Wanasiasa wajanja wengi wamejificha, kidole mdomoni, wanaadabu. Onyo la MO29 ni mpumbavu pekee anaweza kulipuuza

Wanasiasa wajanja wengi wamejificha, kidole mdomoni, wanaadabu. Onyo la MO29 ni mpumbavu pekee anaweza kulipuuza

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo wote!

1. MO29 ilikuwa ni mawingu. Ilionyesha uwezekano pasipo uwezekano.

2. Uliwahi kujiuliza kama MO29 ingefanikiwa walau kwa asilimia 50% nini kingetokea? Najua sio Kila MTU anaweza ku-project matukio, lakini ninakuhakikishia ukweli ni kuwa MO29 ingefanikiwa walau kwa 50% mpaka sasa nchi ingekuwa kwenye milio ya risasi, mabomu na hekaheka.

3. Wahanga wa MO29 wangekuwa Wanasiasa wote mashuhuri wenye historia za kukosa uadilifu, wapambe wap maarufu, wasanii maarufu, baadhi ya matajiri wakigeni...

4. Wanasiasa na matajiri wenye Akili kwa sasa wameshapata Somo, ingawaje tangu awali. Wanasiasa wajanja na wafanyabiashara wenye akili huficha majina ya biashara na Mali zao kama wanajihusisha na siasa.

5. Ingawaje wapo wachache ambao hawajifunzi mpaka yawakute moja kwa moja.

6. Kama hakutakuwa na mabadiliko ya wazi kubadilisha zile kero za msingi ndani ya taifa. Basi Ile volcano imelala. Haipo active wala haijafa. Ilitishia tuu kulipuka ikazima. Na Siku ikifanikiwa kulipuka. Watu tutatafutana humu.

7. Siongei haya kumtisha yeyote. Bali kutoa tahadhari. Kuona mambo yanafanyikaje ili kuhakikisha kero za msingi zinatatuliwa na haki hasa za kisiasa zinawekwa sawa. Maana malalamiko makuu ni haki za kisiasa. Na baadhi ya watu kuonekana wanamamlaka ya nchi na haki kuliko wengine. Wamejimilikisha.

8. Sisi tupo. Wazee na wataalam msiwe waoga kurekebisha na kushauri makosa ya kibinafsi ya mtu au kikundi cha watu kwa maslahi ya Taifa.

9. Juzijuzi hapa almanusura nchi hii iingie kwenye shida.

10. Vyombo vya Dola visikariri na kujivunia kwamba vilidhibiti Hali Ile. Isipokuwa viangalie nini kilisababisha Hali Ile. Kisha marekebisho yafanyike.

11. Kwa sababu Wale Vijana walioandamana hawakuwa na lengo la kuua mtu. Walikuwa na hasira lakini haikufika hasira ya kuua mtu.

12. Kama hasira zao zingefikia kuwaza kuua mtu mambo yangekuwa mengine.

13. 2030 Katiba mpya itakuwa suluhu ya hiki kilichotokea mwaka 2025.

14. Kama kuna mtu mwenye hofu na maslahi yake basi itampasa aandae mfumo wa vyama vikuu kuanza moja na kuacha yaliyopita.

Nawatakia sikukuu njema
 
Wame uwa watu
Wanatunyamazisha kwa kubinya uhuru wa habar
Wamewa ngoS wanazisingizia
Hakuna uchaguzi huru
Bunge li kibogoyo
Hawatuohopi Tena?
 
Back
Top Bottom