Wanasiasa wa Tanzania wanaongeleaga kuhusu viwanda ila sijawahi wasikia wakiongelea na inteligensia ya kuvilinda viwanda


Chief, gharama za uendeshaji Africa na nchi nyingi ni ghali kuliko China hilo lipo wapi.

Gharama ya unit moya ya umeme TZ ni kubwa kuliko China, Ulaya na America. Hiyo tu inaongeza gharama kwa mtumiaji wa mwisho. Hapo sijaongelea umeme hafifu kuendesha viwanda nchini, sahizi ndo bwana la Nyerere limeanza kazi ila nalo bado halikidhi mahitaji ya raia tu let alone viwanda.

Logistical barrier nayo ni changamoto. Huko China kuna miji ni viwanda tu, kila kitu kipo hapo hapo huku bongo pamba inalimwa S/Wanga, hadi ifike kiwandani Arusha kwa lori hadi wk iishe na kama halijaharibika njiani.

Matatizo ni mengi. Hata bila sabotage viwanda kufa kibudu ilikua swala la muda tu kama nchi zingine zote zinavyoagiza bidhaa zote China.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…