Wanasheria Waelimisheni Viongozi Wetu Kitu Kinachoitwa "Vicarious Liability", Hata Kama Wewe Hujaua, Kama Muuaji ni Mtu Wako, Then Unawajibika Wewe

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi
Nimejitolea kuwa mwalimu wa kujitolea wa somo la katiba, sheria na haki, ili kuwaelimisha Watanzania kuhusu haki zao na wajibu wao.

Kujitolea kuwa mwalimu somo la katiba, na sheria, nimehamasishwa na yeye mwenyewe Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au? hebu msikilize mwenyewe akizungumza
View: https://youtu.be/PZ_8JFw_5LM?si=LqdibxLmRJXzlhQY ni kufuatia hoja hii, ndipo mimi nikajitolea Kipindi cha TV, Kutoa Elimu ya Katiba, Sheria na Haki, Kuanza Jumapili Hii Kupita Channel Ten
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=LdYf8WVJTIKw8KCu
Somo la leo ni somo la kitu kinachoitwa vicarious liability. Haya ni mahusiano ya uwajibikaji wa kisheria yanayoitwa fiduciary relationship, yaani uhusiano wa uwajibikaji Kama mke na mume, mzazi na mtoto, daktari na mgonjwa, mwalimu na mwanafunzi, wakili na mteja wake.

Hii fiduciary relationship inampa uwajibikaji wa kisheria wahusika hao, ikiwemo mzazi kuhukumiwa kwa makosa ya mtoto wake wa umri wa chini ya miaka 14.

Kinga hii pia inahusu kutotoa ushahidi dhidi ya mtu huyo, mfano mke akijua mumewe ni jambazi, na ni muuaji, anaweza kusema kuwa anajua mumewe ni jambazi na muuaji ila ana kinga ya fiduciary kutowajibika kutoa ushahidi dhidi ya mumewe. Vivyo hivyo kwa sisi mawakili, unaweza ukawa ni wakili wa muuaji, akakiri ameua kwa 1st degree murder, wewe japo ukweli unaujua, utamshauri akanushe na utamtetea hadi hiyo murder case inageuka manslaughter.

Sasa kuna mauaji mengi yanayotokea na kuwahusisha watu wasiojulikana, kiukweli sio wasiojulikana wote ni wasiojulikana kweli, kuna baadhi ya mauaji yanafanywa na watu "wasiojulikana" kumbe kiukweli watu hao sio "wasiojulikana" bali ni 'wasiojulikana'.

Ili kuwatambua "wasiojulikana" na 'wasiojulikana' tembelea Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana

Hivyo vitendo vyovyote vinavyofanywa na 'wasiojulikana' kwa kujifanya ni "wasiojulikana", then anayewatuma ana wajibika nao vicariously.

Hoja hii ni kufuatia hoja hii humu jf
Rais Samia amesema anasikitishwa baada ya kusikia mwenyekiti (yeye) anavyoshambuliwa na kusema ukweli wanaujua hivyo wasimame imara, kujibu hoja hizo.

hajawai kuua mtu, labda sisimizi ndio amewahi kuua.
Naunga mkono hoja, mtu mwenye wajihi kama huu, Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” hawezi hata kuua panya!, kama ni kuua labda mbu, mende na sisimizi.

Ila kwa vile yuko serikalini na yeye ndie mkuu wa serikali, na anajua kuna mazingira fulani, serikali zote duniani huwa zina waua watu hatarishi kwa usalama wa nchi, dissidents, na kabla hawa dissidents hawajauliwa lazima CinC asaini ile death warrant, then death warrant yoyote ikisainiwa, aliyeua ni aliyesaini death warrant na sio wale watekelezaji.

Ikitokea makosa ya watu wake kumuua kwa makosa mtu safi kwa kudhaniwa ni dissident, then the blood of that person is upon aliyetoa hiyo order kwa niaba yake.

Na kunapotokea vifo ambavyo vingezuilika kwa kufanya kitu lakini hakikufanyika, then damu iliyomwagika is upon yule ambaye angezuia lakini hakuzuia.

Hivyo tumeshauri Kama Walioua ni "Wasiojulikana" Then Karma, Albadir Itawahusu, ila kama ni 'Wasiojulikana', Hata Albadir Haisaidii Kitu, Wametimiza Tuu Wajibu Wao!

