Wanasiasa watano ambao waliipenda siasa ikawanufaisha lakini ikawadhalilisha kuwaondolea utu wao hapa nchini kwa miaka ya karibuni hawa hapa

Wanasiasa watano ambao waliipenda siasa ikawanufaisha lakini ikawadhalilisha kuwaondolea utu wao hapa nchini kwa miaka ya karibuni hawa hapa

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
1. Job Ndugai; alipata madaraka makubwa na katika maeneo yote aliyowahi kuongoza hakuna eneo alifanikiwa kupewa sifa Bali siasa ilimfedgeesha.

Kwa SASA amezeeka lakini uzee wake umeambatana na fedhea kubwa Sana yakuondolewa uspika kabla ya kumaliza muda wake. Mdomo uleule uliompa nafasi ndio huo huo uliomponza alipoutumia vibaya Kwa wenye madaraka kumzidi yetu. Pole Mzee

2. Prof. Kabudi; alipigania nchi Kwa miaka mingi akiwa jalalani. Alipotokea msamaria mwema akampa chakula, mavazi, malazi na usafiri huku akikkaa viti vya mbele Kwa mfalme akaamua kuwadhalilisha aliokuwa anawatetea akiwa jalalani badala yake akawa anataka wakihisi njaa watabasamu.

Leo hata kutokeza kwenye camera Hana hamu; NI kweli kwamba ana fedha na hadhi kubwa lakini ladha ya anavyomiliki haioni tena.

3. Dr. Wilbroad Slaa; alikerwa na Lowasa na akaamua kusimama imara juu ya kile alichokuwa anaamini. Walipomkuta amesimama Hana hili wala lile wakampa chakula akasahu waliomlisha NI maadui wake kuliko hata huyo Lowasa mmoja.

Akaungama nao na kutetea Yale mabaya aliyokuwa anayaponga awali. Ana sifa ya ubalozi lakini shida yake hapo awali ilikuwa sifa hadhi Bali utu. Amepoteza utu wake wa kale na sasa Hana rafiki WA kweli na hata kijijini ajisikii furaha kushirikiana na wanakijiji. Alishindwa kuzichanga karata amepoteza heshima yake yote.

4. Dr. Bashiru wa katiba mpya Kwa SASA Hana agenda, anatamani asingeteuliwa may be angekuwa na sifa kwenye jamii. Kapoteza dira na Hana pakuanzia. Aliwambia wananchi ukubwa wa dola SASA dola imeomwonyesha haina rafiki WA kudumu. Wananchi nao wameona si MTU sasa kuwasemea.

5. Halima Mdee na wenzake hata kwenye mitandao wanaogopa; wapo wengine wamepewa wilaya lakini toka wateuliwe awajawahi kutoka adharani. Wanajua dhambi waliyotenda ilivyo kubwa, ndiyo imetoka hivyo. Ingawa Mdee zipo Tetesi kwamba soon ananunua Uhuru wake na atatema mzigo, but uaminifu wa zamani umekwisha

Tamaa zisikae kwenye ubongo, njaa ibaki tumboni ila siyo kichwani.
 
Bashite na bashiru vijana wa hovyo kbs
 
Ondoa jina la Dk Slaa hapo. Alisimama kwenye msimamo wake na hakuna alipodhalilika. CHADEMA kwasababu ya kukosa mbadala wa Dk Slaa ndo maana mnaweweseka.

Ikumbukwe Dk Slaa hadi akiwa CHADEMA alikuwa hajarudisha kadi ya CCM. Alienda CHADEMA kwasababu ya jina kukatwa Dodoma 1995.

Zilikuwa hasira tu ila ni mwanaCCM damudamu. Itachukua miaka mingi CHADEMA kupata mbadala wa Dk Slaa.
 
Back
Top Bottom