Wanasimba, Derby ya Afrika ni kati ya Mamelodi Sundowns vs Al Ahly

Kilimbatz

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
4,331
Reaction score
5,865
Nimeona Wanasimba wengi wakiongozwa na yule mshereheshaji wao wa kule mtandao wa X wakijifariji kuwa wapo kiwango kimoja na Al Ahly.

MC wao wa Twitter Ndugu Micky Jr anawapamba kuwa mechi ya Simba vs Al Ahly iwe African Derby, ahaa!

Derby ambayo kabla ya mechi unakuwa ushajua nani anashinda na kuendelea mbele? Derby gani, mpinzani wako anapopangiwa na wewe anafurahia badala ya kuogopa? Derby gani, mpinzani miaka nenda rudi anakufanya wewe ngazi ya kupandia? Tena kama haitoshi wewe unajisifu kuwa yeyote anayenifunga au kunitoa anakuwa bingwa?

Al Ahly alikuwa anaomba piga ua garagaza asikutane na Mamelodi Sundowns. Al Ahly anamwogopa Sundowns kwani anaupiga mpira mwingi hadi unamwagika, ana rasilimali fedha na mjuzi wa figisu.

Najua pona ya Al Ahyl ni kuomba Mamelodi Sundowns apigwe red card, tena wapigwe kadi kuanzia wachezaji watatu ndio atashinda

Njoeni mjifunze kwa kaka yake Yanga jinsi ya kumbandua Al Ahyl nje ndani.

 
Mamelodi anaweka mechi yake ya nyumbani saa 9 kwenye jua. Anakubaliwa

Timu zetu zikiweka mechi ya nyumbani saa 9 kwenye jua zinakataliwa

Caf wana upendeleo. Sababu rais wa caf ndie mmiliki wa mamelodi.

Hata Simba angecheza na Al ahly kwenye jua la saa 9. Simba angeshinda goli nyingi
 
Kikubwa tupambane tupande viwango vya CAF ili tuwe na sauti ya kimaamuzi

Mamelodi ashindwe mwenyewe safari hii

Al Ahly kaja mwenyewe gheto
 
Saa nyingine huu ushabiki wa simba na yanga unataka kuwatoa watu akili.

Simba na Al Ahly wamekutana mara 6 na kwenye mechi hizo kila timu imeondoka na ushindi mara 2 dhidi ya mwenzake na zingine 2 wamedroo,sasa hiyo hoja yako ya kusema eti simba na Al Ahly wakikutana basi mshindi wa mechi anajulikana unaisema kwa misingi ipi?
 
Game ya Simba isingewezekana kuchezwa saa 9 kumbuka ilikua ufunguzi
 
SI ndo hapo tim zote zko sawa ,,,jitu kama hili la utopwinyo lisilo tumia akili linaropoka,,, linajisahaulisha mwez ujao yatakutana nao tuone kam hat sare tu yatapatq
 
Currently simba na al ahly wamekutana mara nane simba kashinda mechi 3 na al ahly kashinda 3 wame toa sare 2 sasa huo ukibonde wa simba uko wapi lete takwimu za head to head za al ahly na simba kwa miaka mitatu iliyopita maana mpira ni mchezo wa takwimu weka hapa ili twende sawa.
 
Ndugu Mbumbumbu haliya hewa kule bondeni south ni tofauti na uku kwetu East.
Kule kwao ni kama Iringa tu, mechi inaweza kuchezwa saa saba mchana na wachezaji wasitoke jasho.
Kuna hali ya hewa ya baridi na jua kwa mbali.
 
Umeandika Ukweli Mtupu, yaani watu wamebakia kufurahi "Kufa kiume"

Hicho ndicho walichobakiwa kusema [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kweli kabisa kama ilivyo sasa NBC league... derby ni Yanga na Ihefu
 
Umeandika Ukweli Mtupu, yaani watu wamebakia kufurahi "Kufa kiume"

Hicho ndicho walichobakiwa kusema [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Aahaaaa

Ukweli usemwe
 
Kweli kabisa kama ilivyo sasa NBC league... derby ni Yanga na Ihefu
Aahaaa
Ni bora derby ya Yanga na Ihefu kuliko Al Ahyl na Simba

Matokeo yake yanatabilika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…