Wanasiasa waliosema wamehama vyama vyao na kujiunga na CCM kwa kuwa wananafurahishwa na Magufuli, siku Magufuli muda wake ukiisha wataenda nae Chato?

Wanasiasa waliosema wamehama vyama vyao na kujiunga na CCM kwa kuwa wananafurahishwa na Magufuli, siku Magufuli muda wake ukiisha wataenda nae Chato?

mkuu mbona umeandika mada shallow kuliko ilivyo kawaida yako? Yaani waende nae chato? sasa si ungeuliza hata kama wangehama CCM na kurudi kwenye vyama vyao? hili la kurudi chato umeandika kumshambulia Magufuli personally
Mkuu, tatizo unaangalia kwenye kinyumbulisho cha thread badala ya core issue ya thread. Wewe umeenda ku-focus kwenye suala la "wataenda Chato" ambalo sio udhui la thread, bali ni figurative speech. Ni sawa na nikukuambia nitakupiga hadi baba yako asikutambue, halafu unaanza kujadili suala la baba yako kutokutambua badala ya kupigwa. Sasa huko ni kutokuwa na uwezo mkubwa katika suala la fasihi maandishi.

Suala la msingi katika thread hii ni kukosoa ubendera wa wanasiasa kwa kutojikita katika sera za vyama vyao na badala yake kusimamia kupendezwa na mtu. Katika suala la organizational theory, vyama vya siasa ni organizations ambazo zinapaswa ku-outlive members wake, hivyo wanaojiunga na organizations hizo wanapaswa kuwa na ufahamu huo kama wana akili sawasawa.

Hivi wewe leo unaweza kusema nimeamua kuajiiwa na timu ya Yanga kwa sababu nampenda kepteni wake? Sasa nikukuuliza utaenda kuwa mpishi wa huyo kepteni siku mpira wake ukiisha akaondolewa Yanga suala la kujadili sio kwenda kuwa mpishi wa kepteni. Focus kwenye issue kuu acha trivialities kwenye thread. Huwa zinawekwa kuzipamba thread. Lazima uonyeshe tofauti kati yako na mtu wa kijijini katika kusoma thread zangu, maana umeshasema huwa naandika thread zenye material.
 
Na wale waliomuongezea muda mwenyekiti na kuimba mwamna tuvushe siku akifa wanaenda nae kaburini?
Hilo nalo jambo. Watu wanaongea bila kutumia akili. Kwa nini ufikirie kwamba katika wati karibu zaidi ya milioni 50 nchini hakuna anaeweza kupatikana kuongoza nchi? Watu walifikiri baada ya Nyerere Tanzania ingekwisha sembuse Magufuli?
 
Wala hawakwenda kumuunga mkono wala nini
Ni mkate tuu ndio waliokuwa wanatafuta
Haoo kama wataona mkate bado upo watabaki hukohuko baada Mh Magufuli
Kuna waliohama wanaodhani wakipiga kelele kuvitukana vyama walivyohama kuliko wengine ndani ya CCM basi ndivyo wanaonyesha mapenzi yao ya dhati kwa CCM. Nawaona kama mwanamke anaemkashifu mume wake wa kwanza kwa mume wa pili katika kumuonyesha kuwa anampenda.

Ukiwa mume uliyeoa mwanamke aliyeachika, hivi utajisikia ufahari kuambiwa mume wangu una dushulelele zuri kuliko la mume wangu wa kwanza? Kwanza tukiwa chumbani alikuwa hafanyi kama hivi unavyofanya? Na wewe bila akili unaamini kila unaloambiwa na kukenua meno kwa kicheko? Maana ndivyo wanavyofanya CCM, na kama mume mjinga na mpumbavu, hawaoni hilo kuwa ni tatizo.

Huyo si mke, ni malaya tu. Achana nae. Na CCM wanapaswa kulijua hili.
 
Mkuu, tatizo unaangalia kwenye kinyumbulisho cha thread badala ya core issue ya thread. Wewe umeenda ku-focus kwenye suala la "wataenda Chato" ambalo sio udhui la thread, bali ni figurative speech. Ni sawa na nikukuambia nitakupiga hadi baba yako asikutambue, halafu unaanza kujadili suala la baba yako kutokutambua badala ya kupigwa. Sasa huko ni kutokuwa na uwezo mkubwa katika suala la fasihi maandishi.

Suala la msingi katika thread hii ni kukosoa ubendera wa wanasiasa kwa kutojikita katika sera za vyama vyao na badala yake kusimamia kupendezwa na mtu. Katika suala la organizational theory, vyama vya siasa ni organizations ambazo zinapaswa ku-outlive members wake, hivyo wanaojiunga na organizations hizo wanapaswa kuwa na ufahamu huo kama wana akili sawasawa.

