Wanasheria wa Reginald Mengi wakutana na waandishi wa habari na Kumjibu Rostam Aziz

Wanasheria wa Reginald Mengi wakutana na waandishi wa habari na Kumjibu Rostam Aziz

Status
Not open for further replies.
Kwa nini Mengi alishindwa kuongea na waandishi wa habari?
Angesimama yeye mwenyewe kuliko kuwatumia hawa wapambe wake naona walichemka tu nilikuwa siwaelewi kabisa nikaamua kuzima TV.

Ndugu yetu Fidel80 sema tuu ukweli utasikika. Nadhani ukubali tuu kuwa majibu ya Akina Ngalo yapo makini, na hilo linapigia mtari kuwa RA bado ana hoja ya kujibu ili kumtoa katika nyaya za kuwa PAPA na kumleta kwa sijui vipapa au vitoto papa...lakini papa si papa tuu?
 
Inasikitisha
Hawa watu kama ingekuwa serikali ipo na inatimiza angalau 30% ya katiba ya nchi hawa walitakiwa wakamatwe watiwe lupango harafu uchunguzi ufanyike na mwisho mahakamani.

Mbona mimi nikimtuhumu kalima-nzira kaniibia kuku hapo hapo anafuatwa anapigwa mteke anapigwa pingu na kufikishwa mahakamani??
Mbona huwa hawasubiri wafanye uchunguzi ndio wamkamate kali-manzira ??

Jamani hawa si ndio huwa wanamtia kalima-nzira pingu na kumtia lockup na akiuliza kulikoni na akihoji ushaidi huwa wanamweleza yupo lockup kusaidia upelelezi ,sasa hawa kwanini wasitiwe kolokoloni kusaidia upelelezi?
 
Ukiamua kusema jambo lenye public interest ni sharti uwe umejiandaa , ufanye utafiti na kuhakikisha credibility ya hilo unalotaka kusema. RA alikurupuka akaongea vitu visivyokuwa na credibilty.

Mwenzake amecounter kwa data nasi ni mashahidi wake. Mwisho wa yote status ya RA kama Papa imebaki palepale. Tena this time mbaya zaidi maana mchezo ndio umekwisha . Hawezi tena kuita press conference

Sasa ndio muda muafaka wa vyombo vya serikali kuchukua nafasi yake. Nakumbuka waliwahi kusema mmiliki wa Kagoda hajulikani .......sasa ndio huyu hapa.

Kaeni kimya sasa muone 2010. A very interesting scenario. A boomerang has rebounced . uchiteme wala uchimumunye.
 
Kila uchao tunasonga mbele.

Naamini kila siku Watanzania kadhaa wanapukuta matongotongo machoni mwao na kuanza kuona ukweli halisi.

Si muda mrefu sana ujao Haki tulio ipoteza kwa miaka 48 kwa kuwaamini CCM itarudi mikononi mwetu.

Vita hii ya Kati ya Papa na Nyangumi ni ya moto kweli kweli sioni Tembo wala Simba wanaingilia.

Maji yanzidi kujenga mawimbi mazito kwa vishindo vya Sunami ya Ugomvi wao.

Ukiwa na ngozi nyeusi pengine kwa mara ya kwanza Duniani unaweza kuwa na Thamani nchini mwenu mahali Pengine ni Marekani tu, ambako mtu mweusi ameweza kupiga vikumbo watu hadi Ikulu.

Wenzetu rangi zao zinawaruhusu kwenda kuishi nchi nyingi sana Duniani bila kuonekana ni wazamiaji.

Rostam akiona maji yamezidi unga kiasi kwamba atapika uji mwepesi badla ya Ugali mgumu wa Usukumani kule kwa akina Chenge, huyoo ataanza huku kawaachia radhi akina Kikwete na Lowassa ambao kwao ni hapo TZ hata iweje.

Wengine tunaweza rudi leo hapo leo, kasheshe likizuka kiasi kwamba tuone mambo hayaendi, tunaweza amua tubambikwe lawama kibao na kurudi tena huku ughaibhuni kuliko kubaki hapo bongo tukila vumbi na fedheha.
Hata wapiganaji wa Mwituni si wote hukaa mwituni.

Hata hivyo sina Budi kuwashukuru akina Invisible na Majemadari wengine wa JF kwa kuwa ngangari na kuto kukubali kushindwa na kutuwekea jamvi hili ili nasi tulioko ughaibhuni tupate pa kutolea hewa ya ukaa.

