Wanasiasa wa upinzani wamerogwa au ni matumbo yao?

Wanasiasa wa upinzani wamerogwa au ni matumbo yao?

Cosovo

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2018
Posts
667
Reaction score
1,810
Watanzania sijui tuseme kuna kitu hakipo sawa kwenye vichwa vyetu.

Marais wastaafu wawili waliisha andika vitabu kuhusu maisha yao tangu utotoni mpaka madarakani.

Wameonyesha kwenye maandishi jinsi CCM inavyotumia kila aina za mbinu za hila ili ibaki madarakani.

Mkapa ameonyesha jinsi CCM inavyobana isiwepo Tume huru ambayo itatokana na katiba mpya maana utakuwa mwiba kwa CCM.

Vivyo hivyo kwa Mwinyi jinsi CCM inavyotumia kila aina ya mbinu isiondolewe madarakani.

Inasikitisha bado wanasiasa wa upinzani wanashiriki uchaguzi ambao hawataweza kuingia madarakani inasikitisha sana.

Nilitegemea baada ya vitabu vya mwinyi na mkapa kuwa wazi kwenye masuala ya uchaguzi na demokrasia basi wachukue hatua.

Moja ya hatua ni kutangaza kutoshiriki uchaguzi wowote mpaka katiba mpya iliyo na tume huru ya uchaguzi.

Kuwahamasisha wananchi kupitia vyombo vya habari, mitandao na njia zingine wimbo uwe "Tunataka Katiba mpya yenye Tume huru ya uchaguzi" ili sasa wananchi wapressurelize serikali ili watekeleze matakwa ya wananchi.

Kuendelea kushiriki uchaguzi kwa sasa na maandishi ya watawala yako wazi,inaonyesha wanasiasa walivyo vilaza au wanafanya siasa kwa ajili ya matumbo yao.
 
So right.
Ila pia tuangalie Kama CCM wapo tayari kutengeneza katiba mpya kwa manufaa ya Tanzania.
 
Kushiriki uchagu Tanzania bada ya yote yaliyo tendeka kaika uchaguzi mkuu uliopita ni ukesefu w uoni na kuisaidia CCM kuudnganya Ulimwengu kuwepo kwa Demokrasia Tanzania wakati hakuna demokrasi kabisa.
 
Yaliyofanyika mwaka Jana ni jawabu Tosha Kuwa bila tume huru ya uchaguzi ni kama kumpigia mbuzi gitaa
 
Nilitegemea baada ya vitabu vya mwinyi na mkapa kuwa wazi kwenye masuala ya uchaguzi na demokrasia basi wachukue hatua

Moja ya hatua ni kutangaza kutoshiriki uchaguzi wowote mpaka katiba mpya iliyo na tume huru ya uchaguzi
Hata hao ambao hawashiriki uchaguzi, kazi yao kubwa kwa sasa ni lazima iwe ni kuhusu "Tume Huru ya Ucxhaguzi".

Bila shaka wanaahirisha kazi hiyo kwa sasa kupisha mkutano walio ahidiwa, vinginevyo hawataeleweka wasipofanya hivyo.

Jambo la kuwa na katiba mpya ni muhimu, lakini pengine si muhimu sana kuizidi kuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi kwa sasa. Badala yake kutumia nguvu nyingi juu ya Katiba kutakuwa ni kupunguza nguvu zao kwa jambo hili muhimu sana la Tume Huru ya Uchaguzi.
 
Kushiriki uchagu Tanzania bada ya yote yaliyo tendeka kaika uchaguzi mkuu uliopita ni ukesefu w uoni na kuisaidia CCM kuudnganya Ulimwengu kuwepo kwa Demokrasia TZ wakati hakuna demokrasi kabisa.
Wapinzani halioni kuwa wanawapa ccm kuendelea kudanganya dunia
 
Back
Top Bottom