Tatizo kubwa hatuna chama mbadala chenye Sera na itikadi madhubuti kwa manufaa ya umma. Badala yake tuna vyama vya upinzani vinavyomilikiwa na watu kwa maslahi yao binafsi. Chadema inamilikiwa na Mbowe, ACT inamilikiwa na Zito, CUF inamilikiwa na Lipumba, NCCR inamilikiwa na Mbatia n.k.
Na vijana wao kama wao HAWANA Agenda wala hawajiangalii kama wao.
Wamebaki kuwa Misukule wa Vyama vya siasa, na wasanii, viongozi wa dini.
Hulazimiki kutekeleza mahitaji ya vijana wengi ambao ni wafuasi wa Gwajima wakati ukimpa mtu mmoja tu, Gwajima anachotaka tayari umekamata wafuasi wake wote.
Mfumo huu huu uko kwa wanasiasa, na wasanii.
Vijana wote hawana Agenda wala mahitaji ya pamoja, zaidi ya kuwa misukule ya Agenda binafsi za wanasiasa ambazo mara nyingi hazigusi maslahi ya vijana.
Mfano: Sasa hivi vijana wengi NJAA KALII wanaishi kwa umachinga, lakini kipaumbele cha wanaharakati na wanasiasa mbele ya hii njaa kali ni Tume huru ya uchaguzi na katiba mpya.
Na vijana wanakuwa pushed kuwa nyuma ya Agenda hizi ambazo hazina manufaa kwao ya moja kwa moja.
Wale ambao ni misukule wa Diamond, kazi yao ni kuwa nyuma yake kwa agenda yenye maslahi yake binafsi. Sasa hapo mwanasiasa akishampata yeye ameshapata genge lake lote.