Mtu kaajiri Watumishi wa serikali 6000 walioko kwenye kila idara nyeti ya serikali ili kila siku wamkingie kifua atunyeapo nyusoni mwetu, anadai kaajiri watanzanhia 6000 na anawalipa vizuri.
Ndiyo maana kuna watu hapa wanampa sifa MH RA na wako tayari kufa kwaajili yake kwa kukesha na kupiga yowe kwa bei ya mshiko.

Tangu lini kukopa kwa kufuta taratibu zote na kushindwa kulipa ni kosa la jinai??

Kwa wale wasijua Law 101 ukishindwa kulipa deni unakuwa na shitaka la Madai Mahakamani.
Ukitaka kesi ya madai iwe ya jinai sema mdai unatakiwa kusema ulipoenda kudai deni lako Mzee alikushikia Panga mama akaja na kamba ya kuni akitaka kukunyonga nayo shingoni na watoto wake walitishia kukung'ata ukijifanya kuleta zako.
hata hivyo bado deni lile haliwezi geuka jinai hata siku moja, ila kutakuwa na kesi ya jinai inayozaliwa lutoka na kesi ya madai.

Tangu lini kosa lisilo la jinai likakufanya uwe fisadi wakati Ufisadi ni mkusanyiko jalo wa Jinai za kukata kwa mundu??

Tungemtekenya zaidi, Rostam angefikia mahali angesema majina ya walioko kwenye Pay Roll yake ya siri.

Kibaya zaidi siku akiamua kuanza Ughaibhuni for Good, kwa unaa tu ataiweka list yake ya Pay Roll hadharani, kwa hiyo nyie mmpao sifa kama mungu wenu jiandaeni.

Kazi ya Ibilisi ni kuharibu na kuua tu, kwa kufanya hivyo utawala wake hudumishwa.
 
Last edited:
"Kuhusu uwekezaji wa NICO, Ngalo alidai kuwa si Mengi wala kamati ya uwekezaji ya NICO ilihusika kwa namna yoyote ili katika mchakato wa maamuzi ya kuwekeza kwenye kampuni ya Interchem kwa kuwa alipogundua hilo alijiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa kamati ya uwekezaji na ujumbe na alifanya hivyo kupitia barua aliyoiandikia NICO Agosti 3 mwaka 2007. Aliwataka wanahabari kwenda NICO kuthibitisha suala hilo."

Mwafrika. Angalia na ujifunze. Kusahishana badala ya vijembe visivyo na msingi.

I stand corrected, FMES. Mengi kama mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji asingeweza kumzuia Mwenyekiti wa bodi kupitisha mkataba ulioidhinishwa na bodi yake kwa hiyo ilikuwa hatua sahihi. Lakini swali linabaki kuwa yeye kama Mwenyekiti wa kamati ya uwekezaji, hakuwemo kwenye bodi? Yeye alijiuzulu kama Mwenyekiti, je, alibaki kuwa mjumbe wa kamati hiyo? Au nafasi nyingine ya uongozi katika NICO? Kwenda kuthibitisha kuwa alijiuzulu UENYEKITI hakutoshi.

Amandla.......
 
Kwa kweli mimi nakubali kabisa kwamba sisi ni waDanganyika.

Ati kwa kuwa Mh. Mengi amelipa hela za Import Support December 2008 na yeye alitakuwa kulipa miaka ya 90... in short amekaa na hela za wananchi for a decade/muongo mmoja hivi... ati sio fisadi nyangumi....

Sasa mbona wale wa EPA waliorudisha hela zetu within deadline ya Mh. Rais wamepelekwa mahakamani?

Hizo hela tulikuwa na makubaliano mengi akae nazo muda wote huo...

Wakati nakubaliana kwamba haikuwa lazima Mengi kupelekwa mahakamani kwa hilo deni la import support, lakini ukweli unabaki sio msafi, hana moral authority ya kuzungumzia mafisadi... aache vita ya ufisadi na JF.

Mkuu hapa issue si import support. Issue ni ufisadi? Haya mengine yaliyotokea ni kama kuongeza chumvi kwenye mboga. Maana Import Support haijulikani makubaliano yalikuwaje, hivyo tusichanganye mada maana hata RA alisema yeye na wengine wanaendelea kulipa sasa kipi bora Mengi aliyesema kamaliza au wanaoendelea kulipa tena baada ya serikali kuwakalia kooni?

EPA wamerudisha fedha lakini haiko wazi ni wakina nani, pia hela hizo zilikuwa za wizi sasa hiyo deadline unayosema ni ipi ya kurudisha mali ya wizi? WAKATI HILO NALO LILIKUWA KOSA? MTU KAIBA UNAMWAMBIA RUDISHA HELA UENDE ZAKO? BASI NA WAKINA MAHALU WARUDISHE WAENDE ZAO.