Hata yale matukio ya utekaji, utesaji na mauaji enzi za kipindi kilee... watu humu tulishauri TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe! hao majamaa wali mute kimya, wakijua hawawezi kufanywa lolote, lakini mwisho wa siku aliyewajibishwa na top boss wao!.

Hivyo ni muhimu sana kwa viongozi wetu kuijua hii vicarious liability kwa vifo vyovyote vya kizembe vinavyotokea chini ya mamlaka yao, na matukio yote ya utekaji, utesaji na watu kuuliwa au kupotezwa, hata kama wahusika hawatafutwa, serikali inajifanya kusema itafanya uchunguzi, kumbe ni uongo tuu kwasababu kila kitu wanakijua kwasababu hao watu wanaotenda vitendo hivyo ni watu wao!, hivyo hawatapatikana, hawatashitakiwa popote, na hawata wajibishwa kwa vitendo vyao viovu, lakini hukumu karma ambayo ndio hukumu ya haki hapa duniani, inakuwa ii juu yao!, anayewajibishwa mwisho, sio wale watendaji, wale walikuwa ni watekelezaji tuu, lakini anayewajibika, vicariously ni yule mwenye dhamana. The Power of Karma- Ndio hukumu pekee ya haki kamili hapa Duniani. Unahukumiwa kwa matendo yako! .

Baada ya kifo cha Mzee Kibao, watu wakaanza kupiga ramli, tumewashauri watu waache kupiga ramli chonganishi Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani!

Kanuni yenyewe ya vicarious liability ni hii
"Vicarious liability exists due to the legal doctrine of respondeat superior, which essentially means “let the master answer.” Employers, parents or others with a superior legal relationship to someone who does harm are expected to answer for those who are under their control.

Vicarious liability rules also exist in order to provide protection to victims of injury. Often, an individual employee or a child will not have the resources to provide compensation to those they harm through their negligence or wrongful actions. But companies and parents generally do.

Through the doctrine of vicarious liability, those who have resources (including the ability to buy insurance) and who were in a position to prevent harm but who failed to do so can be held accountable so victims do not go uncompensated"

Tanzania tuna bahati nzuri sana hatuna wanasheria aggressive wa kutetea watu, vinginevyo tungetumia private investigations kuwabaini hawa 'wasiojulikana' na kuwatundika msalabani, hii ingewafanya viongozi wetu kuwa more responsible for the life of its citizens.

Paskali

Update
Hii ni michango very objective
Hiyo Vicarious Liability mpaka iwepo ni lazima uwepo ushahidi wa kutosha kwamba wauaji wametumwa na mamlaka ya Rais.
Mkuu Steve, Steven Joel Ntamusano, vicarious liability, haihusu kiongozi kuhusika direct au kumtuma, kiongozi anahusika vicariously kama baba anavyo wajibika kwa makosa ya mwanae hata kama hajamtuma!
Waliuliwa wengi kule MKIRU na wengine miili ikawa inaokotwa Coco Beach sikuwahi kuisikia hiyo liability ikiwa kazini kwa maana ya Hayati JPM kubebeshwa mzigo wa hayo mauaji.
Ni bahati Bongo hatuna mawakili aggressive kutetea haki za watu wanyonge masikini wa kutupwa ambao wanauawa kwa makosa na serikali. Kuna vifo vingi serikali zimehusika, lakini watu hao hawana uwezo wa kuajiri mawakili na wengi wa mawakili wetu ni after money, hakuna mawakili wa kutosha wa pro borno kufungua mashitaka hayo kwa kujitolea matokeo yake ni kuiachia tuu karma, na kweli karma inawashughulikia viongozi wetu kikamilifu na matokeo yake ndio kama vile...

Tatizo la karma, inapokushughulikia haikuambii kosa lako!.

Lakini alipouliwa Imran Kombe, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TISS, familia yake ilifungua shauri la vicarious liability na familia walilipwa fidia ya zaidi ya shilingi milioni 300!.
Vyombo vya upelelezi vipo siku zote na ni jukumu lao, kuanza kumhusisha moja kwa moja Rais na murder cases za raia wake kisa masuala ya kisiasa ni uoga na wasiwasi wetu ambao siku hizi unaendelea kuwa mkubwa zaidi.
Hakuna mtu yoyote amemuhusisha rais na mauaji, ninachofanya hapa ni kufundisha somo la kuwajibika, watendaji wote wa serikali, kila wanàlofanya, wanalotenda, wanalosema, ni wanafanya kwa niaba ya rais wa JMT, hivyo muwajibikaji wa mwisho anayewajibika na uhai wa raia wake, ni rais wetu, ikitokea waserekili wamefanya madudu ya ajabua ajabu, rais, anapaswa kuwawajibisha, na wasipowajibishwa, ni rais ndio anakuja kuwajibishwa yeye na karma kwa makosa ya watendaji wake!.

