William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
- Yaaani umezwe na papa kama serikali yetu halafu upone?
FMES!
FMES!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa mapenzi ya 'nyangumi' ni bora zaidi kwangu hasa nikikumbuka maneno ya biblia kuwa alimmeza Yohane na kumtapika baada ya siku tatu. Lakini sioni mahala kokote kwenye biblia au kwenye kashfa za mafisadi ambako PAPA anaweza kukula na kukutapika, akikumeza ndio imetoka, na sisi hapa hatukubali mpaka kieleweke. Narudia kwenye mpambano huu, namkubali zaidi 'Nyangumi' kuliko PAPA RA.
Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe 31 Disemba 2007 siku ilipowasilisha taarifa yake kwako, Kamati Teule ilikuwa imewahoji jumla ya mashahidi 75 na kuuliza maswali 2717 na kuzipitia nyaraka na kumbukumbu 104. Mashahidi 4 kati ya hao walikuja kwa hiari yao bila kupelekewa hati za kuitwa. Mashahidi 7 waliitwa mara mbili. Mashahidi wawili, Ndugu Daniel Yona na Mhe. Rostam Aziz, (Mb) walipelekewa hati za kuitwa mbele ya Kamati Teule lakini hawakufika kwa maelezo kwamba walikuwa nje ya nchi.
Mheshimiwa Spika, Ndugu Daniel Yona alitakiwa na Kamati Teule atoe maelezo kuhusu msingi wa uamuzi wake wa kuipa Richmond Development Company LLC, haki maalum ya kipekee (exclusive right) ya miezi 18 kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza mwaka 2004 wakati huo akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Maelezo ya ziada ya mradi huu nitayatoa baadaye.
Mheshimiwa Spika, vilevile Mhe. Rostam Aziz alitakiwa atoe maelezo kuhusu uhusiano wake na Kampuni za Richmond Development Company LLC na Dowans Holdings S.A baada ya mashahidi kadhaa kudai kuwa ana uhusiano nazo. Aidha, alitakiwa na Kamati Teule aeleze kwa nini anwani ya barua pepe ya kampuni yake ya Caspian Construction Ltd ilitumiwa na Dowans. Kamati Teule ilitaka vilevile kupata ufafanuzi kutoka kwake kuhusu baadhi ya wafanyakazi wa kampuni yake wanaosemekana kuwa ni watumishi vilevile wa Dowans Holdings S.A.
Kwani share zinauzwa kiasi gani? kama share moja ni shilingi 1000, share 300 zitakuwa ni kiasi cha shilingi laki 3 ambazo ni wastani wa kupanda mbegu DECI. Ukisema maskini Bongo hawanunui share, angalia wateja wakubwa wa DECI ni akina nani kama sio hao maskini unaowakandia kuwa hawawezi kuwekeza.
Mengi kupitia mwanasheria wake aitwaye Nguma atamfungulia mashitaa Rostam kujibu maswali manne,
1) ni kutaka kujua anafanya biashara gani nchini na ataje biashara hizo anazoziendesha na pia kama kampuni zake zimesajiliwa BRELA kwa kutumia jina lake.
2) Pia alimtaka aeleze kama zinalipa kodi,
3) na kuhusu kuwa hana uhusiano na Kagoda aeleze alikuwa akienda benki kujadiliana juu ya akaunti ya Kagoda alikuwa akifanya hivyo kama nani.
4) Kuhusu Dowans aeleze mipango ya benki kuipatia Dowans fedha za mkopo aliokuwa na aliushughulikia kama nani, na uhusiano na Richmond anawafahamu vipi wahusika wake.
Mheshimiwa Spika, vilevile Mhe. Rostam Aziz alitakiwa atoe maelezo kuhusu uhusiano wake na Kampuni za Richmond Development Company LLC na Dowans Holdings S.A baada ya mashahidi kadhaa kudai kuwa ana uhusiano nazo. Aidha, alitakiwa na Kamati Teule aeleze kwa nini anwani ya barua pepe ya kampuni yake ya Caspian Construction Ltd ilitumiwa na Dowans. Kamati Teule ilitaka vilevile kupata ufafanuzi kutoka kwake kuhusu baadhi ya wafanyakazi wa kampuni yake wanaosemekana kuwa ni watumishi vilevile wa Dowans Holdings S.A.
Rostam anajua anachofanya
Hata alipokuwa anakwenda Benki Kuu kuchota hela kwa Kagoda alijua alichokuwa akifanya ndo maana alihakikisha kuwa haachi alama yoyote ya kuja kumshika na kosa endapo watokea wanoko wakaibuka na hoja ya wizi wa hizo hela za EPA.
Kukosekana kwa saini zake kwenye mashirika yake na kuwaweka vibaraka wake kuwa signatories ni maelezo tosha kwamba RA hana mpango wa kufanya shighuli halali hapa Tanzania.
Kwaherini
Tuwekee bandiko la kuonyesha Rostam ni shareholder wa Kagoda, au board member wa Kagoda au Dowans..
Acha porojo kaka!
Maswali ya Mengi![]()
Kwa hiyo Bunge linajua kuwa RA ana kampuni [angalau moja] yenye jina lake iliyoandikishwa kisheria BRELA kwa jina Caspian Contructions Ltd.
Au hapa Bunge lilipotoshwa bila ya kamati kuwa na facts [kwa maana kuwa Caspian Contructions Ltd siyo ya RA??
Au RA anajua kuwa Caspian Contructions Ltd haijaandikishwa kwa jina lake ndio maana anakataa kuwa hahusiki na Richmond wala Dowans??
Hapa UK kuna kitu kinaitwa Judicial Review, Tanzania kuna kitu kama hiki?