Inawezekana kana kuwa siyo msafi lakini alichosema kina impact fulani compared to wewe na mimi. Na pia wao kama waliona yeye ni fisadi walikuwa wapi siku zote hizo? Kwanini wasubiri sasa baada ya wao kuanikwa? Hapa hawa wanajaribu kujibu makombora hivyo tusidanganyike tujaribu kupima maneno haya siyo kuyachukulia kama yalivyo.
 
Inasikitisha
Hawa watu kama ingekuwa serikali ipo na inatimiza angalau 30% ya katiba ya nchi hawa walitakiwa wakamatwe watiwe lupango harafu uchunguzi ufanyike na mwisho mahakamani.

Mbona mimi nikimtuhumu kalima-nzira kaniibia kuku hapo hapo anafuatwa anapigwa mteke anapigwa pingu na kufikishwa mahakamani??
Mbona huwa hawasubiri wafanye uchunguzi ndio wamkamate kali-manzira ??

Jamani hawa si ndio huwa wanamtia kalima-nzira pingu na kumtia lockup na akiuliza kulikoni na akihoji ushaidi huwa wanamweleza yupo lockup kusaidia upelelezi ,sasa hawa kwanini wasitiwe kolokoloni kusaidia upelelezi?

Mkuu jamaa wameshindwa kabisa wanatuyumbisha tu hawa wanasheria wa Mengi kama wazalendo si wampleke mahakamani RA kuwa mwizi ameliibia taifa na ushahidi huu sio kuitisha wanahabari eti RA anafanya biashara gani?
Kama wanajua jamaa anafanya biashara flani si wangesema jamaa anapiga dili na CASPIAN amekwepa kodi hivi na hivi huku kavuta hiki na ushahidi huu . Kuliko kuanza kuleta vioja tu wameongea sasa wanasikilizia jamaa atajibu nini.
 
hehehe
leo bluu itakuwa bluu na zambarau itaitwa zambarau
true colours emerge.
Tusubiri press nyingine ya RA baada ya kiukao kingine cha dharura cha CC
 
Lakini swali linabaki kuwa yeye kama Mwenyekiti wa kamati ya uwekezaji, hakuwemo kwenye bodi? Yeye alijiuzulu kama Mwenyekiti, je, alibaki kuwa mjumbe wa kamati hiyo? Au nafasi nyingine ya uongozi katika NICO? Kwenda kuthibitisha kuwa alijiuzulu UENYEKITI hakutoshi.

Amandla.......

FM,

Kufuatana na barua ya resignation iliyosomwa na wakili wake, Mengi alijiuzulu UENYEKITI NA UJUMBE wa kamati ile........!

Ukienda NICO, sio eti ukathibitishe kujiuzulu uenyekiti tu, basi ukadadisi na maswali mengine pia uliyo nayo kuhusu Mengi vs NICO!
 
Kibaya zaidi siku akiamua kuanza Ughaibhuni for Good kwa unaa tu ataiweka list yake ya Pay Roll hadharani, kwa hiyo nyie mmpao sifa kama mungu wenu jiandani.

Na hii ndio tabia halisi ya Wahindi na hiyo type ya RA.

Wakishabanwa banwa lazima wakikoshe na hapo ndipo atakapoiweka pay roll hadharani akisema " Ninyi niliwafadhili na sasa mmenisaliti " why JK , why Sophia Simba , Why Mkuchika , Why makamba etc tec...That time is just around the coner.
 
FM,

Kufuatana na barua ya resignation iliyosomwa na wakili wake, Mengi alijiuzulu UENYEKITI NA UJUMBE wa kamati ile........!

Ukienda NICO, sio eti ukathibitishe kujiuzulu uenyekiti tu, basi ukadadisi na maswali mengine pia uliyo nayo kuhusu Mengi vs NICO!

- Saaafi sana mkuu, tupo pamoja hapa, dawa ni kwenda NICO badala ya speculations zisizokwisha.

FMES!
 
Mkuu jamaa wameshindwa kabisa wanatuyumbisha tu hawa wanasheria wa Mengi kama wazalendo si wampleke mahakamani RA kuwa mwizi ameliibia taifa na ushahidi huu sio kuitisha wanahabari eti RA anafanya biashara gani?
Kama wanajua jamaa anafanya biashara flani si wangesema jamaa anapiga dili na CASPIAN amekwepa kodi hivi na hivi huku kavuta hiki na ushahidi huu . Kuliko kuanza kuleta vioja tu wameongea sasa wanasikilizia jamaa atajibu nini.

