Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 12,599
- 26,263
Ni ngumu ku notice sabotage, kwasababu inafanyika at lower level, mfano mdogo tu, utajuaje kwamba AC huwa zipo on mpaka usiku alihali zilitakiwa kuzimwa?
Au delivery ya raw materials ilitakiwa kuja ijumaa, unaambiwa itakuja jumatatu ijayo, obviously kwa akili ya kawaida, unaweza kuona kwamba haina impact lakini ina madhara makubwa
At corporate level, vitu vidogo vidogo kama hivo huwezi kuona kama vinaweza kuua taasisi, ila vina mchango wa kipekee.
Speaking of capital, hivi viwanda kwa mara ya kwanza viliweza kuanzishwa na vilikuwa vipo capitalized vya kutosha, hoja ya kukosekana capital, maana yake ni kwamba vilikuwa loss making entities.
Sasa ukichunguza kwanini loss making, kwa namna moja lazima urudi kwenye expenses na machine failures ambayo mimi ndio nina mashaka, kwamba these might have been sabotage operations, na ndo hoja yangu ilipolalia
Chief, gharama za uendeshaji Africa na nchi nyingi ni ghali kuliko China hilo lipo wapi.
Gharama ya unit moya ya umeme TZ ni kubwa kuliko China, Ulaya na America. Hiyo tu inaongeza gharama kwa mtumiaji wa mwisho. Hapo sijaongelea umeme hafifu kuendesha viwanda nchini, sahizi ndo bwana la Nyerere limeanza kazi ila nalo bado halikidhi mahitaji ya raia tu let alone viwanda.
Logistical barrier nayo ni changamoto. Huko China kuna miji ni viwanda tu, kila kitu kipo hapo hapo huku bongo pamba inalimwa S/Wanga, hadi ifike kiwandani Arusha kwa lori hadi wk iishe na kama halijaharibika njiani.
Matatizo ni mengi. Hata bila sabotage viwanda kufa kibudu ilikua swala la muda tu kama nchi zingine zote zinavyoagiza bidhaa zote China.