Hivi wewe leo unaweza kusema nimeamua kuajiiwa na timu ya Yanga kwa sababu nampenda kepteni wake? Sasa nikukuuliza utaenda kuwa mpishi wa huyo kepteni siku mpira wake ukiisha akaondolewa Yanga suala la kujadili sio kwenda kuwa mpishi wa kepteni. Focus kwenye issue kuu acha trivialities kwenye thread. Huwa zinawekwa kuzipamba thread. Lazima uonyeshe tofauti kati yako na mtu wa kijijini katika kusoma thread zangu, maana umeshasema huwa naandika thread zenye material.
Ok, ila vyama vingi Africa ndivyo vilivyo, havina itikadi bali hufuata msimamo wa kiongozi wao, ndio maana Uongozi wa Magufuli, Kikweta na Mkpa na mwinyi, wote wana itikadi tofauti kabisa, mwingine anaunga mkono ubinafsishaji, mwingine anakuja kuupinga na kuonekana anaenda mwendo wa reverse kabisa badala ya kuboresha

So siasa zetu ni za kufuata viongozi kwa kuangalia personalities zao na maoni yao binafsi, na sio itikadi ya chama, hili ni CCM, na wapinzani wote, so mwanasiasa akitoka chama fulani kwenda kingine sababu ya kiongozi haishangazi
 
Ewaaa! Sasa tunaanza kuongea lugha moja. Lengo la thread hii ni kufunua ubaya huo wa siasa zetu unaousema. Kwani wewe unaona sio tatizo tuendelee nao? Mie unaniudhi sana. KUna thread moja humu nilisema afadhali kuanza upya, kuondoa vyama vyote hivi CCM, Chadema nk na tuanze upya kwa kuwa wote sasa wamefikia kuwa na mentality mbaya tu, hakuna aliye b bora. Hata niliuliza, hivi mnadhani Chadema wakichukua nchi ndio amani yetu itarudi? Nikasema jambo la kwanza watataka kumweka Magufuli ndani, Makonda ahukumiwe kunyongwa, Siro afungwe maisha, Gambo wa Arusha afungwe miaka kumi nk Nilisema wazi naona ubabe na uonevu unafanywa sana kwa vyama vya upinzani, lakini tatizo kubwa zaidi ni kwamba simwoni Mandela kati ya viongozi wa vyama vya upinzani atakaehubiri kusahau yaliyopita wakichukua nchi na kuwa chama tawala.

Hata nikasema ni vema sana tungekuwa na mgombea binafsi ili atuanzishie mambo upya - na CCM wanajua hilo ndio maana hawataki kulikubali!
 
Sasa Hilo tatizo lakini umeliangalia kwa juu juu sana
Siasa za nchi zinakuwa shaped na wananchi ambao ndio wafuasi wanaowapa umaarufu wanasiasa
Kama wananchi wanapenda na kuitikia zaidi siasa za kimhemuko za kukomoana kuliko za kisera, ni dhahiri wanasiasa watakaokuwa maarufu ni wale walio na kipaji Cha kutema misemo ya kuwashambulia wapinzani wao na sio wale wa ku analyze na kuja na itikadi na sera mbadala

So elimu ndio tatizo kubwa hapa, watu wakielimka, hata siasa zetu zitabadilika kwa kuwa walaji ni tofauti
 
Wanafurahishwa na Magufuli au utendaji kazi wake?

BTW: Kwani ULIPO TUPO waliohamia CDM na Lowasa wapo wapi now?
 
Hakuna kitu kilichokuwa kikinishangaza - kama sio kuchefusha, kama kumsikia mwanasiasa, mwanaume au mwanamke mzima ambaye tunatumaini ana akili timamu na za kutosha, akitamka hadharani kwamba ameamua kutoka chama chake kwa kuwa eti amefurahishwa sana na Magufuli!

Hivi kweli hawa wanasiasa hawaoni aibu kutamka maneno kama haya mbele ya watu?

Wote siku zote tumeamini kwamba mwanasiasa anakuwa mwanachama wa chama fulani kwa kuamoni itikati au sera za chama hicho. Lakini mwanasiasa kuonyesha kwamba yeye suala la itikadi au sera za chama sio muhimu bali mtu fulani baki katika chama ndio anamvutia kiasi cha kuacha chama chake, huo ni ulevi na ujinga wa kisiasa ambao unatia hata aibu kuusema hdharani.

Mwalimu Nyerere aliwahi kutamka kwamba kuna watu katika siasa ni malaya wa kisiasa (political prostitution). Naamini kabisa alikuwa akiongelea watu kama hawa pia. Na baadae aliongelea kwamba kumpenda mtu na kutumia mapenzi hayo kwa mtu binafsi kama msingi wa kufanya uamuzi wa kisiasa haifai kabisa, kwa kuwa kupenda kwa namna hiyo kunapaswa kuhusianishwe na kutoleana posa! Alisema peleka posa tukacheka bila kuelewa aliwaza mbali sana.

