Kumekuwa na unyanyasaji sana kwa watoto wetu wanaochukuliwa kwenye Ofisi za Serikali kwa ajili ya mafunzo ya kazi (internship programs).
Ukienda sekata binafsi kuna nafuu kubwa sana sana hasa kwa waajiri wale wa uhakika. Vijana wanaochukuliwa Serikalini hata wanaotokea Taesa hawana chochote cha kujifunza zaidi ya kufananishwa na wale waliopo field (yaan mafunzo ya bvitendo wakiwa masomoni bado).
Ukipitia maandiko mbalimbali ya HR utagundua kuwa internship ina tofauti ndogo sana na on-job training (mafunzo kazini).
Lakini mafunzo ya field yana tofauti kubwa sana na intesnhip na on-the-job training. Kwa internship ni fani ya madakatari tu na zamani wanasheria ndiyo walikuwa wakitendewa haki. Hawa walilipwa karibu sana na waajiriwa wapya na mishahara yao haikukatwa kodi.
Waliruhusuiwa kutekeleza ila wajibu na hata ilipostahili wasafiri kikazi walisafiri na kulipwa kama Maafisa wa chini. Siku hizi internship imefanywa kama favour - mtu nia Mwanasheria anaenda kupewa kazi ya kukusanya kodi kwa wafanyabiashara waliopo manispaa. Mtu ni HR eti anapewa kazi ya procurement au mpokezi (yaani receptionist). Mbali ya hayo inapotokea maslahi yeyote huyu mtu wa internship hapewi kamwe.
Kuna taasisi baadhi za Serikali hutoa stahiki mbalimbali kwa watumishi wao baadhi inapofikia wakati wa kuwapatia stahiki hizo vijana wa internship hupuuzwa na kuachwa wasubiri nauli zao toka Taesa.
Discrimination ya namna hii ni ya wazi kabisa kabisa - na inazuiwa katika Sheria yetu ya Ajira na Mahusiano Kazini. Kwa kuwa watendaji kama akina Katibu Mkuu Dr. Ndumbaro na wengine wanajifanya hawalijui hili ni vema wanasiasa ambao ni watawala wetu mlisemee hili kwa nguvu zote mkiwa huko Bungeni. Tafadhali toeni mwongozo ili internship isiwe na elements za ubaguzi.