Dowans??

Hapa UK kuna kitu kinaitwa Judicial Review, Tanzania kuna kitu kama hiki?

- Mkuu Yebo Yebo, Rostam alishazihamisha hizi mali kwa jina la Manji siku nyingi sana. Huyu Rostam hana huo ujanja ila ni sisi wabongo tunampa na umasikini wetu, mimi nilisema mapema sana hapa JF alipoanza kuzihamisha hizo mali, alinyamaza kimyaa baada tu ya kumaliza ndio akaanza ngebele!

FMES!
 
Wako wapi akina Mkuchika na Sophia Simba wamzodoe papa fisadi Rostam kama walivyomzodoa Mengi kwamba kakurupuka, kachemsha na watamchunguza kwa kutumia vyombo vyake vya habari vibaya? Kimya cha hawa watetezi wa mafisadi waliofichwa mifukoni mwa mapapa mafisadi kuhusiana na news conference ya papa fisadi Rostam ni ushahidi mwingine tosha kwamba Serikali imo mifukoni mwa mapapa mafisadi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom