DOKEZO Wanasiasa na mipango ovu ya kuiua eGA

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Huu uzi ni mzuri sana kufahamisha watanzania kinachoendelea,cha ajabu TISS wanakenua tu meno,
Lingine,. hapa jukwaani wamejaa chawa wa hao wanataka kuua huo mfumo,ndio maana uzi wako hauna wachangiaji,
 
kwakweli kama kuna kitu cha manufaa kwa nchi yetu na kiuna wajanja wanataka kuingilia kati kuvuruga, wananchi tunatakiwa kuingilia kati chapi kuikumbusha serikali isidanganywe. shida ni pale ambao hatuaminiani, unakuta hata aliyeleta hii mada huyo wa EGA naye anafaidika nao sasa anaona tonge linataka kunyang'anywa. sijui tumwamini nani sasa. endeleeni kutupatia elimu.
 
Yes RAIS ni taasisi kubwa ana jua ndio maana hata sisi tunasema hapa , lakini haimaanishi ana endorse hio move.
wanasiasa waovu wanapambana kutaka kumruka asijue ujanja wao , lakini bahati nzuri kamba yao imejulikana
Mkuu kwa mkataba wa pesa ndefu kama hiyo rais lazima ajue. Haiwezi kulipwa bila rais kujua na mkataba hausaini bila rais kujua . Inshort na yeye yumo, anajua.
 
Mtakapo sikia jogoo akilia mara tatu kila mtu ndipo atakapo Kiri kweli alikuwa kiumbe toka sayari ya Mars.
 
Kwa ujuzi wangu na navyowajua Ega hawana uwezo wa kutengeneza mifumo waliyonunua TRA wala TANESCO hata asilimia 10. Ile ni mifumo mikubwa inayotumika Duniani.

Ega ukiangalia tu website za serikali unaweza kujua ni watu wa uwezo gani halafu wapewe kutengeneza mifumo mikubwa kama ya TRA ama TANESCO kweli?

Sio kila kitu lazima kifanywe na wataalamu wetu wakuu. Vitu vingine viko juu ya wataalamu wetu.
 
Baada ya shule ya huruma, leo EGov
 
E-GA kumbukumbu zangu zinaniambia ni ya mkurugenzi wa tcra,class mate wangu
 
Huu uzi ni mzuri sana kufahamisha watanzania kinachoendelea,cha ajabu TISS wanakenua tu meno,
Lingine hapa jukwaani wamejaa chawa wa hao wanataka kuua huo mfumo,ndio maana uzi wako hauna wachangiaji,
Hivi unayajua majukumu ya TISS?..unadhani TISS ni polisi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…