Mimi nilitegemea kwamba wanasiasa hawa, hata kama ni kweli walihama vyama vyao kwa kufurahishwa na Magufuli, basi angalau wangekuwa na aibu ya kutuambia "nimehama chama changu kwa kuwa nimeipenda CCM na sera zake", sio "nimehama chama changu kwa kuwa nimempenda Magufuli". Huwezi kuwa mwanasiasa mwenye akili sawasawa ikiwa unahama chama chako kwenda CCM kwa kumfanya Magufuli ndio CCM.

Hebu fikiria, wewe unahama Chadema au CUF, na unajiunga na CCM kwa kuwa unafurahishwa na Magufuli. Sasa siku Magufuli akimaliza muda wake, au hata akishindwa uchaguzi wa 2020, utaenda aye Chato ukasaidiane kazi za nyumbani kwake na Mama Magufuli? Au tutarajie kwamba Magufuli akiondoka ikulu basi hawa wanasiasa itabidi watutangazie tena kurudi vyama walivyotoka kwa kuwa Magufuli sio raisi tena?

Kwa kweli akili ni nywele.
Mwenyekiti wa Ccm ambae ndio Rais wa Tanzania amewafurahisha kwa kufanya waliyoyataka. Kama wakihamia Ccm hakuna tatizo. We ulikuwa hutaki haya yanayofanyika yafanyanyike?
 
Synthesizer kwani na wale wote wanaompenda pia Mbowe, Lissu, Sugu, Lema na Msigwa nao Wakistaafu Siasa watawafuata huko Makwao Kiasili?
 
Kuna waliohama wanaodhani wakipga kelele kuvitukana vyama walivyohama kuliko wengine ndani ya CCM basi ndivyo wanaonyesha mapaenzi yao ya dhati kwa CCM. Nawaona kama mwanamke anaemkashifu mume wake wa kwanza kwa mume wa pili katika kumuonyesha kuwa anampenda.

Ukiwa mume uliyeoa mwanamke aliyeachika, hivi utajisikia ufahari kuambiwa mume wangu unajua una dushulelele nzuri kuliko la mume wangu wa kwanza? Kwanza tukiwa chumbani alikuwa hafanyi kama hivi unavyofanya? Na wewe bila akili unaamini kila unaloambiwa na kukenua meno kwa kicheko? Maana ndivyo wanavyofanya CCM, na kama mume mjinga na mpumbavu, hawaoni hilo kuwa ni tatizo.

Huyo si mke, ni malaya tu. Achana nae. Na CCM wanapaswa kulijua hili.
Umetishaa mkuuuu
Kuna wimbo moja wa injili unasema Mikateee mtu anaweza kuisha mkatee
 
Synthesizer kwani na wale wote wanaompenda pia Mbowe, Lissu, Sugu, Lema na Msigwa nao Wakistaafu Siasa watawafuata huko Makwao Kiasili?
Mkuu kama vitu vidogo kama hivi unashindwa kuelewa sijui tukusaidieje? Nenda shule. Thread inaongelea kuhama chama chako na kujiunga na CCM na sababu yako ya kuhama unasema ni kumpenda Magufuli. Hatuongelei watu wanaompenda Magufuli wakiwa ndani ya CCM au wanaowapenda kina Mbowe wakiwa ndani ya Chadema. Kumpenda kiongozi wa chama chako ni jambo la kawaida, lakini kuhama chama kwa kumpenda kiongozi wa chama kingine ni jambo la uendawazimu na umalaya wa kisiasa
 
Mwenyekiti wa Ccm ambae ndio Rais wa Tanzania amewafurahisha kwa kufanya waliyoyataka. Kama wakihamia Ccm hakuna tatizo. We ulikuwa hutaki haya yanayofanyika yafanyanyike?
Bado hujaelewa. Jaribu kusoma tena thread, la sivyo nenda shule. Unachoonyesha hapa ni tofauti kati yako na mtu aliyyeenda shule katika kusoma na kuelewa maudhui.
 
Mwenyekiti yeyote wa CCM baada ya Magufuli, akiwa na akili nzuri itabidi awaweke mbali kabisa hawa wanasiasa waliohamia CCM kwa sababu ya kufurahishwa na Magufuli. Walimfuata Magufuli sio CCM!
wewe nawe ni mshauri wa Chama Cha Mapinduzi? Haya maneno yangefaa sana pale ufipa 2015 walipoiacha "mbachao kwa msala upitao" RIP Ukawa
 
Back
Top Bottom