Kwa vile si wengi wanaijua karma, ndio maana tunawashauri wateule wake wawajibike kikamilifu kumuepushia adhabu ya karma kwa bosi wao Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karma
Na Utamaduni Viongozi Kuwajibika umeishia wapi?, Mbona Mwinyi, mauaji Mwanza aliwajibika?. Tusiruhusu madoa haya ya damu kuichafua nchi yetu -Wajibikeni!
P
 
Sawa

Mkapa: Najutia madhara yaliyowakuta Wanachama wa CUF wengine wakakimbilia Shimoni Mombasa

Magufuli: Sijawahi kusaini Hati ya Hukumu ya Kifo hata Moja, Uhai tumepewa na Mungu

Mh Rais Samia: Sijawahi kuua labda sisimizi

Prof Kindiki: Mimi natimiza majukumu yaliyomo kwenye Katiba kama Polisi wameuwa kila Mtu atabeba Msalaba wake mwenyewe

Kiroho haya mambo ni mapana sana
 
shida viongozi wetu neno accountability wanajua linatumika tu kwa watu wa chini yao. Sababu ni kwamba kuna kiongozi yuko yuko juu ya katiba.
Accountability kwa serikal zetu za kimatumbi halipo. Limebaki kwenye vitabu vya sheria lakini utekelezaji 0
Mahali utapoona wanalipigia kelele ni kwa watumishi wa chini ila wao wenyewe ahh
 
Huu ndiyo uandishi wa Pascal ninayemjua. Ulikuwa kama unamsubiri aongee ile utoe lecture. Asante Mwamba. Duniani tunapita.
 
Sijui SSH kapatwa na nini. Mambo yanayofanyika wakati huu hayaingii akilini kabisa.

Hii miaka minne aliyopewa na Mungu kuliongoza taifa hili angeweza kuacha legacy ya uhuru kamili! Vizazi na vizazi vingemshukuru na kumkumbuka daima.

Lakini yeye ameamua kuitumia kusaka mitano tena kwa njia yoyote ile. What a waste!
 
mm tangu ile hotuba yake aliosema kuna watu.wamekaa kikako na walioyaongea nayajua,nikajua huyu mama kuna vijana wanamdanganya kwa makusudi kua kuna maadui wa kuwashugulikia. hivi kina mbowe hawa wa miaka nenda rudi wana lipi jipya la kuisumbua tanzania yetu!!

anatakiwa aogope ccm wenzio kama watathubutu kuka vikao vya siri lakini hakuna mpinzani kwasasa mwenye makucha wa kuleta shida kwa yeyote.
 
Ngumu sana kuelewa watawala wa Taifa hili,ambalo wapumbavu ndo wako kwenye ngazi za maamuzi/kimaamuzi na wenye akili timamu kuwa wafuasi.

Kuna mambo ukisikia kiongozi anaongea, unaona kabisa Kuna shida ya kuandaa viongozi kwenye nafasi kubwa.
 
Huyu kiongozi ana akili za kuelewa? Unabaki kushangaa inakuwaje unakuwa kiongozi hata unashindwa kuelewa vitu vidogo kama hivyo. Kwamba eti alitegemea yeye awe ameshika bunduki na kuua
Nadhani hapa mama yetu amechochoa! Bila shaka haelewi ile dhana halisi ya uwajibikaji akiwa kama Mkuu wa nchi.
 
