Wanasiasa wachovu acheni kumsakama Rais Samia!

Sasa hivi ngoma ni CCM kwa CCM wanavyomnanga Magufuli utafikri hawakumuweka wao madarakani na wanavyomnanga mama utafikri siyo mtu wao.

Huu ni ulaghai kwa watanzania, Tanzania iwe na neema wakupewa sifa ni CCM kwa kuwa ndio wanaongoza nchi hata nchi inapoharibika wanaoiharibu nchi ni CCM kwa kuwa ndio wanaongoza nchi, wapinzani hawajawahi kuongoza nchi na hawakusanyi kodi.
 
Well Noted Mkuu..
 
Sukuma Gang wanazulia Samia mambo mengi sana
Huko China, lilizuka kundi la The Gang of Four baada ya kifo cha Mao Tse Tung aliyekuwa kiongozi wa China.
Katika hilo kundi alikuwemo hata mke wa Mao.
Nia ya kundi ilikuwa kuchukua madaraka yote ya kisiasa na dola.

Wakawahiwa, sina uhakika kama hawakunyongwa.

Hapa kwetu vile vile kundi kama hilo limejitokeza, lishughulikiwe kikamilifu.
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Mama kawapa uhuru wa kuongea; wacha waendelee kujianika ili wajulikane wasaliti..

Mpk kufika 2025 (Mungu akipenda) watajulikana wote
 
Haya sema wewe basi kama unaona kumsema Samia wanafaidika na lolote...

Na ukiona husemwi basi ujue hakuna jipya unafanya.
 
Haya sema wewe basi kama unaona kumsema Samia wanafaidika na lolote...

Na ukiona husemwi basi ujue hakuna jipya unafanya.
Nampa mama BIG UP kwa kugeuza upepo wa serikali yake ukilinganisha na Magufuli.
Kuna akina nyie mlishangilia chochote tu mradi hamguswi Awamu ya Tano.
Kuna tulio ibiwa , komolewa, na kunyang'anywa kwa kutumia mkono wa serikali.
 
Kama hataki kusemwa aachie ngazi hii ni ofisi ya umma siyo mali yake binafsi, mbona Bakheresa hasemwi?
 
Atulie au aachie ngazi
Uzuri wa Mama Samia si kichwa kigumu kama yule bichwa.
Naamini hata humu JF anaona maoni na kuyapima.
Mfumuko wa bei kutokana na kupanda bei ya mafuta ni lazima umewashitua na malamiko yapo mengi toka bungeni hadi mitaani.
Lakini naona analishughulikia kupunguza makali, tusubiri june 1st.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…