Wanasiasa watendeeni wengine mema ili kulinda kesho bora ya vizazi vyenu

Wanasiasa watendeeni wengine mema ili kulinda kesho bora ya vizazi vyenu

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
4,095
Reaction score
13,016
Wanasiasa kumbukeni madaraka hukoma, sasa kama mtawatendea wengine mabaya kipindi cha uongozi wenu, huenda moja kwa moja msione madhara kwa sasa.

Ila kesho hao ambao mnawatendea mabaya wakishika hatamu ya uongozi vizazi vyenu havitakuwa salama.

Sishangai kuona baadhi ya viongozi hasa Africa kuendelea kung'ang'ania madaraka, ni kulinda mabaya waliyoyatenda wakati wa uongozi wao.

Kesho bora ya vizazi vyenu na mali zenu mnatakiwa kuandaa leo, leo hii mpo kwenye uongozi lakini vizazi vyenu vinachukiwa, siku mkitoka je! Usiku mwema.
 
Hii tabia ya viongozi wa Afrika kung'ang'ania viti inatokana na vicious cycle ya kisasi. Aliyepo madarakani anajua alimfanyia mabaya aliyepita, na anajua anayekuja atamfanyia yeye mabaya pia. Huwa hawawazi kabisa habari ya kujenga taasisi imara, huwa wanawaza kujilinda wao wenyewe na matumbo yao kwanza.

Ni kama wanajitengenezea jela yao wenyewe, maana kulazimika kubaki madarakani kwa nguvu nao ni utumwa fulani hivi wa kisaikolojia.
 
Maridhiano ni yale CCM wakitoka madarakani waombe wasifunguliwe mashitaka, mali zao zisitaifishwe na wasiwekewe vikwazo

Jambo ambao sio rahisi kuwasikiliza
 
Back
Top Bottom