Mambo haya yakienda Mahakamani yanapigwa kufuri zito na Walioko kwenye Pay Roll ya Rostamu wanachukua nafasi zao na kuua so.

Bila hata kusita Mkurugenzi wa Mashitaka na Mkurugenzi wa Takukurukakara wote wamo kwenye Pay list ya Rostam Aziz.

Kwa mwendo wa nchi yetu Ulivyo sasa kwamba Sheria ni Mahoka Vitabuni tu ni vema tusikilize hoja za Papa na Nyangumi kupitia mahakam ya wazi.

Toka watu wazito waanze kufikishwa Mhakamani ni Mzee Mlingwa tu ndiye aliyefungwa jela kama mbuzi wa kuondoa dhambi za CCM wengine wanapeta wakisubiri siku ya kurudisha namba au siku Watanzania wakigeuka Nyati wa Mikumi.
 
FM,

Kufuatana na barua ya resignation iliyosomwa na wakili wake, Mengi alijiuzulu UENYEKITI NA UJUMBE wa kamati ile........!

Ukienda NICO, sio eti ukathibitishe kujiuzulu uenyekiti tu, basi ukadadisi na maswali mengine pia uliyo nayo kuhusu Mengi vs NICO!

Thanks but no thanks. Niende NICO kufanya nini? Mimi nitaendelea kusoma na kuchambua hayo tunayoletewa na wahusika wenyewe.

Amndla............
 
- Saaafi sana mkuu, tupo pamoja hapa, dawa ni kwenda NICO badala ya speculations zisizokwisha.

FMES!

Sio NICO peke yake. Bali kufuatilia hata hiyo InterChem! Hapa wote tuna speculate unless Mengi na Rostam wako miongoni mwetu!

Amandla.........
 
"Kuhusu uwekezaji wa NICO, Ngalo alidai kuwa si Mengi wala kamati ya uwekezaji ya NICO ilihusika kwa namna yoyote ili katika mchakato wa maamuzi ya kuwekeza kwenye kampuni ya Interchem kwa kuwa alipogundua hilo alijiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa kamati ya uwekezaji na ujumbe na alifanya hivyo kupitia barua aliyoiandikia NICO Agosti 3 mwaka 2007. Aliwataka wanahabari kwenda NICO kuthibitisha suala hilo."

- Wahusika wamesema haya juu, au?

FMES!
 
Mwafrika. Angalia na ujifunze. Kusahishana badala ya vijembe visivyo na msingi.

I stand corrected, FMES. Mengi kama mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji asingeweza kumzuia Mwenyekiti wa bodi kupitisha mkataba ulioidhinishwa na bodi yake kwa hiyo ilikuwa hatua sahihi. Lakini swali linabaki kuwa yeye kama Mwenyekiti wa kamati ya uwekezaji, hakuwemo kwenye bodi? Yeye alijiuzulu kama Mwenyekiti, je, alibaki kuwa mjumbe wa kamati hiyo? Au nafasi nyingine ya uongozi katika NICO? Kwenda kuthibitisha kuwa alijiuzulu UENYEKITI hakutoshi.

Amandla.......

Hata Lowasa alipogunduwa Richmond ilikuwa na utapeli Alijiuzulu teh teh teh teh
Kwahiyo Lowasa ni msafi na msimguse kabisaa
 
fm,

kufuatana na barua ya resignation iliyosomwa na wakili wake, mengi alijiuzulu uenyekiti na ujumbe wa kamati ile........!

Ukienda nico, sio eti ukathibitishe kujiuzulu uenyekiti tu, basi ukadadisi na maswali mengine pia uliyo nayo kuhusu mengi vs nico!

je mengi ni board member wa nico?
 
Tuhuma ambazo hazikujibiwa na Mengi ambazo zilitolewa na Rostam ni kuhusu kuwa na akaunti ya fedha za kigeni nje ya nchi, malipo kwa wafanyakazi wake, kuhusu kuwa na ugomvi na baadhi ya viongozi na kutaka matatizo hayo yawe ya kitaifa na tuhuma nyinginezo.

Kashehe, tuhuma hizi mbona ni shallow sana ku justify ufisadi wa Mengi!! Kuwa na akaunti nje ya nchi sio kosa kabisa ila Rostam angetoa ushahidi kuwa fedha zilizopo kwenye hiyo akaunti zilipatikana kifisadi sio blabla tu.

Malipo ya wafanya kazi wake ni makubaliano kati ya mwajiri na mwajiriwa unless anawalipa chini ya kima cha chini cha mishahara kilichowekwa na RA or sorry! (soma serikali)

Ugomvi na baadhi ya viongozi kumbe nao ni ufisadi?! hili sikulijua
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom