Wanasiasa wanaolewa vyeo wanaweza kujishusha kama Said Bakhresa?, kuna somo kwa wanasiasa vijana kutolewa vyeo

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
18,487
Reaction score
13,611
Hayati mmoja mwanasiasa akiwa waziri wa fedha aliongea kwa jeuri sana kauli iliyomfuata hata baada ya kifo chake, pale aliposema ndege ya Rais ni lazima itanunuliwa ikibidi hata wote tule majani!. Kauli ile ilileta mijadala mingi miongoni mwa wafuatiliaji wa siasa za nchi hii.

Ilikuwa ni jeuri ya hali ya juu sana, kwamba walio katika tabaka la siasa hawawajali wavuja jasho wala hisia zao kwamba watayapokea maneno yao. Ndege ya Rais ikaja na kutumika na ndipo tukagundua kuwa tumepigwa tena pesa ndefu.

Kauli kama ile ya RIP waziri wa fedha wa awamu ya tatu ni kama ilijirudia mwaka huu kutoka kwa waziri mwingine mwenye cheo hicho hicho. Aliposema kuwa tozo zitalipwa tu kama mtu hapendi basi na aende Burundi. Alikutana na kauli nyingi za wanaharakati na ikambidi ajirudi aongee kwa adabu siku alipotangaza kuwa tozo zimefutwa.

Hiki kiburi ni tofauti kabisa na ile hulka ya Bilionea mmoja mwenye asili ya visiwani, ambaye tangu miaka ile ya 1980 mwanzoni akiishi kariakoo amekuwa ni binadamu mwenye kujishusha sana. Miaka ile kila siku ya Ijumaa na siku zile za sherehe za kiislam Mzee Bakhresa anagawa pesa kwa wazee maskini na watu wasiojiweza.

Mpaka miaka ya sasa anabeba jukumu la mazishi ya wapemba wengi wanaofia huku bara, kubeba mwili kuupeleka visiwani na gharama nyingine anazichukua yeye. Utu wake ni baraka kubwa kwa biashara zake.

Watu wanapomuona Bakhresa akitanua biashara zake katika mataifa yanayotuzunguka watambue kuwa hiyo ni faida ya kujishusha na wema ndani yake. Kujinyenyekeza kwamba mzee kuna watu wanakuita hapo nje na yeye akaenda kuwasikiliza shida zao, sio kila mtu mwenye uwezo huo.

Wanasiasa vijana msilewe sana vyeo, magari mazuri ya bei mbaya, walinzi na wasaidizi. Hivyo ni vitu vya kupita tu. Chungeni kauli zenu muda wote, msitegemee ulinzi wa kibinadamu huo hutoweka kama upepo wa baharini.

Ni fahari ya muda mfupi tu. Malkia Elizabeth aliishi ndani ya kasri yenye thamani ya dola bilioni tano lakini siku ya kufa ilipofika walimtoa kutoka alipokuwa analala na kuandaa mipango ya mazishi yake.

Ile kofia ya Malkia ni mabilioni ya fedha thamani yake, siku moyo wake uliposimama na uhai kumtoka kila alichokuwa anavaa kikawekwa pembeni.

Wanasiasa vijana jishusheni siku zote, vyeo na madaraka ni mtego wa muda mfupi.
 
Mkuu

Kwanza kabisa kwa kuleta mada hii ila umeponyoka njia kidogo

1. Bakheresa sio mwanasiasa kwa hiyo mfano wako hautekelezeki
2. Mwanasiasa yeyote ndiye chanzo cha kufanikiwa mwingine au kushindwa
3. Kiini cha uovu wote chanzo chake ni siasa
4. Diplomasia, demokrasia ya kizungu na siasa za kushika dola ni chanzo cha mzizi wa wa uovu wote duniani (kauli na kitendo chochote cha mwanasiasa kinaweza kusababisha furaha au huzuni ya kudumu.....
5. Mbona hujataja kauli ya David Msuya, John Malecela zinazofanana na hizo za mawaziri wa fedha lakini bado wapo?
 
Kujishusha ndio ujumbe wangu.
 
Lengo la Ujumbe wako- ni Kujishusha na kujinyenyekeza. Hapo nimekupata vizuri kabisa ndugu, isipokuwa mfano uliotoa wa kumlinganisha mfanyabiashara na mwanasiasa hauna uwiano sawa. Ni kama kulinganisha tunda la tufaa (apple) na ndimu.
 
Ungetolea tu mfano mwingine... mfanyabiashara kama Bakresa hadi kufikia hapo lazima kuna "behind the scenes" nyingi sana. Halafu hata huyo Bakresa ni mnafiki kwa sababu ana tamaa ya kukusanya hela zetu zote bila kujali kuumiza wengine... hadi chapati anataka awe yeye peke yake. Isitoshe hata yeye alikuwa na kashfa ya kutolipa kodi.. Magu akamlazimisha alipe. Hakuna mfanyabiashara anayetoa tu hela zake bila kujua zinarudije. Na pia kwenye kutoa lazima mwisho wa mwaka iandikwe kwenye Financial Statements... anaweza kutoa 5000 akaandika alitoa 9000. TAFUTA MFANO MWINGINE ILI UZI WAKO UPATE UHALALI
 
Wanasiasa vijana msilewe sana vyeo, magari mazuri ya bei mbaya, walinzi na wasaidizi. Hivyo ni vitu vya kupita tu. Chungeni kauli zenu muda wote, msitegemee ulinzi wa kibinadamu huo hutoweka kama upepo wa baharini.

Wanasiasa vijana jishusheni siku zote, vyeo na madaraka ni mtego wa muda mfupi.
Naunga mkono hoja
P
 
Back
Top Bottom