Wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa hujiona spesho sana!

Weakman

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2021
Posts
995
Reaction score
1,607
Serikali yoyote duniani Ina kitengo cha uuaji!

Kitengo rasmi Cha kuwashughulikia wahuni, wenye kuhatarisha usalama wa raia, amani ya Nchi, au wenye kuhatarisha mustakabali na utulivu wa serikali inayotawala!

Leo hii tunaona serikali inavyowashughulikia raia wake kwa kututanabaisha kuwa wao ni panya road! Na Jamii inafurahi! Na tutake tusitake, wapo wanaouawa humu si panya road! Haya Ni mauaji ya serikali, na damu hii inabebwa na mtawala husika!

Huo ni mfano tu wa mauaji yaliyo wazi na halisi, yapo yaliyo gizani pia! Serikali yoyote humwaga damu za raia wake!

Point yangu ni nini?

Point yangu Ni kuwakumbusha wanasiasa wasijione spesho kuliko wengine! Kama serikali imeweka idara za kuua raia, basi wawe tayari kushughulikiwa Kama wamebainika kuwa hatari kwa amani na usalama wa Nchi, au wanadhalilisha serikali yao. Ni kosa la kiusalama kudhalilisha serikali!

Leo hii tunaona ni sahihi kuua panya road, lakini uchunguzi wa kipolisi ungebaini kuwa mwanasiasa Fulani, au mfanya biashara mkubwa anafadhili genge la panya road ili kuharibu taswira ya Nchi, basi hapo tungelalamika Sana iwapo mwanasiasa huyo angeuawa!

Wanasiasa wajue hawana thamani yoyote mbele ya Mungu ya kuwazidi raia wengine. Nanyi munastahili kuuawa Kama raia wengine! Kama hamustahili Basi na raia wengine wasiuawe pia!

Leo hii kelele ni nyingi za kumsema JPM Ni muuaji. Ukiuliza amemuua nani? Unatajiwa Ben saanane, Azori, na risasi za Lisu. Hawa Ni wanasiasa. Mauaji kule kibiti hayatajwi, kwasababu tu hakuna mwanasiasa aliyekufa.

Kama Ben saanane ameuawa bila hatia, dhambi yake Ni sawasawa na "panyaroad" aliyeuawa bila hatia!
Kama Lisu alipigwa risasi bila hatia, dhambi yake ni ileile ya kumpiga risasi "panyaroad" asiye na hatia!

Tutulie, tuendelee kushuhudia mauaji ya raia kwa raia, Serikali kwa raia!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mada za mauaji zimekua nyingi sana.

Watanzania wote tunahaki sawa bila kujali cheo au mali.

Chukua hatua binafsi na epukana na yale yatakayo kupelekea katika hali ya kupoteza uhai wako kwa mtutu.
 
Huna point wewe unajambajamba tu hapa. Usihalalishe uovu kwa jinsi hisia zako zinavyokutuma. Nchi zote zinaongozwa na Katiba, tuwekee Ibara au kifungu kinacho sapoti hizo pumba zako ulizoandika hapo juu.
 
Kweli wewe ni weakman, Unaongea pumba tu, sidhani kama una uwezo wa kufikiri wa kutosha.
 
Kwahiyo watanzania wote, bila kujali tofauti zetu za kipato, dini, kabila wala umaarufu tujumuike pamoja KUUAWA BILA KILULALAMIKA. (Hata kama tunauawa bila hatia). Si ndio umemaanisha hivyo ndugu mtaalam ?
 
We jmaa akili inakuruka sasa waliokaribu wakushikilie vizuri😀🤣

yaan haya mawazo ulibidi uishie kuwaza kwene kichwa chako c kuleta pumba hapa😀😀Ukiamua kuandika jiulize hiki kitu kinamaana au maslahi kwa jamii!!
 
Sio serikali zote,
Ni serikali za Afrika.
 
KOSOVU KWENE ANDIKO
1.Hukufaa uanzishe uzi we unafaa uwe unakoment kwa walioandika uzi za maana !! ndo utoe hisia zako huko maana n hisia mkanganyiko n mtafaruku
2.Huelewi tofauti ya presentation na self thinking !! yako hii n self thinking no mpangilio wa mawazo,habar zisizoshabihiana na utahira mwingi

3.Unaichamba serikali , acha taarabu serikali c mangekimambi ni taasisi! Jiwe kizan
4.Unaonekana unatetea panya road na wale magaidi wa kibiti (Ushikwe uchunguzwe)
5.Una mihemuko hujui unachoongea wala unachotarget wala huna conclusion (Upewe msaada wa kisaikologia)
6.Unadharirisha wene simu za infinix tusnze kuona labda wako na shida
 
Huna point wewe unajambajamba tu hapa. Usihalalishe uovu kwa jinsi hisia zako zinavyokutuma. Nchi zote zinaongozwa na Katiba, tuwekee Ibara au kifungu kinacho sapoti hizo pumba zako ulizoandika hapo juu.
Mbona wewe ndio umejambajamba
 
Kama angezaliwa ngombe wa maziwa badala yako mtoa mada ingekuwa bora zaidi!
 
Huna point wewe unajambajamba tu hapa. Usihalalishe uovu kwa jinsi hisia zako zinavyokutuma. Nchi zote zinaongozwa na Katiba, tuwekee Ibara au kifungu kinacho sapoti hizo pumba zako ulizoandika hapo juu.
Ulinzi na usalama ni haki ya raia wote!
Raia lazima walindwe
Serikali lazima ilindwe

Taifa lazima liwe na idara za kuilinda serikali na kuwalinda raia!

Ni kweli kuanzisha idara ya ulinzi na usalama Unasubiri katiba iseme?

Je, katiba pia imesapoti uanzishaji wa hospitali ya Muhimbili, au Chuo kikuu Cha Dar es Salaam, au Tanesco

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kama Ben saanane ameuawa bila hatia, dhambi yake Ni sawasawa na "panyaroad" aliyeuawa bila hatia!
Its true, kuna, kuna kitu kinaitwa karma hakina mswalie Mtume, hata Ben, huwezi jua kilimtokea nini ila na yeye aliwahi kutuhumiwa humu kutumwa kumuua mtu fulani wa Chadema kwa sumu ya panya. Mtanzania: Dr. Slaa atajwa kumtuma Ben Saanane kummaliza Zitto taarifa hii ilithibitishwa na mwana jf huyu Uthibitisho wa kazi maalum ya Ben Saanane na hujuma za Dr. Slaa kwenye siasa za Juliana Shonza
Kama Lisu alipigwa risasi bila hatia, dhambi yake ni ileile ya kumpiga risasi "panyaroad" asiye na hatia!
Its true hata hapa karma applies, Kagenzi wa Chadema aliingizwa kwenye torture chamber pale ufipa na kutoka mwili umetobolewa tobolewa kwa majeraha huu ni ushahidi wa mwana jf huyu
Hivyo inawezekana kilichomkuta ni karma ya Kagenzi!.
Tutulie, tuendelee kushuhudia mauaji ya raia kwa raia, Serikali kwa raia!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Wauwaji wote karma itawashughulikia na wao watakufa.
P
 
Unaijua mbinu ya kung'ata na kupuliza kwa kupigapiga kwa upole mgongoni aisee.Upo vizuri.Pale Lumumba watakuambia weye ni msemakweli hadi basi.
 
Sawa sawa,serikali ingesting sheria ya kunyonga mtu akipatikana na kosa la kuiba Mali na pesa za umma

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…