Viongozi wetu wengi hawana uwezo,karama wala mafunzo/maandalizi.
Ni upepo,makelele,ulozi na ujinga wa wananchi ndiyo huwafikisha kwenye viti walivyokalia!
Hawawezi kutupa matokeo mazuri/makubwa maana si nafasi walizostahili kuwepo hatakidogo.
Tizama uingereza wanabadili/ondoa viongozi(waziri mkuu) kwa makosa ya kawaida LAKINI hukukwetu sisi sijui tunalaana gani...
Mauaji,
utekaji,
uteswaji watu,
kufunga jela watu hovyo,
kutisha wananchi,
kusigina katiba,
ufisadi,
kunyimwa kusema/kukutana,
kukiri kuiba kura,
unyang'anyi,
kufukuza wanakijiji makwao,
kukopakopa vibaya ukisema unafukuzwa,
mihimili kuingiliwa na kuburuzwa,
kuuzwa rasilinali nyeti nk. nk.
Nabado majinga yanagaragara mavumbini na kuimba eti unapigwa mwingi.....phtuuu mpaka!!!!
 
Nakiri kusoma Uzi wa mkuu Pascal Mayalla akielezea dhana ya Uongozi kuwajibika kwa mema na mabaya
Mkuu Yohana Mbatizaji, johnthebaddest , next time ukijibu hoja kwa bandiko jipya, weka na link ya bandiko la mtoa hoja.
Kwamba nani anauwa ni swala Pana sana ndipo Yesu Kristo alisema " Baba Uwasamehe hawajui walitendalo"
Ni kwenye kabisa, hata sisi Wakatoliki siku zote tunasisitizwa kusamehe, Mungu wetu ni Mungu Mwema, Mwenye upendo, mwenye huruma na kusamehe dhambi na makosa yote, ila dhambi ya umwagwaji damu ya watu wasio na hatia, hainaga msamaha, ni lazima ifidiwe kwa damu!. Kuna majitu majinga yamemzunguka, yanamwaga damu zisizo na hatia, na kumdanganya kuwa walitaka kufanya uhaini ndio tumewafanya vile!. Akiukubali uongo huo, hizo damu zinakuja kuwa juu yake na mwisho wa siku anayekuja kuhukumiwa, sio wale wamwaga damu, bali yeye aliyeruhusu damu hizo kumwagika!.
sisi watu wa ushauri wa bure tuneshauri
Ikumbukwe pia hata yule mnyongaji wa Magereza kuna taratibu fulani huwa anazifanyia kabla na baada ya kumnyonga Mtu Kiroho na Kisheria
Hili nimelisemea vizuri kabisa, kuna watu kuua kwao ni duty ya kutimiza wajibu wao, hivyo wanaua na kumwaga damu za wenye hatia kwa kutekeleza wajibu wao, ila pia zipo damu za wasio na hatia, zinamwagwa kwa makosa bila hatia, damu hizi zisizo hatia zinazomwagika, sio juu yao hao wamwagaji bali ni juu ya mamlaka yao ya aliyewatuma!. Kama Walioua ni "Wasiojulikana" Then Karma, Albadir Itawahusu, ila kama ni 'Wasiojulikana', Hata Albadir Haisaidii Kitu, Wametimiza Tuu Wajibu Wao!
Kwamba anayeua ni Mkuu wa Nchi haiko hivyo duniani labda pale anapouwa yeye mwenyewe kama Iddi Amin alivyofanya
sijasema anayeua ni Mkuu wa Nchi, kumaanisha ni yeye na pull the trigger nimesema damu za wasio na hatia zinazomwagika, ni upon mamlaka ya juu yenye wajibu wa kuzuia but it does nothing!.

No one knows for sure kwanini yule Blaza aliitwa mapema vile!, ila sisi waumini wa karma tunajua ni karma!, hivyo tunapoona vitendo viovu vya kumsabishia a bad karma tuna wajibu wa kumsaidia. Tumeisha shauri sana
Sasa niko tayari kwa Mjadala nikianza na swali, Je Pilato ndiye aliyemuua Yesu Kristo?

Vijana msilale 🐼
Sio Pilato aliyemuua Yesu Kristo, ameuliwa na wauaji waliokuwa wanatimiza tuu wajibu wao, hivyo wauaji wale hawana hatia ya kifo cha Yesu, ila ni Pilato ndie aliyemhukumu kifo cha msalabani, japo Pilato alinawa kuondoa hatia ya hukumu hiyo, kunawa kule ni kujikosha tuu lakini hatia ya kifo cha Bwana wetu Yesu Kristo ii juu ya Ponsio Pilato, ila justification yake ni tumemuua sisi kwa dhambi zetu na ni kwa kupigwa kwake sisi tumeponywa.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…